Rev.Kishoka
Platinum Member
- Mar 7, 2006
- 4,527
- 1,555
Much said bro, but recently you have been very vague about where you stand.
i have never been vague about my stand at all. What I don't agree with many is the selective-ness of whayt may be endorsed as kosher/halal or not!
Vyama vikuu CCM na Chadema (Ukawa) vimevunja kanuni zao na kufanya maamuzi ya kidikteta kuidhalilisha demokrasia, katiba na hata kanuni.
Ila kilichofanywa na Chadema na Ukawa kinashikiliwa bango kubwa sana kama kesi ya mauaji huku lile la CCM linanyamazishwa kuwa kilikuwa kitendo cha kishujaa. Huo ni UNAFIKI!
Leo mgombea wa Ukawa Lowassa anashinikizwa Ufisadi zaidi, Richmond inashikiwa bango kubwa na vitisho vya mengine hatuyasemi.
Ufisadi wa Magufuli wa nyumba za Serikali, uzembe kusimamia wizara na kufanya wizara kuongoza kwa wizi na hujum na hata maamuzi yake mabaya ya kukamata samaki, watu tunalazimishwa tuyafukie chini ya zulia na mkeka na tunaambiwa huyu ndio atakayesawazisha nchi: huo ni UNAFIKI mkubwa.
Kuna mahusisho ya Udini, Lowassa na Uluteri na Gwajima wake kila mtu anaamka na kudai huyu atatuletea udini, lakini ya chinichini ya Magufuli hata ya Lukuvi kuhubiri na kupanda mbegu chafu za udini, yanamwagiwa maji ya sabuni.
Tukubaliane kuwa kama mtu hamtaki Lowassa na aseme hivyo na si kulazimisha ya ufisadi, maana hata Magufuli ni fisadi na waliomweka hapo kama chaguo na kuacha watu waadilifu kabisa wasio na tuhuma ni mafisadi wakubwa.
Sitasimama kwenye Unafiki wa aina yeyote, ndio maana nasema tuchambue ilani na sera na si kupotezeana muda kuchambua mgombea huku haramu tupu imetumika kuleta wagombea na wagombea wenyewe wana najisi na uharamu!
That is my stand bro!