Twitter Mbili za Mo Dewji na Mustakabali wa Simba SC

Mk54

JF-Expert Member
Dec 29, 2016
1,997
3,933
1. Je ni kweli Mo anajaribu kuwa mkubwa kuliko timu ya Simba SC; au ni kweli Mo akiachana na Simba SC, timu hiyo itayumba na kukosa mustakabali elekezi?

2. Je kuna mafanikio gani ambayo Simba SC imeyapata chini ya Mo; kwa mantiki kwamba haikuwahi kuyapata miaka ya nyuma kabda ya Mo?

3. Yeye kama Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi; kuna haja ya kuleta kwenye mitandao mambo ambayo yanaweza kujadiliwa kwenye kamati? Katiba ya Simba inasemaje ikiwa Mwenyekiti wa Bodi anataka kujiuzulu? Je alifuatisha utaratibu huu ? Je yupo juu ya katiba ya Simba ?

Je Wajumbe wa Bodi walipewa Taarifa in advance au Social Media ndiyo ilitumika kama official information kwa wajumbe wake? Ameivunjia Bodi nidhamu? Je kuna haja ya kuhojiwa na kamati ya Bodi ?

Je anapaswa kulazimishwa kujiuzulu kwa ukosefu wa nidhamu na maadili ya utumishi wa Simba SC ?

4. Je kuna anayefahamu sababu nyuma ya pazia ya bwana huyu kuwa Muwekezaji at the same time kuwa mwenyekiti wa Bodi? What is the secret behind ?

5 . Mbona siku zote anawasimanga wana Simba juu ya Bili 20??? Lakini hazungumzii kile anachochuma kupitia mgongo wa Simba SC !

Aidha, Wengi walistushwa na Twitter mbili za Mo; Moja akijiuzulu kama Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi.
IMG_1195.JPG

Na nyingine akijirudisha kwenye Uenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi simply kwa kusema it was unfortunate.
6c96396a-3e1e-4f78-9396-81b3959c7ec9.jpg

Kuna haja ya Serikali ya Jamhuri kulitizama hili kwa jicho la tatu. Naelewa dhamiri ya dhati ya Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania chini ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa, ndugu Pombe Magufuli kutoruhusu mtu mmoja kuwa na Hisa zaidi ya 49% kwenye Klabu hizi mbili za Simba na Yanga.

Hizi ni Klabu zenye historia ya Tanzania na haitoweza kutokea klabu hizi kupoteza dira hata siku moja kwa kumkosa mtu au jamii fulani. Ifahamike kwamba Klabu hizi zote zimepitia Financial Crisis kwa nyakati tofauti na hakuna iliyoanguka.

Aidha, Mo alilalamikia kuhusu Bilioni 4 zinazolipwa wachezaji ambao wanashindwa kufanya kama matarajio yake; ( lakini sio matarajio yake; ni matarajio ya wana Simba). Bilioni 4 ni pesa ndogo sana kwenye Mpira kwa vilabu vingi Barani Africa; Ni pesa ambayo haikuweza hata kumuhamisha Makusu kutoka As Vita kuja Simba SC.

Halikadhalika, Simba ina umri zaidi ya Umri wa Mo na Uwanja wa Bunju ulikuwepo kabda ya Mo; marekebisho na ujenzi unaoendelea ni kutokana na fedha zinazoingizwa na Klabu ya Simba SC, sio fedha kutoka mfukoni mwa Mo D.

Kuna Malalamiko mengi ndani ya Klabu kuwa Mo anajaribu kuwa mkubwa kuliko Simba kwa Investment yake ya 20 Bil ambazo mpaka sasa hakuna anayeelewa amezi invest wapi na vipi. View attachment 1327081

Taarifa iliyoandaliwa na kocha Mkuu wa Simba, Patrick Uchebe ilisisitiza baadhi ya Wachezaji wasiondoke lakini Mo akasisitiza atakuja na wachezaji wake wazuri; Ndio hao Wabrazili pamoja na Shibobo matokeo yake yeye ndiyo kuwa sababu ya Simba kutolewa nje ya michuano kwenye hatua za awali kabisa kitu ambacho hutokea nadra sana kwa Vijana hao wa Msimbazi.

Hata makocha wanaoletwa kwenye Klabu; wengi wao wanakuwa na influence ya Mo pasipo kujali uwezo halisi wa kocha na Background yake. ( Mfano ni huyu Kocha mpya; hata rekodi zake haziridhishi). Hii ni hatari sana kwa Ustawi wa Klabu.

Hivyo; kupitia Twitter 2 za Mo;

—Kuna haja ya Serikali ku review 49% ya Mo ikiwa ni pamoja na kufanya amendment ya figure tajwa hapo juu. Tenda itangazwe kwa wanaotaka kuwekeza katika asilimia zitakazo baki na si ajabu Hata Mbwana Samatha akataka kuwekeza.

—Ukomo wa mtu mmoja kumiliki Hisa za Klabu hizi uwe at-most 15% only. Ili kutoa nafasi kwa watanzania wengine wenye nia thabiti ya kuwekeza kwenye Klabu;

—Samba samba na hilo; Muwekezaji hatopaswa kuwa Mwenyekiti wa Bodi; Muwekezaji abaki kuwa Muwekezaji ili kuzuia Personal Interest and Judgement kwenye timu.

—Aidha, Mapato yote ya timu as of Financial Year yawe wazi kwa wanachama wote wa Simba.

—Mwenyekiti wa Bodi ataajiriwa kama wanavyoajiriwa wafanyakazi wengine.

Hii itapunguza kuona kwamba mtu mmoja kwa fedha zake za kufikirika anaweza kufanya lolote kwenye Klabu na akaweza kuchochea maamuzi kwenye timu.

Mwisho, ukweli ni kwamba hata Mo akiondoka Muda huu timu itaendelea kuwepo kama alivyoikuta, na ataiacha kama ilivyoachwa na wengine.

Tweet zake mbili zimeonesha ni jinsi gani Mo alivyo Immature and he has no control over himself; he is not acting his age.

The Club itself isn't in the Control. Bodi ya Wakurugenzi ikiliacha hili lipite kimya; basi Bodi Ijitathmini Power na Authority ilizokuwa nazo over one person. Otherwise; Bodi Ivunjwe kwa sababu haiwezi kumuwajibisha mtu, nonsense!

Thank you !

On Date 18th January 2020
 
Attachments

  • IMG_1195.JPG
    IMG_1195.JPG
    33 KB · Views: 1
  • 6c96396a-3e1e-4f78-9396-81b3959c7ec9.jpg
    6c96396a-3e1e-4f78-9396-81b3959c7ec9.jpg
    39.7 KB · Views: 1
  • IMG_1197.JPG
    IMG_1197.JPG
    52.4 KB · Views: 1
Mafanikio waliyoyapata simba toka Mo ajiunge ni kuwa na uwanja wao wa tizi, kabla ya mo walikuwa wanakodi uwanja wa tizi
 
Mafanikio waliyoyapata simba toka Mo ajiunge ni kuwa na uwanja wao wa tizi, kabla ya mo walikuwa wanakodi uwanja wa tizi

Uwanja ulikuwa upo kwenye Plan. Uwanja unajengwa kwa pesa za klabu. Je unajua zile Bilion ilizopata Simba kwenye Robo Fainali zimetumika ?Yeye Mo atoe pesa zake mfukoni kwa faida gani ? Ushawahi kujiuliza hilo?

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nafikiri hatujaelewana mkuu, simba haikuanza kupata pesa leo lakini walikuwa hawajengi baada ya mo kuja wamejenga, kwa taarifa yako uwanja umejengwa kwa pesa za mo
 
Nafikiri hatujaelewana mkuu, simba haikuanza kupata pesa leo lakini walikuwa hawajengi baada ya mo kuja wamejenga, kwa taarifa yako uwanja umejengwa kwa pesa za mo

Kwahiyo Mo ndio katoa pesa zake kajenga Uwanja? Unamaanisha Uwanja ni wa Mo na sio Simba ?

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kwahiyo Mo ndio katoa pesa zake kajenga Uwanja? Unamaanisha Uwanja ni wa Mo na sio Simba ?

Sent from my iPhone using JamiiForums
Uwanja wa simba kajenga Mo, hivi unajua huo uwanja umepewa jina gani?
 
Uwanja wa simba kajenga Mo, hivi unajua huo uwanja umepewa jina gani?

Unaniuliza au unaniambia ninajua? Please be specific. And kindly inform us

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kwa kipindi hiki mo atake au asitake lazima awepo simba

Sent using Jamii Forums mobile app

Mimi nafurahi kuona Timu inapata muwekezaji wa kueleweka. Lakini pia nitafurahi kwa Watanzania wakifahamu kuwa Mo hafanyi kwa Ubure; anafanya kwa maslahi yake binafsi. Ni vizuri akibaki kuwa Muwekezaji.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Unaniuliza au unaniambia ninajua? Please be specific. And kindly inform us

Sent from my iPhone using JamiiForums
We githeri man huoni question mark hapo? Ok iko hivi uwanja ni wa simba Mo kawajengea kwa pesa zake, unaitwa Mo arena...
 
We githeri man huoni question mark hapo? Ok iko hivi uwanja ni wa simba Mo kawajengea kwa pesa zake, unaitwa Mo arena...

Ndiyo Muelewe kuwa mwenzenu yupo kibiashara. And Mark this post Brother time will tell.

Haiwezekani Uwanja uliotolewa na serikali tangu enzi za JK kwa ajili ya Timu kubwa kama Simba yeye kuipa Jina lake.

Watakapokuja kushindwana kati ya Simba na huyu Muhindi ndiyo mtakuja kuelewa.
IMG_1197.JPG

Kimsingi ni kutokujua kwako tu; uwanja umejengwa kwa mapato ya timu, na kama Mo alichangia basi ni asilimia chache sana tena amefanya hivyo kwa manufaa na sio kwa hasara. Hakuna muhindi anayefanya kitu kwa faida ya mtu fulani.

Umeishia darasa la ngapi frère? Je unajua Simba kama Simba inaingiza kiasi gani kwa mwezi? Na hizo pesa matumizi yake yapoje ? Bilioni walizopata kwenye Klabu Bingwa Africa, where are they ?

Why does he pretend that everything comes from his pocket, Ina maana hiyo Klabu haiingizi kitu?

Tatizo ni elimu au tatizo ni kutoelimika?

Haki wa TZ!
 
View attachment 1327658

Mwamba sielewi tunachobishana hapa ni nini? Simba walianza kujenga uwanja walipokwamia ndio Mo alipoanzia kwa pesa zake, kama anapata faida au hasara hiyo ni yeye na najua ni ngumu sana kufanya kitu kwa hasara
 
Mo apate hasara asipate hasara, we inakuhusu nini?
Kumbuka mpira ni kama siasa tu iliyojaa mbinu kibao, kwani yeye ku-post vile mtandaoni unajuaje kama ndo mbinu ya kuipa Simba mafanikio kwa kuwachanganya wapinzani wake.
Sote tunajua uwekezaji wa Mo pale Simba wapinzani wake hawaupendi, wanatamani Simba iwe kama yao.

Mbona huo uwanja wa bunju haukujengwa kabla ya Mo kuwekeza?
Nachelea kusema uwekezaji wa Mo tangu aje Simba umechangia more than 75% Simba kuanza ujenzi wa ule uwanja.

MAONI: NA nyie tafuteni muwekezaji wenu wa uhakika na siyo kubakia kupiga majungu club ya Simba
 
Back
Top Bottom