Twafaa: Sukari bei juu, nyanya hazikamatiki sokoni

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Maisha yanazidi kuwa magumu mtaani baada ya bidhaa muhimu kuzidi kupanda bei.Mchele, maharage, unga,gesi bei zipo juu.

Sasa jana nilienda kununua sukari kwa mangi nikakuta bei imepanda tofauti na ilivyokuwa last week. Imepanda kutoka 2300 hadi 2800, shilingi 500 zaidi. Hili ongezeko ni kubwa sana kwetu walalahoi.

Juzi pia baada ya kuchoka nyanya ghali za gengeni, nikajitosha kwenda Soko la ndizi Mabibo kununua za jumla, haki nilichokuta huko ilibidi niwaachie laana watawala. Sado shilingi 8000 na ndoo ya lita 10 shilingi 12,000, shubhaamit. Niliachana nazo ngoja nikomae tu na za gengeni za jero jero kila siku.

----------Habari Gazeti la mwananchi----------
Screenshot from 2017-03-16 10-47-10.png

Bei ya nyanya katika siku mbili hizi haishikiki na sababu tatu za hali hiyo zimetajwa. Mosi ni mvua zinazoendelea kunyesha ambazo zimeathiri uzalishaji wake.

Nyingine ni wakulima kushindwa kumudu gharama za uzalishaji na mwisho ni hasara waliyopata msimu uliopita walipozalisha nyanya nyingi zilizokosa soko.

Bei hiyo imepanda katika baadhi ya masoko ambayo waandishi wetu waliyatembelea juzi Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya, Moshi na baadhi ya mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Jiji la Dar es Salaam, juzi kuanzia saa tatu hadi saa sita mchana, bei ya nyanya ilikuwa Sh70,000 kwa tenga wakati miezi mitatu iliyopita katika masoko ya Ilala, Buguruni na Kariakoo ilikuwa Sh25,000.

Mwenyekiti wa wauza nyanya Soko la Buguruni, Amos Mtala alisema bei ya nyanya kwa msimu huu imekuwa juu zaidi kutokana na baadhi ya wakulima kutoka Iringa na Njombe kushindwa kumudu gharama za uzalishaji.

Mwenyekiti wa wauza mazao ya jumla katika Soko la Ilala, Habibu Uroki alisema kilichosababisha bei kuwa juu ni kudoda kwa nyanya msimu uliopita na kusababisha wakulima kupata hasara kutokana na kukosa soko.

Katika masoko mbalimbali ya mjini Dodoma, zao hilo limepanda katika masoko ya Sabasaba na Majengo. Mwandishi wetu aliyetembelea masoko hayo kati ya saa tano asubuhi na saa saba mchana juzi alikutaka tenga moja likiuzwa kwa wastani wa Sh130,000 ikilinganishwa na Sh90,000 msimu uliopita.

 
Maisha yanazidi kuwa magumu mtaani baada ya bidhaa muhimu kuzidi kupanda bei.Mchele, maharage, unga,gesi bei zipo juu.

Sasa jana nilienda kununua sukari kwa mangi nikakuta bei imepanda tofauti na ilivyokuwa last week. Imepanda kutoka 2300 hadi 2800, shilingi 500 zaidi. Hili ongezeko ni kubwa sana kwetu walalahoi.

Juzi pia baada ya kuchoka nyanya ghali za gengeni, nikajitosha kwenda Soko la ndizi Mabibo kununua za jumla, haki nilichokuta huko ilibidi niwaachie laana watawala. Sado shilingi 8000 na ndoo ya lita 10 shilingi 12,000, shubhaamit. Niliachana nazo ngoja nikomae tu na za gengeni za jero jero kila siku.


Si ilikuwa 2,400 ilishuka lini?
 
Sukari labda imported, viwanda vyetu vinazalisha ya kutosha na nasikia ni Tsh. 1,800/- kwa kilo.
Mimi chai nimeacha kitambo.
 
People's power
Ndugu wananchi tumekuwa tukipambana ktk kuikomboa Tanzania kiuchumi, kisiasa na Kijamii.
Watanzania wenzangu ni muda wa mabadiliko. Tanzania tunakabiliwa na maadui 4 wa maendeleo nao ni ccm, ujinga, maradhi na umasikini.
-Wananchi ccm ni mzigo na kimeshazeeka na hakifao kuwepo madarakani.
Angalien watoto wenu mnaowategemea wamefutiwa ajira, je huyo raisi ana nia ya dhati kweli kuikomboa Tanzania? Chagua Chadema kwa Maendeleo yenu
Ajira za serikali zitakuwa zinatolewa mwezi wa 1 kwa kila mwaka tutaajiri watu weng sasa. Mkichagua Ccm mtabaki hiv hiv hakuna ajira. Huyo mnayemsifiwa kafuta ajira na hatoajiri. Nani kaajiriwa mpaka sasa?
-Suala la mikopo kwa wanafunzi limekuwa ni kilio, watoto wengi wanatoka ktk familia za chini. Onen watoto wenu wapo nyumbani sasa hivi na wamekosa mwelekeo kbsa. CHADEMA TUTATOA 50% KWA KILA MWANAFUNZI ANAYEINGIA CHUONI
-Suala la HELSB 15% tutarudisha ktk asilimia za mwanzo 8% na hii italeta haueni kwa wafanyakazi.
PEOPL'S POWER
Jaman ndugu wananchi increment zenu meshapewa? Nilishangaa sana watu weng bado wanakimbizana na chama kilichozoeeka na chenye mawazo ya kimasikini. !eo hii ni october 25, 2019 bado hamjapewa increment, hamjapandishwa madaraja. Polen sana kwa uhakiki wa wapiga dili wa ccm. CHAGUA CHADEMA KWA MAENDELEO YAKO
Walimu poleni sana kwa kupigishwa deki, huu uuonevu mnabid muukomeshe kwa kuichagua chadema. People's power
Huyo mliyemchagua kafanya nn mpaka sasa hivi?
Suala la vyeti feki siyo kama tunashabikia ila tunataka haki itendeke. Iweje wengine wafukuzwe lkn yy alindwe.
Ona sasa sukari mnanunua 1 kilo kwa 3,000.
Wanakagera mpoooooooooooooooooooo
"BILA KUMUONDOA ADUI WA MAENDELEO CCM MTAENDELEO KULIA KILA SIKU. HUYO MSEMA KWELI MPENZ WA MUNGU MBONA KADANGANYA UMMA? MWEZI MMOJA AU MIWILI UNA SIKU NGAPI? WATANZANIA MEJICHANGANYA SANA NA HII DHAMBI ITAWATAFUNA MPAKA KESHO KUTWA.
Najaribu tu Wala usiogope mwanaccm. 2019 itakuwa poa sana.
 
Si juzi tu hapa nyanya zilikuwa zinaharibika kwa kukosa soko?

Ndoo ilikuwa elfu 1000
 
Sukari labda imported, viwanda vyetu vinazalisha ya kutosha na nasikia ni Tsh. 1,800/- kwa kilo.
Mimi chai nimeacha kitambo.
Mkuu, kuna ile ya kupima na kuna iliyo kwenye vifungashio ya Kilombero na Kagera Sugar. Ya kupima ilikuwa 2,300 na kwenye vifungashio 2400 ila kwa sasa bei ni sawa. Labda kama mangi kanipiga.
 
mkuu kwanza pongezi nyingi kwako kwa kuamua kuwa mzalendo na kukosoa pale panapotakiwa kukosoa/kushauri..

Ukweli ni kwamba vitu vingi vimepanda bei madukani na masokoni pia, hela mtaani pia hamna na cha ajabu bei za bidhaa mbalimbali ziko palepale au kupanda zaidi, tukilalamika tunaitwa wapiga dili.......
 
Unasikia wapi? Sukaru ni kati ya 2400-2600 uku mtaani.
Mkuu, nakumbuka mwaka jana PM mwenyewe akitamka kuwa sukari isiuzwe zaidi ya 1,800/-. Tatizo mimi sijainunua tokea wakati huo na siamini kama kuna mfanyabiashara mtanzania anayeweza kukiuka agizo la waziri mkuu!
 
Back
Top Bottom