TV Ya JF: We Thio Lafki Yangu Teena! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TV Ya JF: We Thio Lafki Yangu Teena!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by X-PASTER, Jul 12, 2010.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Jul 12, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  WE THIO LAFKI YANGU TEENA!

  NILIRUDI nyumbani jioni baada ya mizunguuko yangu ya kimaisha. Kwa kawaida mwanangu mdogo, Lubna, (jina la kitoto tunapenda kumwita Lu), hunikimbilia kwa shangwe kuja kunipokea, lakini siku ile nilishangaa alikuwa "kauchuna". Nikamuuliza: "Lu, vipi mwanangu?" Kimya! "Hujambo?" Kimya!

  Baada ya kumhojihoji ili kumdadisi nifahamu tatizo lilikuwa nini, alitoa maneno ya ukali akisema: "We thio lafki yangu teena!"

  Waliokuwepo waliangua kicheko na kusema tu, "Lu bwana!"

  Nilimuuliza kwa nini mimi sio rafiki yake, nikagundua sababu. Kumbe nilikuwa nimemfinya asubuhi kabla sijaenda kazini, kwa sababu alikuwa hataki kwenda shuleni (chekechea) eti kwa sababu alikuwa amechoka sana ile asubuhi.

  Nilichokifanya ni kutoa kafuko ambako ndani kalikuwa na vituvitu vya kutafuna, kama ilivyo kawaida nikirudi nyumbani. Nikasema: "Sawa kama mimi thio lafki yako".

  Lu alipoona kale kafuko akajua mna vitu. Akawa anatafuta suluhu. Akaja mbio huku akisema: "Thalamaleku, baba!" Waliokuwepo wakaangua kicheko tena. Bila ya kuwajali waliokuwa wakicheka, alisema: "Nilikuwa nadanganya tu baba, wewe ni lafki yangu".

  Kwa nini alifanya hivyo? Alijua kwamba uadui wake kwangu ungemkosesha maslahi, walau kwa kipindi kile kifupi cha neema.

  Wengi waliokuwepo waliangua kicheko tu, wakiishia kusema: "Lu bwana!...Watoto bwana!... blah...blah...blah! Lakini kwa watu wa fasihi kila tukio lina maanisho (implication) katika maisha, na vile vile kwa watu wa fasihi maisha yote ni tamthilia (drama), unaweza kuyafanyia uchambuzi. Nilikuwa nafikiria niandike nini kwenye JF Leo, lakini tukio lile dogo kwangu likawa na maanisho kubwa zaidi katika maisha yetu leo kuliko wale waliokuwa wakicheka tu walivyolichukulia.

  Juzi hapa kuna kigogo mmoja wa chama fulani alikuwa amealikwa na chama tawala kuhudhuria mkutano mkuu wa Chama hicho Kizota, Dodoma. Alishangiliwa sana na wana CCM kwa nyimbo na vigelegele... Na inasemekana kuwa amesema kwamba CCM haikamatiki. CCM Chama Kubwa... Sasa baadhi ya wapinzani wanajiuliza, amesalimu amri!?

  Kwani mwaka 1995 alishindwa, mwaka 2000 aligaragazwa na Mh. Mkapa, na mwaka 2005 ndio kabisaa Kikwete akammaliza. Hivyo CCM ni chama imara, hakishikiki. "Kweli CCM inagaragaza upinzani".

  Mheshimiwa wa inji hii inasemekana aliongeza, "Kila mwaka wa uchaguzi inakula kwangu, sasa nimechoka" alisema kwa hamasa huku akiendelea kuisifia CCM na uongozi wake.

  Kwa maneno yake amesema, hana sababu ya kuacha kumsifia Rais Kikwete kwani ndiye Rais pekee anayemjua. Amefanya kazi kubwa sana katika kipindi cha miaka mitano hususan katika harakati za kupambana na ufisadi na mafisadi nchini.

  Zile hasira zake kwa chama tawala wakati ule zilikuwa za kweli au ilikuwa ni ile ile "we thio lafki yangu teena!"

  Sasa hivi kila kona unayokwenda watu wanalalamika hali ngumu za kimaisha, ufisadi kila mahala. Utamkuta mtu jicho limemtoka: "Hatukubali. Ngoja elfu mbili na kumi inakuja. Huyu sasa basi. Mimi kura yangu kwa dk Maslaha tu safari hii. Eeh, ndio! Mf€xyz%£*&! Kshxnz$!!! kabisa! Blah...blah...blah...!"

  Ukimkuta mtu utadhani mkali kweli, lakini ngoja fulana na vitenge vitolewe. Ona watu watakavyobadilika rangi. Angalia watu watakavyorudisha kadi na kuomba radhi. Cha kuchekesha, wengine ni wasomi wazuri na pia wapo wanasiasa wenye wafuasi wengi tu... Wapo pia mashehe na maaskofu. Wakati wa kaneemeka kwa muda mfupi ndio waja huo.

  Ukiwa nje ya mchezo ndio unafaidi. Miye sina chama lakini ninapo pa kupiga kura. Usiniulize wapi, kwa sababu wenye busara zao wameshatupa uhuru wa kuchagua tunapopapenda. Nauliza tu wale wanaojidai wana hasira, hasira hizo ni za kweli au ni zile zile za "We thio lafki yangu teeeeeena!" Vifuko vikitolewa tu, "Thalamaleku baba!"

  Haya, tutaona!
   
 2. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160


  Nachoweza kusema umezama na umefikiri sana. Lu ni binti mdogo maskini, lakini watanzania wapiga kura watu wazima na akili zetu hivi ni kweli fulana pilau na kofia ndo zinatufanya tusahau matatizo yetu ya kweli ya kila siku na kukimbilia raha ya siku mbili na shida za miaka mitano.

  Inaumiza, Anyisile alisema kweli watanzania ni shake well before use

   
 3. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  shukrani mkuu, Lyatonga thio lafki yangu teeeeeena
   
 4. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  X Paster,

  We subiri tu oct 2010 ikiwa inakaribia.
  Wadanganyika bana!!!
   
 5. m

  matambo JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 728
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  well said kaka, wewe kweli ni mwanafasihi na mfano ulioutoa ni halisia kabisa,wengi wetu tumekuwa 'victims' wa vijizawadi na takrima bila kutambua ni maumivu kiasi gani ya kufinywa tutayapata kesho asubuhi.
  laiti kama watanzania tungejitambua leo sisiemu isingekuwa na jeuri ya kuita wafanyakazi mbayuwayu au kukiuka ilani yake yenyewe
   
 6. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #6
  Jul 13, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Toa hii hapa peleka huko kwenu kwenye jukwaa la siasa.

  Hapa ni Gaucho, AC Milan, Azzurri, wozza, champions league, NBA, Muziki na burdaan ningine.
   
 7. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #7
  Jul 13, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ndio maana wakaitwa Watanzania... Itachukuwa nusu karne kubadilika kama si karne nzima.
   
 8. m

  magee Senior Member

  #8
  Jul 13, 2010
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35

  kauli hii ndo inawaumiza wengi......mimi naipambanua kwa mapana zaidi mbali na kupewa vizawadi kuna hata kupewa kauli za vitisho zitakazo kufanya unywee tu na kuwa mpole ndugu yangu mfano mzuri wafanyabiashara wengi wasipoisapoti ccm inakula kwao,mara waanze kufuatiliwa kama kodi wanalipa mara waambiwe sijui vibali gani hawana ,yaani taabu tu..........ukweli jamaa wameshika mpini na sisi tumeshika makali,wakivuta tu imekula kwetu.what we need is to fight for total liberty maana bila hio kila siku tutakuwa watuwazima tunaotishiwa nyau!!!!!
   
 9. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #9
  Jul 14, 2010
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Beautiful narration.

  Mkuu, kila ulichokisema hapa ndicho kilichopo na ndicho kitakachotokea ifikapo wakati wa kupiga kura. Ni dhahiri kuwa watu wengi wenye heshima na wasio na heshima nyingi na wenye hasira na matendo waliyofanyiwa na watawala wa leo, wataanza kujipendekeza na kuomba suluhu kwa kufanya kile wasichokusudia kukifanya. Hivyo ndivyo tulivyo.

  Nilikuwa nasoma Ilani ya uchaguzi ya CCM yenye kurasa kama 135 hivi. Katika maelezo marefu sana yaliyotolewa, nikagundua kuwa mengi ni taarifa za kupikwa na ni exaggerations za hali ya juu. Zimewekwa hivyo ili watakaotaka kuzisoma, walewe mafanikio na mipango ambayo kama kweli ingetekelezwa kwa kiasi hicho, tusingekuwa na lawama. Lakini la msingi ni kuwa, wanajua hakuna wa ku-challenge maelezo hayo kwasababu ni wachache wenye nia na uwezo wa kukaa na kuyasoma. Pia, hakuna chombo cha kufuatilia ukweli na uongo uliopo. Mafanikio mengi yaliyotajwa yalikuwa ni yale yaliyopatikana miaka mitano ya mwisho ya awamu ya tatu.

  Turudi kwenye simulizi ya "wewe thio lafki yangu teeeena". CCM inajua bayana kabisa ni t-shirt ngapi zinatosha kumlaghai mtoto abadili msimamo. Na sina uhakika kama kweli mtoto hataki kilichomo kwenye mfuko ulioshikwa na baba yake.

  Mimi nimeshaamua na hakuna lawalawa wala t-shirt itakayo badili msimamo wangu. Ninachotafakari ni je, msimamo wangu unaweza kufanikiwa kwa kuwa na wafuasi wengi? Na hata usipofanikiwa, itakuwa faraja tu kwangu kuonyesha nimefanya nilichoamua bila kuyumba wala kutetereka. Wewe thio lafki yangu teeeena.
   
 10. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #10
  Jul 22, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kuna aja ya Watanzania kuamka kutoka kwenye usingizi mzito...!
   
 11. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #11
  Jul 22, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  X-paster,

  Hii makala yako imeende shule. Sikutaka kuisoma mwanzo kwa kufikiri ni ya kitoto......

  Umeniacha hoi na huo mfano hai wa Bi Lu. Msalimie sana na tafadhali mchukulie weekend kifuko cha zawadi kwelikweli. Kunako majaliwa siku moja ntakurudishia hela na mwambie alichokifanya, kimetoa shule nzuri. I wish Mrema angelikuwa hapa asome.
  I wish hao VINYONGA wote watakaosema "nazitaka mbichi hizi za KIJANI watafikria mara mbili.

  Lazima niseme nasubiri nyingine.
   
 12. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #12
  Jul 29, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Insha'Allah... nyingine zipo zaja...!
   
Loading...