Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,987
- 20,271
Kaka yangu Prof Kitila Mkumbo, mimi nakuheshimu sana kama mtu msomi na mweledi wa hali ya juu, ninafurahi kuwa na bahati ya kufanyakazi na wewe katika siasa.
Unatambua wazi kuwa rais alivunja katiba na sheria za nchi kutangaza marufuku ya vyama vya siasa kufanya shughuli za kisiasa, hili kama Prof msomi ulitakiwa kumshauri rais kwamba anavunja katiba.
Hakukuwa na sababu za amri hiyo ya kirais katika nchi ya kidemokrasia inayofuata mfumo wa vyama vingi, isipokuwa tu kunapokuwa na vita katika nchi au hatari yoyote inayoweza kupimwa kwa Def Cond walau 001 hivi. Kitendo cha wewe kushindwa kumshauri rais vizuri juu ya hili, kiliondoa uhalali wako katika taifa juu ya mapambano yako ya miaka mingi kuhusu Demokrasia, yaani taifa halijanufaika juu yako katika hili kwa mtu uliyepigania demokrasia kwa miaka zaidi ya 30.
Rais akasema Wabunge tu wakuchaguliwa na madiwani ndio wafanye mikutano yao. Zingatia Mkutano wa kibunge sio wa chama cha siasa, ni mkutano wa kiutumishi. Hivyo John Heche hajafanya mkutano wa Chadema, amefanya mkutano wa Kibunge. Hili usipotofautisha utakuwa huna tofauti na akina Chakubanga tu.
Bashiru, Polepole, Pinda na makada wa ccm wengine nchi nzima wanazungunga nchi nzima wanafanya mikutano ya hadhara ya ccm huku wao sio wabunge wala sio watumishi wa umma bali wanaccm. Wakati huo Mbowe ambae ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa au Mashinji ambae ni Katibu Mkuu wa Chadema hawaruhusiwi kufanya mkutano wa hadhara Dar au popote na hata jimboni kwa Mbowa anazuiwa na polisi.
Tumia taaluma yako kulisaidia taifa kuliko kujali maslahi binafsi huku taifa likiangamia kwa ubaguzi nakulijaza chuki za kisiasa zisizo na ulazima.
Na Yericko Nyerere