Tuwe na wabunge wa jimbo la kitaifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuwe na wabunge wa jimbo la kitaifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mrekebishaji, Jul 12, 2009.

 1. M

  Mrekebishaji Senior Member

  #1
  Jul 12, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 168
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Lianzishwe jimbo jipya.(Kuwe na wabunge wa Kitaifa)

  Ndugu zangu, mimi ni kijana ambaye wakati wote nimekuwa nikiamini kuwa kuna vitu vikubwa viwili ambavyo vinategeneza au kuharibu maisha ya mwanadamu. Hivi ni SIASA na DINI.

  Ktk imani hii, nilikuwa napenda kufuatilia na kushiriki ktk mambo hayo. Kuthibitisha hilo, wakati nasoma Mlimani, nlipata kuwa DARUSO President mwaka 2004/2005.


  Leo nina hoja ya ubunge wa kitaifa. Ktk tafakuru yangu, nimekundua kuwa kuna wabunge ambao wapenda maendeleo wanawahitaji lakini kuna hatari majimboni kwao wasikidhi matakwa ya jimbo. Kwa mfano kuna majimbo wanahitaji huduma za jamii, lakini inawezekana mbunge wao bado hana uwezo wa kutekeleza hayo kwa kadri ya mahitaji ya watu wake.Lakini utakuta mbunge huyo huyo ni kinara wa kupinga ufisadi jambo ambalo linasaidia nchi kwa ujumla nap engine jimboni kwake watu wakaona si tija sana kwao.

  Sasa, nasema kwa wale wapenda maendeleo, naomba tuangalie namna ya kupenyeza hoja, tupate wabunge walau 10 wa kitaifa hawa wachaguliwe na wapiga kura wote kama ilivyo kwa tiketi ya urais. Kwa maelezo mafupi, tusipofanya hivi, mafisadi wanaweza kutuondolea kwa urahisi watu kama Dr. MWAKYEMBE, MAMA KILANGO, ZITTO, DR.SLAA, SELELI na wengineo ambao wameonekana kuwa na uchungu na nchi pengine kulingo hata majimbo yao tu.

  Pia, kwa vijana wengi wengi(watoto wa wakulima) bado hawajakusanya kipato cha kutosha kupambana na ‘wakongwe’ japo hao vijana wanauwezo mzuri lakini kwa bahati mbaya siasa zetu zinahitaji zaidi pesa kuliko uwezo wa mtu ktk kutetea jamii.

  Naombeni kuungwa mkono au kukosolewa.

  (KWA MAONI YANGU WABUNGE HAWA NI MUHIMU KULIKO HATA WALE KUMI WA MH. RAIS)

  Asanteni.

   
 2. A

  August JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Ni nchi gani Duniani umeona ina mfumo huo?
  Pili Raisi wety ana influence barabara ijengwe Chalinze Mkata Segerea na ndio Kiongozi wa wa nchi, itakuwa hao wabunge wa Kitaifa, nao si wanasehemu wanazo toka?
  Kitu kikubwa ni kuwa na vision na principle za kutekeleza miradi, usimamizi etc.
   
 3. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Inaelekea sana na hoja nzuri kabisa ,lakini ukumbuke kunahitakika uwiano kati ya Zanzibar na Tanganyika ,upitishaji wa majina ya wabunge hao katika ugombea nafasi hio halikadhalika nini nguvu ya wabunge hao pale bungeni au watakuwa sawa na wabunge wengine ,ambao kazi ni kupiga kofi na hata kukitokea kupingwa kwa hoja mwisho wake hao wapingaji wanaunga mkono ,je watakuwa na kura ya veto ? Pia sijaona nini kazi ya wabunge hao au labda sijafahamu vizuri ! Nimehisi labda kuwa baadhi ya wabunge wapiganaji ndani ya bunge hawatochaguliwa tena ila kwa kupitia huku kwenye Jimbo la kitaifa wataweza kupita kutokana na kueleweka na Watz wengi.

  Nikirudia bado vipi wataweza kutupatia faida ikiwa watarudi kama wabunge wa Jimbo la kitaifa ,ukizingatia nguvu na mikakati wanayoionyesha sasa ,huwa hakuna mwisho unaomfurahisha mpiga kura ,kwani huundwa tume na kamati na mwisho wake ni kapuni. Huoni kama nalo hili litakuwa kundi la mafisadi kivyake.
   
 5. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  MWIBA,
  Mimi sioni umuhimu wa huo uwiano.
  Kusisitiza uwiano ni kulazimisha watu kukubaliana na itikadi fulani.
  Au siyo?
   
 6. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Hakika mawazo ni mazuri sana. Mimi wazo langu ni kufanya mabadiliko makubwa sana ya kikatiba kama sio kuandika katiba mpya inayoendana na maisha halisi ya WaTanzania.

  Mfano mdogo ni kuwa kwa mujibu wa KATIBA ya TANZANIA na hata ile ya ZANZIBAR. MBUNGE ANAWAKILISHA CHAMA PALE BUNGENI NA WALA HAMWAKILISHI MWANANCHI ALIYEMPA KULA ya kuingia Bungeni.

  Sasa tukiwa na Wabunge wenye kuwakilisha wananchi waliowapa kura hii itatoa uhuru zaidi kwa wabunge kuwa wakweli na wataacha unafiki
   
 7. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #7
  Jul 12, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hapana ,ukiangalia harakati hapo bungeni utaona wabunge kutoka bara hawajawahi kuzungumzia au kuhoji au kulalamikia mambu ya Zanzibar lakini Wabunge kutoka Zanzibar wanakuwa wanauliza na kuhoji mambo yalioko huko mikoani utafikiri ndiko walikochaguliwa ,lakini hakuna jingine ila ni uzalendo wao kuwa wao wapo hapo kwa ajili ya WaTanzania wote na si WaZanzibari peke yao ,hivyo kutokana na imani ya uwiano ikiwa ni kama nchi mbili zilizoungana basi ni vyema pakawepo nusu kwa nusu ,bila ya kuangalia wapi kuna mamilioni ya walio hai. Mimi nawahakikishia kuwa WaBunge kutoka Zanzibar wana imani kubwa sana na hawabagui wala hawaangalii yeye anatoka wapi ,ila huu ukiritimba wa CCM ndio unao wabana ,ila kama kutakuwa na nguvu fulani ya hawa Jimbo la Kitaifa ,mtaona mambo yao.
   
 8. Che Guevara

  Che Guevara JF-Expert Member

  #8
  Jul 12, 2009
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Hilo wazo ni zuri ila kwa sasa ni ngumu kwani itabidi lipitishwe na haohao walio madarakani...

  Nadhani cha muhimu zaidi ni kutumia Mahakama kushinikiza haki ambayo ipo tayari kwenye Katiba. Nayo ni haki ya mtu kugombea uongozi bila kuhitajika kupitia kwenye Chama chochote cha siasa. Wengine wanaita ni "Wagombea binafsi".

  Hiyo ndiyo more practical hata kwa uchaguzi wa 2010, kwani inasemekana ni kweli RA na wapambe wake wana mikakati ya kuwang'oa wabunge wanaopambana na ufisadi nchini.
   
 9. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #9
  Jul 12, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Umeeleweka mkuu.
  Tuzidishe harakati.
   
 10. A

  August JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
   
 11. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Sasa huko ndiyo kuto kuona mbali mkuu. Wewe sababu yako ya kutaka huo uwiano sawa ni kwa sababu ya ukiritimba wa CCM je siku isipo kuwepo CCM? Na huo uwiano uondolewe?
  Pia your idea doesn't make sense. Kazi ya wabunge ni kuwakilisha wananchi. Sasa iweje wananchi milioni moja wakaklishiwe na idadi sawa na wananchi milioni 40? Ni sawa na kusema sehemu fulani kuwa na daktari mmoja kwa kila wananchi mia na sehemu nyingine kuwa na daktari kwa kila wananchi elfu moja. kwako hiyo unaona ndiyo mfumo unaofaa? Na ikiacha hilo Z'bar bado watakuwa na wawakilishi wao wenyewe kutoka baraza la wawakilishi.
  Mfumo unaotakiwa ni kila mbunge mmoja awakilishe roughly idadi fulani ya wananchi na hiyo itaangalia population nzima ya Tanzania. Another option ni kuangalia landmass. Kuwa kila square kilometer fulani itakuwa na wawakilishi wake.
   
 12. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #12
  Jul 12, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  The Westminster Parliamentary system, which for historical reasons we follow, largely refrain itself to parliamentarians elected on district based constituencies rather than country wide proportional vote based constituencies (Israel and New Zealand are the only exceptions coming to mind, so to those asking which countries follow the country wide constituencies, I know of at least these two, though the comparison is a bit imprecise because these are not mixed systems as the proposed one).

  I would rather educate constituencies on national issues and cultivate a sense of sensible patriotism that will allow constituencies - rather than to be disenfranchised- to understand, even be proud of, an MP with nationwide issues at the forefront of his agenda.Moreover, there is absolutely no reason why any MP should not be able to emlpoy a healthy balance between local and nationwide issues, after all, as they say, all politics is local so even the national issues have local implications, however apparently indiscernible.

  Sometimes for the and long term vision to be implemented, some immediate and overly tangible rewards must be postponed.
   
  Last edited: Jul 12, 2009
 13. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Duplicate
   
 14. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #14
  Jul 12, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  MwanaFalsafa ,hapa kuna muungano wa nchi mbili, sio ukiritimba wa CCM,chochote kitakachoamuliwa kitakuwa ni lazima kwa hali yeyote ile kiwe na uwiano ,hivi unataka kunambia kwa hivyo unavyopiga hesabu Zanzibar inawezekana kabisa isiwe na hata mbunge mmoja katika hao Wabunge kumi au mkituonea huruma mnaweza kusema Zanzibar leteni mmoja au sivyo ? Halafu hapa kwa jinsi ilivyo hawa wabunge hawatakuwa ni kuwakilisha majimbo hawa watakuwa wasemaji wa kuu wa waTanzania wote,hapo utaona ile hesabu ya 1:4 inaondoka ,vilevile huko juu nilihoji namna ya wabunge hawa watakavyokuwa ,kabla hatujafika mbali ,ni nini nguvu ya wabunge hawa ? Au watakuwa kama waliopo na wao wapo tu ndani ya bunge hawana uzito wowote zaidi ya kupiga makelele ? Au ni kipi wanachoshindwa kukifanya hivi sasa na wataweza kukifanya iwapo watakuwa kumi bora zaidi ya tukionacho sasa cha kulipuwa mabomu na watu wakiyazima ? Hiyo ni point yangu muhimu kabla ya yote try to understand nonesense statement,hivyo nahitaji kujua nguvu ya wabunge hao kumi na si vinginevyo ,ili kuweza kuona umuhimu wa kuwa na watu hao kumi..
   
 15. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #15
  Jul 12, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mwiba,
  Kuwa na wabunge sawa toka Bara na Visiwani vitaongezaje hiyo nguvu ya wabunge? Nguvu ya wabunge imeainishwa kwenye katiba ya nchi. Kama wabunge wamekosa nguvu then it means ni katiba ndiyo inayo takiwa itazamwe lakini bado sijaona huo uwiano sawa utaongezaje nguvu ya wabunge. Maybe uexplain kidogo how you figure it will increase the power of the MP's.
  Hiyo ya Zanzibar kuwa nchi is a non issue and it doesn't make sense kwenye kila kitu basi kiwe 50-50 because Z'bar was or is a country. Wabunge ni wawakilishi wa wananchi. Z'bar will be represented maana itakuwa na wabunge wake. Na kama nilivyo sema Z'bar tayari ina baraza la wawakilishi. So kama fairness ndicho unacho aim wewe iweje Z'bar iwe na wabunge sawa na wa Bara na on top of that wananchi wa Z'bar wawe na extara representation kwenye baraza la wawakilishi? Hata kama zbar ilikua ni nchi kuna vitu watu mnabidi mconsider. Kuwa na muungano is all about compromises.
   
 16. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #16
  Jul 12, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu Bluray,
  Do you mind expalining what system Israel and New Zealand uses? Because sijawahi kusikia kuhusu mifumo yao so maybe you can educate those of us who didn't know.
   
 17. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #17
  Jul 12, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  The Knesset (Israel) and Paremata Aotearoa (New Zealand) do not use district based constituencies like most of the commonwealth legislatures, including ours, that are largely based on the Westminster Parliament. Instead they use what is proposed in this thread, nationwide constituencies (though the proposition is not to change the system, but to have a few members elected based on a countrywide constituency)

  In this system, all Israelis and New Zealanders elect all MPs. MPs are elected based on the proportion of nationwide votes they gather, there is no MP elected on a district based constituency.This way the concerns raised by this post are largely addressed because every MP has a nationwide constituency and there is no chance of a single MP being responsible for, say, the Malagarasi river bridge.
   
  Last edited: Jul 12, 2009
 18. M

  Mrekebishaji Senior Member

  #18
  Jul 13, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 168
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Wakati naleta hoja hii jamvini nimezingatia mengi lakini nina hofu kubwa kuwa pengine wengi hawajaelewa hoja yangu. Maana yangu ni kwamba maendeleo ya nchi kwa asilimia kubwa yanaletwa na wananchi wenyewe, lakini ukiangalia wabunge niliowataja wana-tija zaidi ktk taifa pengine kuzidi hata matakwa ya majimbo yao.

  Wakati ngazi ya kitaifa, kwa mfano hoja za kupiga vita ufisadi inaonekana kuwa ni muhimu kwa sasa ilim kulinda raslimali za kitaifa, unaweza kukuta mbunge kinara wa kupiga vita ufisadi hana uwezo wa 'ku-mobilize funds' za kutoshekeza miradi ya maendeleo jimboni kwake.

  Tukumbuke kwamba, kwa hali ya mtazania wa kawaida mbunge wanayemtaka at constituency level ni yule anayeweza kusadia jimbo na wenye uwezo huo wengi wao(si wote) ni wale ambao ni mafisadi. Angalia hata ambao tunawaita mafisadi kwa sasa, wengi wao wanakubalika majimboni mwao.

  Sasa, ugumu upo wapi, mimi nashangaa tumekubali Mh. Rais tumchague, halafu atuteulie watu 10, anyway si tatizo anahitaji 'wapambe' lakini kwa nini tusikubali kuwa na wabunge wa kitaifa.

  Kwa mf,Kuna mbunge mmoja kijana aliteuliwa na Mh. Rais, ukiangalia sidhani kama anafanya chochote bungeni, zaid zaidi posho zake zinampa kiburi na network na ukaribu na 'mkuu wa kaya' mpaka amekuwa akileta usumbufu usioo na maana mkoa M kwa kumfitini Waziri wa M na U, waziri ambaye aligombea hata urais mwaka 2005.
   
 19. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #19
  Jul 13, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Tatizo ni kwamba wale wanaotakiwa kutoa uamuzi juu ya jambo hili muhimu ni hao hao wanaowapiga vita wabunge wanaopambana na ufisadi. Nadhani ni wananchi tu(wapiga kura) wanaoweza kulipatia BUNGE letu la 2010 wabunge wenye mawazo ya kitaifa na wanaoweza kupiga vita ufisadi kwa masilahi ya taifa.
   
 20. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #20
  Jul 13, 2009
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mrekebishaji
  Gharama! Gharama kwa Watanzania, waoneeni huruma Watanzania masalaba wa hao 300 wanaouza sura Dodoma na madeni ya hao wachache wakutuwakilisha huko bungeni Afrika, yanatuacha na nguo zenye viraka. Tukiwaza tusisahau kupima faida na gharama
   
Loading...