Tuweke vituko vya watoto wetu hapa

Tuweke vituko vya watoto wetu hapa

Zero IQ

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
13,985
Reaction score
25,204
Tuweke vituko vya watoto wetu hapa ambavyo wewe kama mzazi ulimuona au unaona mtoto wako anafanya.
Chaweza kuwa cha kuchekesha au kukufanya ufikirie tu kwa nini mtoto wako kafanya hivyo .

Mi kituko nilichoshuudia kuna mtoto wa Jirani hapa ukisahau sabuni tu dakika sifuri tu imeshaliwa na huyo mtoto,
Yaani ni wa kumuangalia sana ni one mistake one goal.

Nb;Lakini licha ya vituko vya wanetu ni vituko hivyo hivyo ndivyo vinatufanya tuinjoi sana kuwa na familia .

Weka cha mwanao hapa.
 
6070b2bc201a851866ca4f1586dd63b6.jpg
 
Kuhusu kula sabuni ni hatari kwa afya mkuu! Watoto wanahitaji ulinzi madhubuti
 
Ndugu hapa ninapoishi kuna mtoto wa kiume muda wote analia hadi mamake amshike dudu ndo anatulia.Yan ni kero aseee
Hiyo ya kushika dudu ni Noma siku ataombwa anyonywe
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Viko vingi saaaana, ila Leo nasimulia hiki kilichonifundisha sana

Kuna siku mdogo wangu aliye na miaka miwili alifumwa na mother akichora ukutani kwa kutumia maua flani hivi mekundu. Mother alimmaindi dogo mixer kumtia kipondo then akampa order kuwa hayo marangirangi asiyaone.

Dogo akasepa ndani huku akilia akatoka akiwa na kikombe cha maji. Akaanza kupamwagia huku akifuta kwa mkono wake mwingine. Nilivitiwa na ile response yake na nikaamua kuanza kumchukua video. Kiukweli alifanya kwa moyo huku akilia kwa kwikwi na pia sehemu aliyokuwa amechora ilikuwa ni ya juu hivyo alikuwa anapata shida kufikisha maji lakini aliendelea kukomaa. Maji yaliisha akafata mengine, tulishindwa kuvumilia ikatubidi tucheke. Alirudi tena na akamalizia then akaja kumuonyesha mother kuwa amemaliza.

Mother akampongeza na kumkumbatia...naye akatulia tuli huku akifuta kamasi baada kupokea kipindi. Video ntajitahidi kuitunza ili akikua aikute...

Ila siku hiyo nikapata picha kuwa yesu aliposema ili tuion mbingu ni lazima tuwe kama watoto, alikuwa na maana pana sana.
 
...Some years back nilikuwa kwenye daladala nimekaa na dada mmoja na mtoto wake wa about 4 yrs. Sasa wakati mama analipa nauli kwa konda (alitoa elfu kumi) mtoto hakuona, alikuja kuona mama anapokea chenji toka kwa konda. Aisee ghafla yule mtoto akatamka ' mama leo naenda kumwambia baba unachukua hela kwa watu, ntamwambia baba, ntamwambia...' aisee basi zima liliangua kicheko...
 
Daaaaah, noma xana
 
Watoto nao wana vikao vyao vya kila siku...!

Huwa nina tabia ya kuwafuatilia nyendo, kujua Mada yao/zao...nini maazimio yao...!! Malengo n.k..
f74ccb65afe2b8b4d3c9d3a4603df608.jpg

Hapa ndipo watoto wanapojenga urafiki, na kumbukumbu nzuri za baadae katika maisha yao...
 
Mimi kamwanangu kana vituko vingi sana, ana miezi 6 sasa. Kulala halali mpaka apewe rushwa ya aidha kubebwa au anyonyeshwe, Siku nyingine anaamka usiku wa manane na kutaka kucheza na wazazi.
Anaboa ila analeta raha.
 
...Some years back nilikuwa kwenye daladala nimekaa na dada mmoja na mtoto wake wa about 4 yrs. Sasa wakati mama analipa nauli kwa konda (alitoa elfu kumi) mtoto hakuona, alikuja kuona mama anapokea chenji toka kwa konda. Aisee ghafla yule mtoto akatamka ' mama leo naenda kumwambia baba unachukua hela kwa watu, ntamwambia baba, ntamwambia...' aisee basi zima liliangua kicheko...
Hahahah miii mwenyewe uku nmeangua kiçheko
 
Kuna mtoto wa kike hapa kitaa akilia ukitaka anyamaze unampa hela..usipompa utabembeleza hadi uchoke
 
Wakati nilipokuwa nakaa kwa ankoo.alikuwa na mtoto Wa kike alikuwa na miaka kama mitano.
Sasa alishazoea kuniona na simu ndogo.
Kuna siku nikanunua simu kubwa.akaniuliza una simu mbili.
Nikamjibu hapana Bali ile ndogo imekuwa kubwa.akakataa akaniambia simu haiwezi kukua sababu haina miguu wala mikono wala Roho.
Mimi nikabaki na msimamo wangu ule ule kuwa simu imekuwa
Sasa baada ya siku kama tano.alikuja chumbani kwangu akanikuta na simu zote mbili.
Akaniambia MJINGA WEWE.
Unasema simu imekuwa wakati hiyo hapo.
Nikabaki nacheka tu.
 
Sisahau siku tulioalikwa chakula cha mchana
Watu kibao hapo ndio msosi umetengwa watu wanaanza kula
Kwa bahat mbaya kuna mzee mmoja ushuzi ukamtoka wa kimya kimya
Yulle mzee akajikausha harufu ilivozidi yule mtt nliokua nimekaa nae karibu
Akaongea kwa nguvu huku akimsonta kwa kidole“HUYU MZEE NDIO KAJAMBA”
Chakula kilinipalia[emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom