Tv station taifa za afrika ni wapambaji wa watawala

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
122,488
96,053
Wana bodi hivi sasa natazama ubc tv wanaonyesha jinsi museven alivyokuwa anaanza kupigana na wapinzani wake hadi kuingia ikulu,wakati hiki ni kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wiki ijayo,hivi kumbe hata tbc nawao lazima watekeleze matakwa ya watawala
 
Hii ndio silaha ya utawala uliochokwa na wananchi, utawala unaolazimisha kubaki madarakani, kuudanganya uma kwa nguvu kubw kuwa wao ndio wafaao, badala ya kuacha matendo yao kwa jamii iwabebe na kuwapa ushindi, aibu tu ni kuwa vyombo vinaendeshwa kwa kodi za wanyonge.
 
Tanzania hali uwa mbaya zaidi kwa sababu StarTV, Channel 10, Clouds TV zilikuwa zinatekeleza maagizo ya makada wa chama tawala nakuacha ITVDaima pekee kuwa sehemu pekee utamuona Hashim Rungwe Spunda, Mama Anna Mghwira, na UKAWA sana. sasa ukienda TBC ndio ungeweza amini upinzani ni MAGAIDI
 
Yaani hivi vituo vya tv vya taifa sidhani kama hao wakurugenzi wake wanapatikana kwa kufuata sifa za nafasi hizo,zaidi ya ukada wa chama tawala
 
Uliona alichokutana nacho Tido Mhando alivyoendesha TBC kwa uweredi na taaluma yake?
"wajibu wako kuyatenda yanayompendeza aliyekupeleka, na haki yako ni kupokea mshahara na posho"
usifikirie heshima yako katika jamii bali vitu viwili "wajibu wako, na haki yako"
 
Tanzania hali uwa mbaya zaidi kwa sababu StarTV, Channel 10, Clouds TV zilikuwa zinatekeleza maagizo ya makada wa chama tawala nakuacha ITVDaima pekee kuwa sehemu pekee utamuona Hashim Rungwe Spunda, Mama Anna Mghwira, na UKAWA sana. sasa ukienda TBC ndio ungeweza amini upinzani ni MAGAIDI
Lkn naamini kama ni fedha wanapata kipindi kile cha uchaguzi tu maana kwa sasa hivyo vituo ulivyo vitaja tofauti na kwa sasa wanaonja machungu ya undumila kuwili maana wateja wao wengi wamewatupa mkono sasa wanatangaza vipindi vya mabingwa wa miti shamba na wale mabingwa wa kuombea na kutoa mapepo
 
Uliona alichokutana nacho Tido Mhando alivyoendesha TBC kwa uweredi na taaluma yake?
"wajibu wako kuyatenda yanayompendeza aliyekupeleka, na haki yako ni kupokea mshahara na posho"
usifikirie heshima yako katika jamii bali vitu viwili "wajibu wako, na haki yako"
Niliona mkuu yaliyo mtokea ila ni ktk mwendelezo ule ule wa ubabe na ufisadi wa kutumia rasilimali za taifa kwa manufaa ya watawala bila hata ya uoga
 
Kwanza naomba kuweka wazi kwamba SIJIVUNII KUWA MUAFRIKA , halafu ndio nije kwenye hoja yako , ni hivi , ukiacha Kenya , tv stations za nchi nyingi za africa na hasa chini ya jangwa la sahara wanatumia ulimbukeni wa wananchi wao kuwatizamisha sifa feki za viongozi ili kuwarubuni waendelee kuwachagua , tazama RT ya Rwanda au MBC ya malawi utacheka !
 
Televisheni za taifa hazina tofauti sana na SHOW za vikatuni "pika bom puppet show" ya Startv TAARIFA YA HABARI YA MKOLONI.
 
Back
Top Bottom