TV Show Mpya: FAMILY FULL MAPESA

Rogart

Member
May 5, 2011
6
2
Hodi hodi wanajamvi.

Kwanza napenda kuwapongeza kwa kazi mnayoifanya ya kujadili na kuchambua masuala ya taifa letu. Iwe inahusu masuala ya kisiasa, kiuchumi, kijamii au kimahusiano, moto wenu ni ule ule tu. Hongereni sana. Mnatufungua macho wengi wetu ambao tumekuwa wasomaji kwa muda mrefu sasa.

Sasa mimi jamani napenda kuwatangazia TV PROGRAM yangu mpya. Program hii ni gameshow na inaitwa FAMILY FULL MAPESA. Ni program ya kijamii ambayo inaenda hewani kupitia kituo cha STAR TV kila JUMAPILI saa 12:30 -1:00 jioni. Ni program mzuri sana ambayo inalenga kuburudisha, kuelimisha, kugusa hisia, pamoja na kugawa “vijisenti.”

Hapo chini, nimebandika sehemu ya episode moja kwa ajili ya utangulizi kwenu. Kuweza kuona kipindi kizima, vijavyo, pamoja na picha mbalimbali za utengenezaji wa hiki kipindi, tafadhali tembelea SAHIHI ENTERTAINMENT

Mlango wa maoni, maswali, mapendekezo, na makosoaji siku zote utakuwa wazi. Mnaweza kuwasiliana nami hapa hapa au kupitia email zifuatazo: rogart.mmole@gmail.com na rmmole@hotmail.com.

Karibuni sana

[video=youtube_share;Y4v1oejey5g]http://youtu.be/Y4v1oejey5g[/video]
 
Yule mtangazaji is HOT!!Hiyo ndo sifa pekee nnayotoa maana nliboreka na maelezo ambayo kila mwenye akili angeelewa bila kurefushwa vile so sikuendelea kuangalia.Kazeni buti labda na mie ntaleta familia yangu kushiriki mkiahidi maelezo hayatakua mengi vile!
 
Ahsante Lizzy kwa maoni yako.

Labda tu ningekuuliza kama unazungumzia ile episode ambayo host alikuwa peke yake akielezea mtiririko wa show? Kama ni hiyo, basi ililazimu kutengeneza ile special episode kwa ajili ya kuwaelewesha watazamaji. Kwa sababu, watazamaji wengi walikuwa wanawasiliana nasi kujaribu kuelewa vizuri. Kwa hiyo ndio maana tukaamua kutengeneza ile episode.

Vinginevyo, show yenyewe hiko very interesting. Brain ya hii show ni jinsi maswali ya show yalivyokuwa structured. Maswali ambayo yanatokana na ishu za kawaida tunazokumbana katika jamii yetu kila siku lakini uwezi kudhani mtu anaweza kutenga muda na kutengeneza maswali ya show.

Pia, usisite kuileta familia yako kuja kushiriki...:)

Karibu sana!
 
Yeahhh hiyo ndo nlikua naongelea!Kesho ntajaribu kuangalia hizo nyingine basi nionje ladha ya kipindi!!

Nwy ukitaka kushiriki unafanyaje?!
 
Rogart kazi yako ni nzuri ,hasa nikiiangalia kwa upeo wa siku za mbeleni,Naona utafanya kazi maridhawa kabisa-WELL DONE!! Ila Artist design ya studio yako inatuacha hoi sana!!Hizo impression haziendani na mvuto wa kile unachotuonyesha.Hebu jaribu kupata studio nzuri zaidi.Wale jamaa wa Benchmark najua wana studio za kisasa kabisa,Pamoja na kwamba ndo umeanza kijasiria mali pia jaribu ku team Up na watu wazoefu zaidi wanaweza kukupiga tafu mwanangu ukatoka kiukweli kweli. BIG UP MY BROTHER is a good try keep It Up!
 
mi nimewahi kuiona ka mara moja tu! Sio mbaya is a good start, ila kuna mambo fulani unabidi urekebishe kama aina ya maswali yawe open questions ila tricky ili kuminimize guessing mengine ni usomaji wa maswali wale participants wanatakiwa kusoma maswali from screen ambayo juu yake inakua na camera same as kwa mtangazaji asishike karatasi and some time u've to include few audience for applause na vitu ka hivyo. I like those shows saaana kama utakuwa interested niko tayari kuaandaa maswali ambayo ni entertaining, simple, and logic which measures knowledge for free ila ni wewe tu kusema yatoke ktk mfumo upi na ya mlengo upi nina ka xperience kidooogo ka quiz and ans reality shows nimeparticipate zain african challenges tanzania qualfiers hadi tournament Uganda as a player and as a coach
 
nafkiri pia mfumo wa mchezo unaweza ukaupanga upya hebu jaribu kuangalia series za reality shows za questions and answers like whowants to be a millionaire, weakest link, zain african challenges na temptatio Nigeria they will give you many different ideas kifanye kipindi chako kibambe na kiwe hot si bongo tu hadi East Africa uone ka multi choice hawatakutafta otherwise good luck comrade
 
Yeahhh hiyo ndo nlikua naongelea!Kesho ntajaribu kuangalia hizo nyingine basi nionje ladha ya kipindi!!

Nwy ukitaka kushiriki unafanyaje?!

Kuna namba ambazo huwa zina scroll wakati wa kipindi. Hizo ndio namba za kuwasiliana nasi. Lakini kwa kifupi ili kushiriki inabidi timu ya watu 5 wanaohusiana kindugu wajikusanye. Ndugu wanaweza kuwa ndugu wa damu, wakambo, na mpaka wakwe (shemeji, wifi, na nk). Hakuna gharama yoyote ya kushiriki.

Ahsante
 
Rogart kazi yako ni nzuri ,hasa nikiiangalia kwa upeo wa siku za mbeleni,Naona utafanya kazi maridhawa kabisa-WELL DONE!! Ila Artist design ya studio yako inatuacha hoi sana!!Hizo impression haziendani na mvuto wa kile unachotuonyesha.Hebu jaribu kupata studio nzuri zaidi.Wale jamaa wa Benchmark najua wana studio za kisasa kabisa,Pamoja na kwamba ndo umeanza kijasiria mali pia jaribu ku team Up na watu wazoefu zaidi wanaweza kukupiga tafu mwanangu ukatoka kiukweli kweli. BIG UP MY BROTHER is a good try keep It Up!

Kiroroma,

Ahsante kwa mchango wako.

Set za studio nimezi-design mwenyewe. Ni mabango tu nimeyatengeneza ambayo naweza kuyasimamisha popote pale..hata sebuleni...lol! Anyway, idea yangu ilikuwa ni kutengeneza set ambayo itavutia "mtanzania wa kawaida." Unapofanya hizi shughuli inakubidi uzingatie mtanzania wa kawadia anataka kuona au kusikia nini. Na ndio maana hata jina la show nimeweka kichombwezo "Mapesa"ambacho mtanzania wa kawaida kinaweza kumvutia kirahisi. Lakini the main idea ya show sio kumwaga mapesa, bali ni kuelimisha, kuongeza upeo wa kufikiri, pamoja na kufurahisha. Lakini nilipokuwa nafikiria jina la show, ilibidi nifirikirie jina ambalo linaweza kuwa na mvuto kwa mtanzania. Sasa kwa sababu kwenye jina kuna neno la "Mapesa", basi sikuwa na budi bali ku-design set ambayo ina picha za noti..lol. Vile vijitu viwili ni logo ya kampuni yangu ya entertainment ambayo inaitwa Sahihi Entertainment.

Ahsante
 
mi nimewahi kuiona ka mara moja tu! Sio mbaya is a good start, ila kuna mambo fulani unabidi urekebishe kama aina ya maswali yawe open questions ila tricky ili kuminimize guessing mengine ni usomaji wa maswali wale participants wanatakiwa kusoma maswali from screen ambayo juu yake inakua na camera same as kwa mtangazaji asishike karatasi and some time u've to include few audience for applause na vitu ka hivyo. I like those shows saaana kama utakuwa interested niko tayari kuaandaa maswali ambayo ni entertaining, simple, and logic which measures knowledge for free ila ni wewe tu kusema yatoke ktk mfumo upi na ya mlengo upi nina ka xperience kidooogo ka quiz and ans reality shows nimeparticipate zain african challenges tanzania qualfiers hadi tournament Uganda as a player and as a coach

System ya maswali ni open. Haihitaji kufika chuo kikuu kuweza kuyajibu yale maswali. Ni maswali yanayohusu mambo tunayokumbana nayo kwenye jamii kila siku.

Kuhusu system ya usomaji maswali - hii show ina fit kwenye category ya reality show. Kwa hiyo idea ni kuwaruhusu washiriki na host wajiachie, ikiwa ni pamoja na kuwafanya washiriki wasikilize kwa makini host anaposoma maswali badala ya kukazania kuangalia kamera. Pia, flow mzima ni ya host kuzunguka na kutamba. Kwa hiyo isingekuwa rahisi kwa host kusoma maswali kutoka kwenye screen fulani na hapohapo kuweza kutamba kwenye flow.

Kuhusu kuhusisha audience - mpango wa kuhusisha audience upo. Ila tu kwa mwanzo, director wangu alishauri tuanze bila ya audience ili kujenga confidence kwa host. Mara tu confidence ikikaa sawa, basi audience wataanza kuwa introduced polepole.

Nashukuru kwa ofa yako kusaidia kutunga maswali. Karibu. Kumbuka tu nahitaji maswali ambayo yako kwenye mfumo wenye majibu mengi, i.e. swali liwe na jibu zaidi ya moja. Maswali yawe yanalenga ku-entertain, ku-educate (ku-bring awareness), na ku-inspire. Sasa hivi nina maswali karibu 2000 kwenye bank yangu ya maswali. Nakaribisha mengine zaidi.

nafkiri pia mfumo wa mchezo unaweza ukaupanga upya hebu jaribu kuangalia series za reality shows za questions and answers like whowants to be a millionaire, weakest link, zain african challenges na temptatio Nigeria they will give you many different ideas kifanye kipindi chako kibambe na kiwe hot si bongo tu hadi East Africa uone ka multi choice hawatakutafta otherwise good luck comrade

Iidea yangu imetokana na reality gameshow inayoitwa Family Feud. Hii ni gameshow ya siku nyingi sana huko U.S. Hata U.K. nao wana version yao inayoitwa Family Fortune. Kwa hiyo mfumo wa FFM ni mmoja wa mifumo ya Q&A gameshows kama hizo ulizoziorodhesha.

Multi-choice niko nao sambamba kwenye Magic channel mpya ya kiswahili. Kwa hiyo muda si mrefu FFM itaanza kuruka huko, Mungu akipenda.

Ahsante kwa mawazo mazuri.
 
Back
Top Bottom