Tuziangalie ajali za barabarani

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
670
We are just consumers! People who are only consumers are parasites

Leo niangalie kwenye mambo ya usafirishaji nchini.

Waliounda vyombo vya usafiri wanafanya tafiti kila leo ili kuhakikisha wanapunguza kiwango cha ajali lakini mtu anawahi kufika aendapo hili ndio swala kubwa

Miaka kadhaa nyuma, magari yalikuwa na carrier juu, na mizigo ikawa inakaa juu, hii ilisababisha ajali nyingi, wanafizikia wakaona magari huanguka sana kwa kuwa carrier ziko juu na hivyo watengenezaji wakaanza kuweka sehemu ya chini ya kuwekea mizigo ili gari isiyumbe sana na kupunguza ajali.

Madhara ya ajali yalizidi kuonekana, kuna kipindi mkanda ulikuwa ni kwa dereva pekee, hivi sasa mikanda ni hadi kwa abiria, yote hii ni kupunguza athari za ajali kwa watumiaji lakini pia kuwafanya wawahi kufika waendapo

Kama mnakumbuka kabla mikanda haikugunduliwa ilikuwa ni rahisi kukuta mtu amerushwa mbali na gari yake na tukasema ni jini amefanya hivyo,mara nyingne walitokea vioo vya mbele. Yalikuwa ni masuala ya MOTION tu

Leo hii zimegundulika hadi gas bags ili kupunguza uwezekano watu wanaokaa mbele kuumia. Bado Ugunduzi zaidi unaendelea ili kufanya raia wafike waendapo kwa haraka bila kupata madhara makubwa barabarani

NINACHOPINGA

Kwa tanzania, ajali ikitokea watu humuacha askari polisi azungumzie ajali hiyo na wote wamekuwa wakisema mwendo kasi! Mwendo kasi! Hali iliyosababisha watu kuamini na hivi sasa ni inakera kuona safari ambayo mwanzo ulisafiri kwa masaa mawili, hivi leo unasafiri kwa masaa manne, sababu kubwa ikiwa ni kuzuiwa kufuta dashboard hata kwa maeneo ambayo hayana makazi ya watu, tochi! tochi!

Je ni kweli ajali zinasababishwa na mwendo kasi tu!? Barabara mbovu na mambo mengi yanaweza kuwa yanachangia vitu hivi lakini sisi tumeamua kusema kuhusu mwendo kasi pekee.

Nia yetu isungwe kwenye watu kufika salama, bali salama na haraka.

Kama mnahisi kufika salama na haraka ni vibaya basi hata miradi ya mwendo kasi, DART na SGR haina maana, magar hayo ya mwendo kasi yanapata abiria wa kutosha kwa sababu watu hutaka kuwahi kufika wanedapo

ANGALIZO

Haya masula ya kutaka watu wasitembee kwa speed kwa kuangali jambo moja huwa na madhara mengi kiuchumi, wengine hulazimika kutumia ndege, wasio na uwezo hulazimika kufuta ratiba zao nyingine ili wafanye kitu kingine, au sis wengine tunaona tusafiri usiku ili kufidia kidogo

USHAURI

Ajali inapotokea, askari athibishe kutokea kwa ajali hiyo ila sababu za kutokea kwa ajali hiyo ziwe ni ushirikiano wa wataalamu wa higways, watu wa usafiri na wahandisi wa magari

Ili tufanye usafiri uwe ni wa kufika haraka na salama

Naweka wazi kabisa mimi ni muumini wa mwendo kasi barabarani. Sikubaliani na speedlimits tulizowekeana

Signed

OEDIPUS
 
Back
Top Bottom