Tuwasahau GSM kwenye tuhuma za dawa za kulevya

Mzee wa hat-trick

JF-Expert Member
Nov 21, 2016
1,730
2,388
Ni kweli kwamba wengi wetu humu jamvini tumetoa tuhuma zetu dhidi ya GSM, tukiwatuhumu kuhusika kwa njia moja au nyingine na uuzaji wa dawa za kulevya.

Kwa jinsi nilivyomuona Kamishna katika kikao cha Makonda cha leo, binafsi imenionesha dhahiri kwamba mamlaka yake yatapokwa na Makonda. Tone yake ni ya kipole pole sana. Hili ni tatizo especially kwa sababu Makonda ndio kma muanzilishi wa vita hii, hvyo ni rahisi sn kamishna kuelekezwa yupi wa kuwekwa na yupi sio wa kuwekwa.

Nadhani majina yatakayotafutwa na Kamishna ni lazima yatapitia tu kwa Makonda, na hata likiwemo la GSM:

1. Possibly Makonda atalitoa kwa sababu ni watu wake wa karibu na yeye atakuwa na sauti kwa Kamishna.

2. Hatutaweza tena kumlaumu Makonda kwa sababu SIO KAZI YAKE TENA, japo ni mchezaji wa kimya kimya.

3. Yawezekana pia kuteuliwa kwake ni kutufumba macho kwa sababu tunaamini yeye ni mgeni machoni pa wengi na hivyo hatujui mahusiano yake na "wazungu wa unga" yapoje.

Time will tell....!!!
 
Huyu Commissioner alifanya kazi na Nzowa hivyo lazima atakuwa anajua the ABC.Pili ni tumzima sana anaelewa namna ya kufanya kazi na watu waliolewa Madaraka na kiburi. Muda ndiyo dawa ila Makonda asifhanie wote ni akina Sirro.Inawezekana Sirro akawa ameamua kuwa alivyosababu ya Mazingira walivyo.

Ila huko atakutana na WM.
 
Mimi hata pharmacy sina, madawa..madawaa.kila kukicha..siju watu hawana la kufanya..wacha nikhazin tu.
0.jpg
 
Ukweli ni kwamba hawa WAYEMEN wanajua kucheza na kuuingilia mfumo wa serikali kwa namna wanavyotaka kwa kutumia "triangular psychology effect". Wanachokifanya wakiona ni vigumu kwa wao kuuingilia utawala fulani moja kwa moja njia wanayopitia ni kumtumia mtu wa pembeni mwenye ushawishi mkubwa kwa mtawala mfano hawa GSM wakati ule wakitambulika kama Home shopping centre walifanikiwa kuuingilia utawala wa JK kwa kumtumia Rizmoja na kufanya wanavyotaka kana kwamba wao ndiyo wamiliki wa Nchi hii, na ndivyo kwa njia ile ile wanayotumia kuuingia utawala wa JPM kwa kumtumia makonda. Nitoe mfano; wakati utawala huu unaingia madarakani wafanyabiashara wengi walibanwa walipe malimbikizo ya kodi ya mapato ambazo walizikwepa miaka ya nyuma ni nani humu jukwaani asiyejua HSC ndiyo walikuwa wakwepa kodi wakubwa ambao walijimilikisha mpaka bandari ya DSM na hakuna kiongozi yeyote wakati wa harakati za kuwabana waliokwepa kodi aliyenyanyua mguu wake kwenda kudai kodi pamoja na kutangaza kampuni yao imefilisika na kuanzisha nyingine GSM. Hivyo kwa muktadha huu ni vigumu hawa GSM kuchukuliwa hatua yoyote kwenye hili la dawa za kulevya sabb kuna mahusiano na bwana wa magogoni kupitia kwa makonda ingawa inafahamika wazi ndiyo mapapa wakubwa wa dawa za kulevya
 
Hawa GSM ndo naskia wanawajengea Bakwata HQ yao pale Biafra? Na si ndo jana nilimwona Sheikh Mkuu akitangulia kutoa neno? Kuna uhusiano hapa? Au ni coincidence tu?
 
Back
Top Bottom