Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 57,103
- 128,718
Hii ni TV Program Alert, ambapo Tume ya Taifa ya Uchaguzi, inashiriki katika maonyesho ya kilimo ya Nane Nane katika uwanja wa Mwl. J.K Nyerere mjini Morogoro.
Ushiriki huo wa Tume ya Uchaguzi kwenye Maonyesho, ni fursa nzuri kwa wale wote wenye madukuduku kuhusu Tume kama ni tume huru, na uchaguzi, kama ulikuwa huru na wa haki.
Kwa vile sii wote wataweza kutembelea banda hilo huko Morogoro, kwa faida ya wengi, nimetembelea banda hilo, na nitarusha vipindi maalum vya banda hilo ndani ya Nane Nane na PPR.
Leo Waziri Mkuu ametembelea banda la Tume, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva, Makamisha Mary Longway na Athina Omari, pamoja na msimamizi mbobezi, Spora Liana, watazungumzia uchaguzi uliopita.
Usikose kuangalia mfululizo wa vipindi vya Tume ya Uchaguzi kwenye Maonyesho ya Nane Nane, kipindi cha kwanza kinaanza leo saa 1:00-1:30 Star TV.
Kesho ni Channel Ten, keshokutwa ITV kisha TBC.
Karibuni msikie na kushuhudia jinsi ambavyo huwezi kudanganya matokeo ya uchaguzi wa rais, hivyo msidanganywe na viongozi wa vyama vya siasa kuhusu bao la mkono kwenye matokeo ya urais!, hakuna kitu kama hicho!.
Paskali
UPDATE.
Kwa ambao hawakukiona kipindi hiki kiliporushwa kwa mara ya kwanza, leo na kesho, kuna fursa ya kuangalia marudio.
Leo Ijumaa, 05/08/2016, kipindi kitarudiwa Channel Ten, saa 2:30 usiku huu.
Kesho Jumamosi, 06/08/2016, kipindi kitarudiwa ITV saa 12:30 jioni!.
Wewe kama mwana jf, be the first to know!.
Paskali