mwandiga
JF-Expert Member
- Dec 5, 2011
- 1,506
- 664
Kwanza nianze kwa kutoa pole kwa wafiwa woote wa ajali ya gati la Lucy Vicent. Mungu azilaze roho za wote mahali pema.
Katika uzi huu sina nia mbaya ya kumsema mtu au kusmea biashara ya mtu. Kengo ni kusaidia jambo kama hilo lisitokee kiuzembe. Nitatoa mfano mmoja hai. Pale Kasulu kuna shule moja ina magari ya Njano aina ya Isuzu journey 3 juzi wameleta basi kubwa moja. Yale mabasi 3 ni mabovu kupindukia. Mengina unakuta vioo hata 3 havipo watoto wananyeshewa na mvua. Hayo magari 3 kila siku lazima yawe gereji kutokana na ubovu. Upakiaji wa watoto kwenye hayo mabasi ni shida kubwa sana. Basi linapakia watoto zaidi ya 50 na barabara ya kwenda shule ni mbaya saaana. Kwa ubebaji ule ikitokea ajali lazima wafe watoto wengi sana. Haifurahishi kubeba watoto vile. Vyombo husika vipo vinaona vinakaa kimya. Nimesikia Arusha leo polisi wanataka ku,filisha mkuu wa shule ya Lucy Vicent mahakamni kwa kupakiza wanafunzi 38 badala ya 30 kwenye gari lilipata ajali sasa hili linalopakiza 50 je.
Naomba vyombo husika chukueni tahadhari kwa haya mabasi lisihe kutokea tena.
Maeneo mengine mnaweza kusemea hali ikoje wahusika wachukue hatua