Princemwalejr
JF-Expert Member
- Nov 9, 2017
- 496
- 492
Ujumbe wa krismas kwenu tuache kuuwa vizee kwa madai ya kuwa ni vichawi. Tuwape matunzo mema kama wenzetu wa Ulaya. Yaani mpaka raha. Wazee wana nyumba zao kama zionekanavyo pichani. Hapo hupati nyumba kama hujafikisha miaka 55. Wana sehemu za kuogelea, kufanyia mazoezi, kula, nyumba za kulala na kadhalika.
Ruhusa kuwatembelea na kuwapelekea zawadi lakini usipige kambi ukahamia hapo hapo. Wanapata huduma za afya. Na wengi wao bado wanaweza kuendesha magari. Nilidadisi habari zao nikaambiwa kuna wazee 2500 wanaoishi kwenye hizi nyumba. Wengi wao wako kwenye miaka ya 80. Mzee wao kabisa ana miaka 105. Ana akili timamu, anatembea na ana rafiki wa kike (girl friend).
Tukijipanga tunayaweza haya. Ndio maana wenzetu wanatuacha mbali kwa maisha mazuri. Wanabarikiwa kwa ubinamu wao wa kuhurumiana wao wenyewe mpaka huruma kwa wanyama.
Isitoshe ni shughuli inayotoa ajira kwa wengi hasa kwa wanafunzi wa shule na wanaotaka kufanya kibarua cha pili.
Vidingi vinapiga tizi hapo. Kuna vijeba vya miaka 90 lakini huviwezi kukimbia navyo kwenye treadmill.
Hapo wazee wanajiweka fiti kwa kuogelea.
Sherehe sherehe na vizibo haziwapiti.
Hapo ni sehemu ya maakuli.
Upepo mwanana yaani hadi raha.
Kwenye michezo pia wako vizuri.