Umeandika kwa hisia sana. Pole kama ulishakutana na miamba ya humu JF ukaishia kuambiwa "you are a wasted sperm!"
Ukweli hata hivyo ni kwamba kwenye kusanyiko la watu wengi kama hili, tena wasiofahamiana, watu hawawezi kufanana kwa sababu hata malezi yao na moral compass ni tofauti.
Wengine wana maumivu makali mioyoni mwao kutoka utotoni kwao huko. Wengine wana stress kali za maisha...Wengine hata wenyewe hawajipendi na hawana hata fununu kwa nini wapo hapa duniani. Umri unakwenda na wanaona hawapigi hatua yo yote ya maana katika maisha yao. Wote hawa wapo mitandaoni humu kujitafutia unafuu. Na njia bora kwao ni kujifanya wako juu sana kimaisha, kudogosha wengine na kuwaumiza. Hawa ndo ukiingia kwenye anga zao siku hiyo utajuta. Utaporomoshewa matusi hata kama hujamkosea. Ndo hawa unakuta mtu ameleta uzi yuko suicidal anaomba ushauri anaishia kuambiwa "nenda tu ukajiue kmmk kwanza huna faida yo yote hapa duniani". Hakuna ubinadamu. Hakuna compassion. Ila waki-log out hapa wanarudi kwenye uhalisia wao na moto wao wa mateso unaendelea kuwawakia.
Kwa vile siyo rahisi kuwadhibiti, jambo la muhimu ni kutochukulia mambo ya humu personal. Mtu akikuporomoshea matusi bila sababu jua kuwa mwenye tatizo ni yeye na siyo wewe. Na njia nzuri ni kumtia kwenye iginoa listi na kuachana naye mazima halafu unaendelea na mambo yako. Ukichukulia personal kila jambo mitandaoni humu kila siku utakuwa mtu wa kudhurika, kutukanana na mwenye hasira. Wewe unaumia kumbe yeye huko ndiyo furaha yake. It is not worth it.
Choose your battles carefully...
Don't take things personal...
Ignore and move on...
Fight if necessary....
Utaishi vizuri tu mbona?...