Tuwashukuru Na Tuwaombee Hawa.

Tuwashukuru Na Tuwaombee Hawa.

ewards

Member
Joined
Aug 16, 2015
Posts
8
Reaction score
15
Leo nataka tuwashukuru wale hatukupata nafasi ya kuwashukuru kwa waliyofanya/support maisha yangu/yetu kwa namna moja ama nyingine.

Nikijitafakari hatua hiihapa nilipo, nimepita kwa mikono ya watu tofauti wengi sana. Wakati huo nilidhani ni jukumu lao pengine kuhakikisha nafanikiwa ktk hatua zote mbazo pengine kwangu peke angu ingekuwa changamoto, kumbe sivyo.!

Ninawashukuru wazee wangu kwa hatua zote, mlifanya kwa uainifu na kwa upendo mkubwa!
Lakini pia Sina hakika kama hawa nitakao saana, kuwashukuru ni wenzetu hapa JF lakini sina namna nyingine ya kufikisha shukurani hizi ispokuwa kupitia hapa na naamini ujumbe utafika.


Kitaaluma, Sito sahau juhudi zako kwangu Mwl J. Mwita kwa somo la Hisabati na kiingereza (Primary School), sikuwa mzuri ktk Hisabati lakini hukutaka kukubali nishindwe kwa namna yeyote ile, leo nimeona/najivunia kile sikuona nyuma ya juhudi zako enzi ile. Ni vile hatuja jaliwa nafasi nyingine kuonana ila naamini Mungu ni mwema tutaonana tena, nakuombea Uzima wenye Afya Mwl. Mwita, Mbabe wa Hesabu huyu!

Hawa wafuatao ninawashukuru kipekee, nikijua ni wachache wanaweza kuwa na Mioyo kama hawa.
Kwanza ni mkuu wa idara ya FST Mzumbe kipindi nikisoma, Madam Tupokigwe. Unaweza usikumbuke nini ulifanya kwangu lakini huwa nikifikiri binafsi nakuombea sana, Mungu akutunze na akubariki kusiko Elezeka. PM me, naamini wewe ni mwenzetu hapa JF.


Wa mwisho ni Mkuu wetu wa chuo Kipindi hicho Prof. F. Kamuzora. Kwanza nisamehe sana Chief, Pili nakushukuru sana. Ombi langu, Mungu akupe Afya njema na akuongoze ktk majumu yako.

Tuendelee Kuwaombea na kuwashukuru,

Jpil njema, Ahsante!
 
Nitarudi mwaka 2020 kwenye huu uzi
 
Namshukuru invisible kwa kunikubalia request ya kuwa jukwaa la wakubwa....nakupenda inv.
 
Back
Top Bottom