TUWE NA RUAHA AMA UDZUNGWA HEROES

Omary Sameer

Member
Oct 17, 2018
6
9
index.jpg

Taifa letu pendwa limekuwa na timu kadhaa za taifa katika michezo mbalimbali miongoni mwao ni za soka, mpira wa kikapu ,riadha, kuongelea na kadhalika.Mara nyingi timu za soka zimekuwa zikipewa majina mbalimbali, kuanzia ile timu ya wakubwa ya wanaume Taifa stars, Twiga ya wanawake, kuna Ngorongoro, Serengeti na nyingine nyingi.
Kuzipa timu zetu majina ya vivutio vya utalii ni moja ya njia ya kuvitangaza na kujivunia vivutio hivyo lakini kuna kitu nakiona katika majina hayo.
Majina mengi yanaakisi ukanda ulioendelea sana kwenye sekta ya Utalii na kwa bahati mbaya kuna baadhi yamerudia jina la mbuga moja kilichobadilishwa ni lile jina linalofuata Heroes na Warriors kitu ambacho kinanifanya nishauri tuite timu yetu hata Ruaha, Rungwe , Udzungwa , Serous ama Mikumi badala ya kukomaa na Ngorongoro pekee.


Naomba kuwasilisha....
 
Mikumi heroes si ndo hiyo inatoka Egypt mda wowote kuanzia sasa ina kikapu cha ndonga 23 kutoka kwa "wanaume kwelikweli"in jpm voice.
 
Back
Top Bottom