Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Kwanza nampongeza Lowasa kwa hizo tuzo alizopata. Binafsi nimeridhika na natembea kifua mbele kujisifu na kukisifu chama changu cha CCM kwa kuwajenga wanachama na wafuasi wake katika misingi ya ustaarabu na siasa za staha. Kama mwana CCM mstaafu, naamini kuwa Lowasa amelelewa katika misingi ya siasa za ushindani na si siasa za chuki na ugomvi.
Pamoja na hayo, sina hakika kama hadi mwaka 2020, Lowasa ataendelea kuwa na nguvu za kushiriki siasa. Natarajia kuwa baada ya kupokea Tuzo hizo, Lowasa atarejea kwao Monduli kuchunga ng'ombe kama alivyotuahidi hapo awali. Akifanya hivyo atazitendea haki hizo tuzo.
Binafsi naziona tuzo hizo kama ni mkono wa Kwaheri ama kwa jina jingine tumezoea kuita Rambirambi kwa kuukosa Urais kwani sitarajii kumuona tena Lowasa akisimama majukwaani kuomba kura kwa wananchi. Natumia fursa hii kumtakia kila la kheri katika kazi yake mpya ya kuchunga ng'ombe, kazi ambayo ndiyo jadi yake. Huku kwenye siasa ni kama alipotea njia tu