Tuwe Makini wasichana tutadanganywa mpaka lini?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuwe Makini wasichana tutadanganywa mpaka lini??

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by SaraM, Sep 9, 2011.

 1. SaraM

  SaraM Senior Member

  #1
  Sep 9, 2011
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru wana jf kwa makaribisho mazuri,
  hivi inakuwaje mwanaume anakuwa muongo anakudanganya for two years kwamba hajaoa, then unakuja unagundua kaoa ,ana mke na watoto
  Mie nimedanganywa na sasa niko kwenye maumivu makali ili niweze kuendelea na maisha,nilikutana nae chuoni yeye anasoma masomo ya juu zaidi yangu, akasema yuko single na mipango yote ya kuoana tukimaliza chuo alikuwa ananiambia.

  Yeye alitangulia kumaliza lakini alikuwa anasafiri anakuja kuniangalia chuoni, baasi nilipomaliza kwa vile tunakaa mikoa tofauti nikaamua kumzukia kwa suprise huko anapoishi, nilienda nilipofika mojakwa moja hadi ofisini, kastuka sana, tukatoka nikajua napelekwa kwake akaishia hotelini, jioni alipokuja ndio akanimwagia hilo shuzi, eti sorry,hivi kweli binadamu wamekuwa na roho mbaya kiasi hiki?nawaasa wasichana wenzangu wawe makini sana na hawa wenzetu kwani sio kila kitu wanachosem ni kweli....sasa nikaamua kukatisha mawasiliano kabisa kwa kipindi kirefu kiasi
  juzjuz kaja na mpya kaniomba anioe mke wa pili kwamba hawezi ishi bila mimi, marafiki zangu wanavutana wengine wanasema nikubali na wengine wanasema niendelee na msimamo wangu, je wewe mwana jf mwenzangu unasemaje?????
   
 2. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #2
  Sep 9, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Uwe mke wa pili? Huna wivu weye?
   
 3. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #3
  Sep 9, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Pole kwa mkasa uliokukumba...endelea na maisha na fungua moyo wako ipo siku utapata wa kwako peke yako.
  Vijana single tupo wa kumwaga,ushindwe kuchagua tu.
   
 4. RGforever

  RGforever JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2011
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 6,186
  Likes Received: 1,907
  Trophy Points: 280
  Wawe makini kivipi Dada angu? Huwezi kumjua mtu Eti pale tu atakapokuja kwa mara ya kwanza, ujue huyu huko hvi au vile. Kinachotakiwa hapa ni wewe kuwa na msimamo wako.sikushaur uje kuw mke wa pili ,achana nae mana bado hajakuletea effect kubwa kam vle Mimba,ambyo inawez kukufany ukakae naye.. Kwa Dunia ya leo wake wawil ni Ugomv ambao hutawez kuhimil kam una moyo mwepes. Ni hayo tu sisy angu na pole sana kwa yaliyokukuta.
   
 5. SaraM

  SaraM Senior Member

  #5
  Sep 9, 2011
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaani nina wivu wa hatari mwanajamii, nilipenda hasa
   
 6. Kbd

  Kbd JF-Expert Member

  #6
  Sep 9, 2011
  Joined: Oct 9, 2009
  Messages: 1,264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Hapana, mwache aendelee na maisha yake na wewe Mungu atakusaidia utampata wako peke yako.
   
 7. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #7
  Sep 9, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Pole dada. Ila la mke wa pili sikushauri. Maana hapa sisi tuko wawili yani husband na wife bado songombingo; sasa nambie muwe na uhusiano wa watu watatu; mume mmoja wake wawili; si kutafuta maradhi huko dada maana hapo ina maana umemuamini mume wako na mke mwenzio.
   
 8. SaraM

  SaraM Senior Member

  #8
  Sep 9, 2011
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ahsante sana kwa kweli huwezi jua ila ukiwa mchunguzi sana unaweza jua mapema, maana kunasimu zingine maybe ningekuwa mpekuzipekuzi ningegundua mapema
   
 9. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #9
  Sep 9, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  pole achana nae
   
 10. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #10
  Sep 9, 2011
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Pole dada kwa yaliokukuta muombe mungu akupe ujasiri utafanikiwa uatapata mwanaumwe wa kweli mwenye mapenzi ya kweli huyo uliekuwa naye hakuwa na mapenzi ya kweli kwako alitaka kukuchezea na kukupotezea tu....
   
 11. SaraM

  SaraM Senior Member

  #11
  Sep 9, 2011
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hili nalo neno, maana hizo zamu!
   
 12. u

  utantambua JF-Expert Member

  #12
  Sep 9, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Pain is love, love is not about hugs and kisses only.
   
 13. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #13
  Sep 9, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  Nadhani hadi kufikia hatua ya "kumzukia kwa surprise" tayari ulikuwa na wasiwasi fulani kuhusu huyo kijana?

  Ungefuata "dhamira" yako usingelizwa, lakini maisha ndivyo yalivyo, wanawake ni wa kudanganywa mara zote!
   
 14. SaraM

  SaraM Senior Member

  #14
  Sep 9, 2011
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baba enock niliamua kum surprise ile ya kimahaba, na nikijua yuko ofisini coz asubuhi na mapema alinipigia kwa landline kwa hiyo nisingewaza namfumania ofisini, pia ilikuwa ya kimahaba bila kuwaza lolote, swali kwako, kwa nini unafikiri alinidanganya? alidhani akisema ameoa ningemkataa au ni kitu gani alikuwa anawaza, kwa maoni yako tu
   
 15. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #15
  Sep 9, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  1.Tatizo wasichana tunajenga mazingira ya kudanganywa tangu awali. Mwanaume ukimdanganya jambo moja na akagundua umemdanganya ujue wewe utadanganywa matano.
  2. Wasichana wamekuwa wepesi sana kuwaamini hawa wanaume hivyo kuwahi kuanzisha mahusiano nao kabla hawajawaelewa.
  3. Wanashindwa kutofautisha wanapopendwa kikweli na wanapotumiwa.
  4. Wasichana wengi ni kama wanalazimisha penzi, yaani unaona kabisa mtu hakupendi ila kwa sababu moyo wako upo pale unaona hakuna mwingine.
  Yaani mimi mtu akinidanganya siku hiyo najua kama ananidanganya. Ndani ya wiki tu nitajua hadi marital status yake labda kama sihitaji kumjua.
   
 16. D

  Domo Zege JF-Expert Member

  #16
  Sep 9, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Niko single kama vipi tuanze upya, kutereza si kuanguka ni PM kwa maelezo zaid
   
 17. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #17
  Sep 9, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  <br />
  <br />
  Sangara bana lol! Kama vile nakuona
   
 18. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #18
  Sep 9, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  wasichana wengi hawapendi kusema ukweli wanapenda kuongopewa tu ..... maana anapenda vitu vya mpito kuliko halisia
   
 19. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #19
  Sep 9, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  <br />
  <br />
  Hili neno, karibu supu ya mawe
   
 20. bombu

  bombu JF-Expert Member

  #20
  Sep 9, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,134
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145

  wow! Sangara naona you are blowing your own trumpet. Mwambie mwayego
   
Loading...