Tuwashtaki January na Tulia, Mkulima Kaonesha Njia

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,555
41,067
Hivi karibuni, mkulima amefungua kesi mahakamani dhidi ya baadhi ya Mawaziri kufuatia report ya CAG kuonesha kuwa kumekuwa na wizi/ubadhirifu/ufujaji mkubwa wa pesa ya umma kwenye wizara zao.

Sasa hapa kuna kashfa kubwa inayomhusisha Waziri wa nishati na spika wa Bunge.

Waziri wa nishati kagawa mitungi 100 ya gas kwa kila mbunge. Na spika wa Bunge kwa sababu alitambua kuwa kitendo hicho kilikuwa na harufu ya uchafu, aliamua kiwe siri.

Mambo muhimu ya kujiuliza:

1) Waziri January kugawa mitungi ya gas 100 kwa kila mbunge wakati bajeti inaenda kujadiliwa na wabunge aliowagawia mitungi ya gas, ilikusudia nini? Ni rushwa au msaada?

2) Hii mitungi 100 ambayo kila mbunge amepewa, alipewa huyo mbunge kama ya kwake, na hivyo aamue namna yoyote anavyotaka kuitumia au alipewa ili akawagawie watu wa jimboni mwake?

3) Kama mbunge alipewa hiyo mitungi ya gas ili akawagawie watu wa jimboni kwake, ni vigezo gani vitatumika mtu fulani apewe na mwingine akose?

4) Kwa hawa wabunge waiba kura, kuna utaratibu gani uliowekwa kuhakikisha kuwa hawaibi hiyo mitungi na kuifanya ya kwao, wakati inajulikana mwizi huwa hachagui cha kuiba? Mwizi wa kura, akipata nafasi ya kuiba pesa ataiba, akipata nafasi ya kuiba gari la Serikali ataiba, akipata nafasi ya kuiba mitungi ya gas, ataacha kuiba?

5) Waziri January, pesa ya kununulia mitungi 100 kwa kila mbunge kwa wabunge wote zaidi ya 300, imetoka kwenye fungu gani? Na ilipitishwa na chombo gani?

6) Je, kila wizara, kabla ya bajeti yake kupitishwa ikaamua kutumia pesa ya wizara kuwanunulia vitu vinachohusiana na Wizara yake, na kisha kuwahonga wabunge kama alivyofanya Waziri January, si utakuwa uhayawani wa pekee duniani?

7) Tunajua kuwa Spika mara nyingi amekaa kinafiki, na mara nyingi ametoa kauli za ajabu kuhusu Bunge, mara eti taasisi zote zinamtumikia mfalme, mara eti Bunge na mahakama vipo kwaajili ya kuisaidia na kuounga mkono Serikali, Serikali yenyewe ndiyo hawa mawaziri akina January, Mwigulu, n.k. Lakini kitendo cha yeye kulifanya tendo alilolifanya January kuwa ni siri, ina maana alijua kuwa ni uovu, na ni kinyume cha kanuni za Bunge, lakini yeye kwa vile ni mnufaika, aliamua kulifanya jambo zima liwe ni siri.

Tufuate mfano wa mkulima, hawa watu wawili tuwafungulie kesi kama washtakiwa wa msingi, na wabunge wote wajumuishwe kwa kukubali kupokea hongo.

Lakini jambo hili pia litazamwe kwa jicho la pili. Huenda imekuwa ni mbinu ambayo haikulenga kuwapa wabunge mitungi ya gas, bali imelenga kuchota pesa ya Serikali, mitungi imetumika kama daraja.

Yawezekana mwenye kampuni badala ya kumpa January pesa, akamwambia nitakupa mitungi, ukiweza kuiuzia Serikali, chukua pesa yote au utapewa nusu ya mauzo. Na ikiwa hivyo msishangae, huu utaratibu wa kupora pesa ya umma kupitia mitungi ukageuzwa kuwa ni utaratibu wa kila kikao cha Bunge. Wabunge wetu kwa vile wengi uelewa ni mdogo, wanaondoka wanashangilia kama mazuzu (neno la Mwalimu kwa mtu asiyejitambua) kwa kupewa mitungi ya gas, huku mwenzao kwa kupitia ujinga wao, anakomba mabilioni.

Tunajua mahakama zetu ni sehemu tu ya idara ya Serikali, lakini tukiwashtaki itabakia kwenye kumbukumbu ambayo siku moja kikija kizazi kilicho makini angalao kitaona juhudi zilizowahi kufanyika na baadhi ya watu lakini zikazimwa na mifumo mibaya ya utawala.
 
Tunajua mahakama zetu ni sehemu tu ya idara ya Serikali, lakini tukiwashtaki itabakia kwenye kumbukumbu ambayo siku moja kikija kizazi kilicho makini //angalao kitaona juhudi zilizowahi kufanyika na baadhi ya watu lakini zikazimwa na mifumo mibaya ya utawala.
Tunawaza uchaguzi,/uchafuzi ujao baathi😂😂😂😂
 
Tunawaza uchaguzi,/uchafuzi ujao baathi
Kwa hiyo yawezekana January ametoa hongo kwa wabunge ili wabunge nao wakatoe hongo kwa wapiga kura!!

Maana inashangaza sana, hata kama Serikali ingekuwa imeamua kutoa msaada wa mitungi kwa wananchi wasio na uwezo wa kununua, kwa nini haikupelekwa halmashauri? Kwa nini wapewe wabunge?
 
Gharama ya chaguzi/ Chafuziii 🤔
 
Hivi karibuni, mkulima amefungua kesi mahakamani dhidi ya baadhi ya Mawaziri kufuatia report ya CAG kuonesha kuwa kumekuwa na wizi/ubadhirifu/ufujaji mkubwa wa pesa ya umma kwenye wizara zao.

Sasa hapa kuna kashfa kubwa inayomhusisha Waziri wa nishati na spika wa Bunge.

Waziri wa nishati kagawa mitungi 100 ya gas kwa kila mbunge. Na spika wa Bunge kwa sababu alitambua kuwa kitendo hicho kilikuwa na harufu ya uchafu, aliamua kiwe siri.

Mambo muhimu ya kujiuliza:

1) Waziri January kugawa mitungi ya gas 100 kwa kila mbunge wakati bajeti inaenda kujadiliwa na wabunge aliowagawia mitungi ya gas, ilikusudia nini? Ni rushwa au msaada?

2) Hii mitungi 100 ambayo kila mbunge amepewa, alipewa huyo mbunge kama ya kwake, na hivyo aamue namna yoyote anavyotaka kuitumia au alipewa ili akawagawie watu wa jimboni mwake?

3) Kama mbunge alipewa hiyo mitungi ya gas ili akawagawie watu wa jimboni kwake, ni vigezo gani vitatumika mtu fulani apewe na mwingine akose?

4) Kwa hawa wabunge waiba kura, kuna utaratibu gani uliowekwa kuhakikisha kuwa hawaibi hiyo mitungi na kuifanya ya kwao, wakati inajulikana mwizi huwa hachagui cha kuiba? Mwizi wa kura, akipata nafasi ya kuiba pesa ataiba, akipata nafasi ya kuiba gari la Serikali ataiba, akipata nafasi ya kuiba mitungi ya gas, ataacha kuiba?

5) Waziri January, pesa ya kununulia mitungi 100 kwa kila mbunge kwa wabunge wote zaidi ya 300, imetoka kwenye fungu gani? Na ilipitishwa na chombo gani?

6) Je, kila wizara, kabla ya bajeti yake kupitishwa ikaamua kutumia pesa ya wizara kuwanunulia vitu vinachohusiana na Wizara yake, na kisha kuwahonga wabunge kama alivyofanya Waziri January, si utakuwa uhayawani wa pekee duniani?

7) Tunajua kuwa Spika mara nyingi amekaa kinafiki, na mara nyingi ametoa kauli za ajabu kuhusu Bunge, mara eti taasisi zote zinamtumikia mfalme, mara eti Bunge na mahakama vipo kwaajili ya kuisaidia na kuounga mkono Serikali, Serikali yenyewe ndiyo hawa mawaziri akina January, Mwigulu, n.k. Lakini kitendo cha yeye kulifanya tendo alilolifanya January kuwa ni siri, ina maana alijua kuwa ni uovu, na ni kinyume cha kanuni za Bunge, lakini yeye kwa vile ni mnufaika, aliamua kulifanya jambo zima liwe ni siri.

Tufuate mfano wa mkulima, hawa watu wawili tuwafungulie kesi kama washtakiwa wa msingi, na wabunge wote wajumuishwe kwa kukubali kupokea hongo.

Lakini jambo hili pia litazamwe kwa jicho la pili. Huenda imekuwa ni mbinu ambayo haikulenga kuwapa wabunge mitungi ya gas, bali imelenga kuchota pesa ya Serikali, mitungi imetumika kama daraja.

Yawezekana mwenye kampuni badala ya kumpa January pesa, akamwambia nitakupa mitungi, ukiweza kuiuzia Serikali, chukua pesa yote au utapewa nusu ya mauzo. Na ikiwa hivyo msishangae, huu utaratibu wa kupora pesa ya umma kupitia mitungi ukageuzwa kuwa ni utaratibu wa kila kikao cha Bunge. Wabunge wetu kwa vile wengi uelewa ni mdogo, wanaondoka wanashangilia kama mazuzu (neno la Mwalimu kwa mtu asiyejitambua) kwa kupewa mitungi ya gas, huku mwenzao kwa kupitia ujinga wao, anakomba mabilioni.

Tunajua mahakama zetu ni sehemu tu ya idara ya Serikali, lakini tukiwashtaki itabakia kwenye kumbukumbu ambayo siku moja kikija kizazi kilicho makini angalao kitaona juhudi zilizowahi kufanyika na baadhi ya watu lakini zikazimwa na mifumo mibaya ya utawala.

Uko sahihi kabisa, wanasheria wetu wanaweza kutusaidia kwenye hili.
 
Back
Top Bottom