Tuwe makini na wauza Dawa za Asili

Mr. MTUI

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
8,130
8,351
Wakuu wa JF..
Kumetokea wingu la watu wanaouza dawa za asili kwenye mitandao ya kijamii kama vile instagram, facebook n.k...

Sina uhakika na taaluma za wauza dawa hawa ila wengi wao wanatangaza dawa wanazonadi zinazobadilisha maumbile kwa wanawake na wanaume na matatizo common kama vile kupunguza uzito, kuongeza nguvu za kiume n.k...

Kutokana na kukosa udhibiti wa uuzaji wa dawa hizi na kuibuka kwa wajasiriamali hawa kuuza dawa nyingi kwa wakati mmoja..

Je hakuna uwezekano wa siku moja mtu kuchanganyiwa dawa ya kupunguza kitambi ukapewa ya kuongeza makalio au hipsi?

Je ninani anahusika katika udhibiti wa hawa watu?
 
Kuna mmasai mmoja alikuja na dawa moja ivi ya kuongeza appetite ya Kugegeda akaniambia hii inaitwa midfielder. Nikamuuliza hii IPO vizuri akasema ndio. Nikahifadhi lile jina na kufanya utafiti. Aisee!!! Kila muuza dawa Nikimuulizia Dawa ya kuongea hamu ya kupasha anataja jina like lile Midfielder, nikasema duh! Kumbe hii dawa ni Qualified.
 
Wakuu wa JF..
Kumetokea wingu la watu wanaouza dawa za asili kwenye mitandao ya kijamii kama vile instagram, facebook n.k...

Sina uhakika na taaluma za wauza dawa hawa ila wengi wao wanatangaza dawa wanazonadi zinazobadilisha maumbile kwa wanawake na wanaume na matatizo common kama vile kupunguza uzito, kuongeza nguvu za kiume n.k...

Kutokana na kukosa udhibiti wa uuzaji wa dawa hizi na kuibuka kwa wajasiriamali hawa kuuza dawa nyingi kwa wakati mmoja..

Je hakuna uwezekano wa siku moja mtu kuchanganyiwa dawa ya kupunguza kitambi ukapewa ya kuongeza makalio au hipsi?

Je ninani anahusika katika udhibiti wa hawa watu?

UMEPIGWA NINI?
 
Soko huria, ukiliwa utaugulia kimya kimya, na kuwazuia ni ngumu, maana mtandaoni, mkishapeana namba popote pale mnakutana na kupeana.

Una tatizo, nenda hospitali ama kwenye maombi ktk imani yako.

Ahsante!
 
UMEPIGWA NINI?
kuna jamaa yangu amepigwa..but licha ya hvyo uuzaji umekua wa holela sana...utashangaa dawa zinauzwa hadi stand dawa zinawekwa kwenye jua..kwa kweli ni shida
 
Huwa nashindwa kuwaelewa watu ambao hawajiamini na maumbile yao.

Kwanini usijikubali kwa vile ulivyo?

Hivi watu huwa hawajifunzi madhara wanayoyaona kutoka kwa wenzao!
 
Huwa nashindwa kuwaelewa watu ambao hawajiamini na maumbile yao.

Kwanini usijikubali kwa vile ulivyo?

Hivi watu huwa hawajifunzi madhara wanayoyaona kutoka kwa wenzao!
Watu wengine wana roho nzuri kwelikweli,yaani anawaza kumfurahisha mwingine kwa gharama ya maisha yake. Kila mtu awajibike kwa utamu wake mwenyewe tuache kujiongezea stress
 
Soko huria, ukiliwa utaugulia kimya kimya, na kuwazuia ni ngumu, maana mtandaoni, mkishapeana namba popote pale mnakutana na kupeana.

Una tatizo, nenda hospitali ama kwenye maombi ktk imani yako.

Ahsante!
Suluhisho la maradhi ni kwenda hospital tu, huyo anayekufanyia maombezi mwenyewe akiumwa anakimbilia hospital
 
Kuna mmoja alikuja kwa ofisi kaonyesha kichupa kina dawa ya maji duh kinatibu karibu magonjwa 17 nikaona ooooh ili changa inakuaje unatibu fangasi alafu hiyo hiyo malaria sugu na wenye vitambi inapunguza
 
Hili tatizo la waganga wa kienyeji ni kubwa sana na lina madhara makubwa kuliko unavyofikiria jana tumemzika mama mmoja hivi ambe aligundulika kuwa ana kansa ya kizazi lakini alidanganywa na mganga mmoja kutoka kigoma kuwa atampa dawa dawa na atapona ampe laki tano na shart la dawa zake ni kuwa asipige mionzi
 
Back
Top Bottom