Tuwe na imani na tunaowapenda.

Karot

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2017
Posts
1,159
Reaction score
1,316
Habari za pirika wanajamii wenzangu.
Naenda moja kwa moja kwenye mada.
Kuna baadhi ya watu wana tabia ya kutowaamini wake/wachumba zao, hayo yote yanasababishwa na maisha wanayoishi huko mitaani.

Kiukweli kuna tabia ambazo haziwavutii wapendanao, ukiona mwenzio anachukia jambo unalolifanya ni vyema ukaliacha ili baadae lisije likaleta mtafaruku.

Kama mtu ambae umemuamini kumvulia nguo zako zote na kupata usingizi usiku kucha haumuamini utamuamini nani sasa?
Lengo langu ni hili hapa.
Niko na binam yangu tunakua tunachat kawaida tu hata mme wake anafaham sana.

Vile vile tuko na group letu la ukoo kwa ujumla tunakua tunapeana habari za hapa na pale kwenye familia zetu. lnafika wiki sasa Dada (Binam) yangu kabadilisha namba sasa sijui sababu nini na wala hajanambia. Lakini kwa bahati njema katika kuibadilisha kwake niliona kwenye group ila nilikua nasubiria aje pte lakini mpaka sasa hajaja na sijamuuliza tatizo.

Sasa jana nikajaribu kuwasiliana na mme wake habari zingine akanambia nionane nae uso kwa uso tiakajadili ( tupo eneo moja la kazi). Sasa nilipofika kabla hatujaongea kitu chochote akaanza kujibabaisha ila mimi nilimshitukia baada ya kuanza maswali.

Kabla ya yote; alianza kuniambia nimpe sim yangu anataka kuangalia "DP" yake jinsi inavyoonekana, sikumkatalia. Alizunguka baadae likaja swali, "Dada yako umemsevu jina gani?" Nikamtajia, akaangalia na kuniuliza tena, "Mara ya mwisho uliwasiliana nae lini?" Nikamjibu yapata wiki sasa, sijui alibadilisha namba? Nilimuuliza.

Cha kushangaza hata yeye akasema inawezekana alibadilisha namba kama vile hafaham. Inawezekana kweli mke wake abadilishe namba bila yeye kujua? Nikasema kuna kitu hapa. Baada ya kumaliza kuangalia alichokusudia na akanirudishia mwenyewe.
Baada ya hapo nikaangalia kafuta details zote ambazo nilikua nachat na mke wake, nikajiuliza mara mbili mbili huyu ana maana gani mbona simuelewi?

Sikumuuliza kitu chochote kuhusiana na hicho, nakaamua kuuchuna tu hata yeye hawezi kunambia kunambia kitu chochote kuhusiana na mke wake vinginevyo anikute juu, ila kwa kuchat nae tu familia kwa ujumla itamuona hana akili kugombana na mimi kisa nachat na mke wake.

Sasa ujinga uliopo, mke wake yupo Tz yeye tupo nje ya Tz sasa atamsimamia huko aliko? Na ubaya sasa atazidi kuwa na presha kwa kuwa mimi nakuja likizo huko yeye bado yupo huku huku si atazimia kabisa. Wakati sina mawazo hayo kwa mke wake hata kidogo.
 
Mwanaume unachat na dada yako binamu kila siku mnaongea nn?!


Kwani ukiacha kuchat nae utapungukiwa nn?
 
Mwanaume unachat na dada yako binamu kila siku mnaongea nn?!


Kwani ukiacha kuchat nae utapungukiwa nn?
Nachat na familia mzima nikiona kwenye group hawajibu, nawafata pembeni, na istoshe kwa huku niliko lazima akili yangu yote niweke kwenye mitandao husasan watu wa nyumbani. Najihisi niko nyumbani kukosa Kukosa kuweka mb japo siku moja najiona tofauti sana mkuu. Ingawa bei ya mb huku ipo juu lakini ntafanyaje mb 500 shilling 5000 ya Tz.
 
Ww ndio uko na makosa mkuu Dada binamu udugu mpk kwa jambo la muhimu tu lkn kuchat kutembeleana vinaleta wcwc
 
Mimi nina imani na Miss Natafuta![emoji28][emoji28][emoji28]
 
Sasa mkuu huna mwanamke wa kuchat nae kutwa uchat na binamu wako?. Huyo mume pengine hapewi tension za text kwenye cm yake kama wewe lazima awe na wivu. Pia kuna watu wengine wanakula mpaka binamu zao sasa huyu mume lazima achukuwe tahadhari. Halafu hapa unajisifu eti yupo likizo Tz na mimi nakwenda Tz, kwahio unataka kusema kama utakula papuchi yake binamu?. Mkuu wewe mbeba boksi wa UK? Manake huko kwa kuchapiana hamchelewi.
 
Rudia post vizuri ili uifaham.
 
Ww ndio uko na makosa mkuu Dada binamu udugu mpk kwa jambo la muhimu tu lkn kuchat kutembeleana vinaleta wcwc
Kwa familia za kwetu tunaona kawaida, maana ukiona tunavyotumiana sms utasema tunagegedana lakini hata mawazo hayapo kabisa. Hata wife alishawahi kununa usiku mzima baada ya kuona text "baby nimekumiss". Ugomvi uliisha baada ya kujuana na wazee kuingilia kati.
 
Kwanini azimie?
 
Nawewe si uache tabia ya kuchat na dada yako binam. Hivi mnaongea nini?
 
Si murudi huku nyumbani. 4 GB kwa buku sita tu
 
Tatizo lipo hapa mkuu may be muwe mnaweka na interpritation za familia yenu kwa kila 3rd party ili kuondoa sintofaham
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…