Tuwe na mmoja, za mwizi ni arobaini

Wakashina

Senior Member
Jan 12, 2014
134
23
Utakapobambwa na mpenzi wako tena kwa ushahidi kabisa utatamani ardhi ipasuke utumbukie ndani, Mimi naapa sitorudia tena maana yamenikuta mzee mwenzenu,,,,

kabla ya huyu wa sasa nimpendaye kiukweli nilishawahi kuwa na msichana mmoja anaitwa x ambaye kiukweli sikuwahi kumpenda kivile nilidumu nae kwa muda kama wa miaka miwili, alikuwa anataka sana nimuoe ila me sikumpenda na nilikuwa nafikiria namna ya kumuacha bahati nzuri nikafanikiwa kupata sababu na tukaachana rasmi. Pamoja na kumuacha lakini alikuwa amenogewa na penzi langu na me bila hiana nikamkubalia kuwa kila akijisikia anitafute nimridishe na me nikijisikia namtafuta ananiridhisha, tukakubaliana hivyo, kiukweli huyu binti alikuwa hana gharama kiupande wangu, tukikutana kuhusu nyumba ya wageni na misosi yote alikuwa anamaliza yeye kiasi ambachi sikuona shida.

Baada ya muda nilibahatika kupata mwingine ambaye nimempenda sana anaitwa y na yeye amenipenda kiukweli, binti ambaye hakujali historia yangu ya kimapenzi, nami nilimdanganya kuwa nilishawahi kuwa na msichana mmoja (nikamtajia msichana wangu wa kwanza ) na kumficha yule wa pili (x) kwa kuwa bado tunaendelea kuibana mpaka wakati huo. Mimi na y wangu tumepanga kuoana muda si mwingi sana, lakini kama ilivyoada sikuacha kukutana na yule dem wangu wa zamani kila nnapohitajika.

kuna sikunikiwa na y wangu mara ikaingia msg ya x na simu alikuwa nayo y, akaifungua ile msg na iliandikwa "Vipi tunaweza kuonana nimekumis sana ati", kwa bahati nzuri ile no sikuisave kwenye simu yangu kwa hiyo nikamdanganya kuwa atakuwa amewrong no, tukabishana sana ila mwishoni alinielewa na tukaendela na mapenzi yetu kama kawaida
Sasa kuna wakati nikasafiri kikazi na kuwa mbali na mpenzi wangu y, kwa jinsi ambavyo tunaamniana tukapena mapaka password zetu za facebook, mimi nilihakikisha nafuta msg zote za yule x kabla ya kufanya hivyo na nilimwambia x kuwa nshapata mpenzi wangu wa ukweli so aache kutumia fb atumie simu tu na asitume msg kali ntakuwa nnampigia au apige hata msg asitume sana.

Ghafla kuna siku y wangu akanipigia simu huku akilia sana nikimuuliza kuna nn y wangu analia tu huku akilalamika tu, kwamba kwa nini ninamfanyia hivyo nn ambacho kwangu ankosa? kwa nn nnamsaliti, ikanibidi na nnatoka na x, kwa kweli nilichanganyikiwa sana ikanibidi nikate simu kwanza, nikawa nafikiria amejuaje na nimjibu nn? mara akapiga tena nikahisi hana uhakika labda anapima tu nikapanga nimdanganye tena,nikabidi ning'ang'anie kuwa hakuna kitu kama hicho aliyemwambia amemdanganya, binti alilia sana kuwa namfanya yeye mtoto mdgo hana akila, akanambia kuwa ameona fb msg nilikuwa nachat na mshikaji wangu wakiume kuhusu huyo x tena hata wiki hazina sasa nitambishiaje? nikakumbuka kweli kuna jamaa yangu alikuwa ananiulizia kama nimeshaachana na x nkamwambie ndio ila bado namega kila nnapohitaji, ni dem wangu wakumpumzikia.

Moyoni niliumia sana kwa kuwa msaliti mbele ya mpenzi wangu ambaye ananipenda na me nnampenda kiukweli, kwa mara ya kwanza mwanaume nikamwaga machozi bila kutegemea, nikamwomba msamaha binti na mwisho akaubali, Sasa nina amani tele na sina mpango tena wa kuchit kwa namna yoyote ile kwni nimeshajifunza mwenzenu na tunamalizia mipango ya ndoa yetu,,,,Nawaasa tu wazee wangu nanyi muache tabia hiyo kwani za mwizi ni arobaini
 
ikuwa unachit lazima uwe mjanja wa kutegua mabomu yote, me napiga mpaka leo na sijashtukiwa wala nn
 
mkeo mtarajiwa ndo kwanza ana siku moja tu. hadi zifike 40 sio leo.

umeacha donda kuu kwenye moyo wa mkeo mtarajiwa.
nahisi humpendi kwa dhati. ungekuwa unampenda kwa dhati usingewaza kumfanyia ufedhuli huo
 
mkeo mtarajiwa ndo kwanza ana siku moja tu. hadi zifike 40 sio leo.

umeacha donda kuu kwenye moyo wa mkeo mtarajiwa.
nahisi humpendi kwa dhati. ungekuwa unampenda kwa dhati usingewaza kumfanyia ufedhuli huo

nilikuwa natamani kuacha ila nilishazoea, ila kwa sasa nimelazimika kwa kuwa nimegundua makosa yangu, na nimeamua kumpenda kwa dhati y wangu na tunajiandaa kuhalalisha mapenzi yetu
 
Back
Top Bottom