'TWAWEZA" pamoja na Kuwekwa Kati Na Wanaharakati, Wapinzani, Bado mmeonesha CCM NI Chama Dume

Trump2

JF-Expert Member
May 28, 2017
1,553
2,608
Nimeona Tweet ya Mwanadada Maria Sarungi akisema kuwa Magufuli na CCM yake wangeporomoka zaidi kama siyo hofu ya kushughulikiwa na dola.

Nadhani SARUNGI ameongea kinyume chake. Hapana shaka kabisa TWAWEZA wamewaogopa zaidi wapinzani na wanaharakati wakaona Wamshushe kidogo JPM na CCM.

tazama hapa:

TWAWEZA, Wakati wa kutoa ripoti yao:
1. Chombo cha habari walichotumia kuwa Mubashara ni 'Kwanza TV'inayomilikiwa na Maria Sarungi Mwenyewe ambaye ni mwanaharakati.
2. Ukimuondoa Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole, TWAWEZA waliwekwa kati na Maria Sarungi Mwenyewe(Mmiliki wa Chombo kilichowafanya wawe Mubashara), Jenerali Ulimwengu(Mwanaharakati), Fatuma Karume (Mwanaharakati).

Ni mtoto mdogo tu anaweza kudanganywa kuwa 'TWAWEZA' wanaweza kuingiwa na hofu ya Dola na siyo wadhamini wao na watu waliowaweka Mtu kati.

Kwa mtu asiyejua 'TWAWEZA' ni akina nani angeweza kufikia hitimisho kuwa ile haikuwa ripoti ya Utafiti bali lilikuwa ni jukwaa la Wanaharakati kutolea mapovu yao kwenda kwa Serikali.

Kwanini tusiamini kuwa Ripoti ile ilihaririwa kabla ya kwenda kwa walaji?
Maneno ya Humphrey Polepole kuwa 2020 wanaweza kushinda kwa 80% siyo ya kubeza.

Waione Maria Sarungi, Fatuma Karume na Ulimwengu

Mapumziko mema ya mwisho wa wiki.
 
Nimewahi kusema humu ndani...

Mtu akikuita wewe ni CCM wakati siyo atakuwa amekutukana tusi kubwa sana la nguoni.. Maneno haya bado yanaishi na mada hii ndio kielelezo..!!

BACK TANGANYIKA
 
Nimeona Tweet ya Mwanadada Maria Sarungi akisema kuwa Magufuli na CCM yake wangeporomoka zaidi kama siyo hofu ya kushughulikiwa na dola.

Nadhani SARUNGI ameongea kinyume chake. Hapana shaka kabisa TWAWEZA wamewaogopa zaidi wapinzani na wanaharakati wakaona Wamshushe kidogo JPM na CCM.

tazama hapa:

TWAWEZA, Wakati wa kutoa ripoti yao:
1. Chombo cha habari walichotumia kuwa Mubashara ni 'Kwanza TV'inayomilikiwa na Maria Sarungi Mwenyewe ambaye ni mwanaharakati.
2. Ukimuondoa Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole, TWAWEZA waliwekwa kati na Maria Sarungi Mwenyewe(Mmiliki wa Chombo kilichowafanya wawe Mubashara), Jenerali Ulimwengu(Mwanaharakati), Fatuma Karume (Mwanaharakati).

Ni mtoto mdogo tu anaweza kudanganywa kuwa 'TWAWEZA' wanaweza kuingiwa na hofu ya Dola na siyo wadhamini wao na watu waliowaweka Mtu kati.

Kwa mtu asiyejua 'TWAWEZA' ni akina nani angeweza kufikia hitimisho kuwa ile haikuwa ripoti ya Utafiti bali lilikuwa ni jukwaa la Wanaharakati kutolea mapovu yao kwenda kwa Serikali.

Kwanini tusiamini kuwa Ripoti ile ilihaririwa kabla ya kwenda kwa walaji?
Maneno ya Humphrey Polepole kuwa 2020 wanaweza kushinda kwa 80% siyo ya kubeza.

Waione Maria Sarungi, Fatuma Karume na Ulimwengu

Mapumziko mema ya mwisho wa wiki.
sidhani kuna aliyepata undue advantage kama CCM tangu JPM aingie madarakani:

- media zote "zimetekwa nyara" na CCM kupitia mwenyekiti wao
- matukio ya kiserikali yamekuwa yakitumika kuikampenia CCM kupitia mwenyekiti wao
- viongozi wa upinzani (wabunge & madiwani) wamekuwa wakirubuniwa na CCM wakati wote
- yote hayo yalikuwa ni kutaka kujiongezea umaarufu na kukubalika - badala yake ime back fire.

rudini kwenye drawing board!
 
Back
Top Bottom