Tuzungumzie asili yetu

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
227
333
Umewahi kusafiri umbali mrefu kwenye basi ukakaa na yule mtu kutoka mwanzo wa safari hadi mwisho kila chakula kinachopita dirishani kikiuzwa yeye husema nipe hicho, mpaka mnanafika ana rundo la vyakula anashindwa hata aweke wapi?

Au wewe ulikutana na yule ambae kila kituo cha kupumzika lazima aende kuchimba dawa arudi na vinywaji kwapani kama mwalimu wa hisabati na ubao wa lura?

Tuachane na hayo leo tujikite kwenye jamii zetu na utamaduni wa ulaji wa vyakula.

Bila shaka kila jamii ina utamaduni wake wa ulaji aina fulani ya vyakula kulingana na upatikanaji wake ingawaje watu wa mjini hula wao kinachopatikana sokoni.

Ukimuuliza mtu wa kigoma "ugali wa lowe" ni kitu gani ataacha shughuli anayoifanya akusimulie utamu wa ugali huo wenye mchanganyiko wa viazi.

Wanyamwezi hawaiti tena Lowe wao wana jina la kipekee huuita "Matoborwa" ingawaje ni aina ileile ya chakula kinacho lingana na lowe kiuandaaji na upishi.

Niseme nini kuhusu watu wa Tukuyu na kile chakula chao "kifughe"? hebu tuketi nikusimulie simulizi za vyakula vya asili.

Katika jamii hivi karibuni kula vyakula vya asili ni kama uganga wa kienyeji watu wanashika kichwa au kiuno wakikuona unakula bila hofu.

Jamii inaamini kwenye kukaangiza zaidi kuliko kuchemsha au kuchoma.

Nimethubutu kuwauliza watoto wa hapa Tukuyu, mkoani Mbeya walio zaliwa miaka ya 2000 waniambie kuna aina ngapi za ugali?

Wengi wakaniona mjinga ninae uliza swali jepesi wengi wao wakajibu zipo mbili tu Sembe na dona hakika nimecheka.

Hii inaonyesha dhahiri kuwa jamii imekuwa ya ki-mayai mayai mno watoto wanalishwa vitu vya dukani na viwandani.

Nimemkumbuka Mwalimu wangu nikiwa sekondari yeye aliyekuwa na utamaduni wa kufungasha kiporo cha dona na mikate ya kikinga akikisweka mdomoni pindi aendapo kazini.

Yako wapi sasa?
"Kipindi kile ukiwa na safari mama au bibi anakuandalia mkate wa mahindi mabichi maarufu kama Kisyesye, ili ule mpaka mwisho wa Safari" aliwahi kusema kusema Francis Mwalugaja mhenga mmoja wa Mwakaleli.

Utamaduni huu haupo kwa sasa badala yake wasafiri hupoteza maelfu ya fedha kununua miguu ya kuku na chipsi pale Comfort hotel wakeinda Dar es na mikoa ya pwani.

Nikajiuliza tena iwapo watoto hawa hawajui aina za ugali, itakuweje nikiwaambia kuna ugali unaotokana na ndizi si wataniona mshirikina.

Haya ni matokeo hasi ya maendeleo ya jamii, tumepoteza uhalisia sambamba na kuweka rehani afya zetu.

Mboga zetu za asili zimepotea tumehamia kula chainizi "Chinese" viazi havinogi tena tunakula chipsi hii ni ajabu sana.

Babu yangu hayati Kajubili alipanda mimea jamii ya viazi vikuu "Vitughu" nilimuona mtu mwenye kutulisha madudu kwakua havikua na radha na ukijaribu kuweka chumvi umeharibu.

Lakini hivi Sasa nimeanza kuamini kuwa wazee wa zamani walikuwa na maono juu ya afya zetu na walijaribu kutufundisha ili mbeleni tuishi vema.

Tudumishe utamaduni wa asili wa vyakula ili kuzilinda afya zetu.

Peter Mwaihola
 
Sikuhizi hata wale mama zetu,bibi zetu au hata wake zetu,ambao walikua na utaalamu wa kupika vyakula asili nao hawapo tena....saiz hata ukila ugali wa viazi ni kama umekula spaghettin
 
Maisha yanabadikika.Watu uhama makazi kutoka mkoa hadi mkoa na huko hubadili hadi mfumo wa kula na kuishi kwa ujumla.Hakuna anayependa kula makapi/junk-food.Yanawakuta tu kutokana na mazingira.
 
ata wazungu karne izo walikuwa ivvyo ivyo na mawazo kama yako ila mifumo na zama zimewabadirisha.

nafuatiliaga sana YouTube channel ya Ibrahim Onami akiwa nchini marekani, uko ulaya vyakula artificial zimekuwa nyingi, ni full GMO, mifumo ndio inayotubana,

ukipanda zao la kitu asilia linachukua miezi 6 adi uvune, lakin GMO inachukua miez miwili ad kuvuna, utachagua kipi kukimbizana na soko lako.
 
Vyakula kama rosholooo,viberee,kiburuuu,ng'andee,ng'ararumu,machalali,ugali wa dona na maziwa ya mtindi,pembeni parachichi umeponda ponda kwenye bakuli,mchicha wa kienyeji mafuta unatumia karanga,vyakula vyote.nimevimiss
 
Back
Top Bottom