Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,936
Habari waJF kwenu mlio na raha,
Hali ya maisha inaendelea kuwa ngumu kila uchwao. Gharama za maisha zinazidi kupanda na uchumi bado uko pale pale.
Vyakula vinagusa familia zote, mmoja mmoja au kundi la wengi. Bei za vyakula kila siku zinazidi kupanda. Ukame nao unazidi kutamalaki. Siku hizi kusema Tanzania kuna njaa ni kosa la jinai, labda useme kuna upungufu kidogo wa chakula.
Baada ya bei ya mchele,unga na sukari kupanda sasa ni zamu ya mboga kuu ya Taifa tuliyoachiwa na Hayati Mwalimu Nyerere, mboga hiyo ni Maharage.
Maharage imekuwa mboga yetu ya kila siku, iwe mashuleni, gerezani, kambi za wakimbizi.Katika hali ya kushangaza bei imepaa kutoka Tsh. 2300 hadi 3000 (ongezeko la Tsh. 700). Bei ya Jumla ilikuwa Tsh. 2100 na sasa ni ths 2800.
Hii ni bei ya eneo ninalokaa Sinza la watu wa kawaida.
Huko kwenu sijui bei imekaaje?