Tuwaombee msamaha Kafulila na wajumbe wengine wajiunge CHADEMA

Tuwaombee msamaha Kafulila na wajumbe wengine wajiunge CHADEMA

Wala haina haja atakuja kutushibuda tu... acha apumzike na kama inawezekana amchukue na huyu mwenzake tusiye na imani nae wakaanzishe chama kingine
 
Yaleyale ya Shibuda yatajirudia kwa Kafulila. Siungi hoja. Anapaswa kujutia ujinga alioufanya,
wewe toka lini ukasapoti mambo ya Chadema? unaona Kafulila ni threat kwa CCM akijiunga Chadema. Mimi nasapoti hilo wazo. Ni vema arejee Chadema.
 
Namsikitikia kafulila, amepoteza ubunge mapema mno na yote ni sababu ya kukosa hekima, swala la kupewa msamaha na Chadema, kafulila hakufukuzwa Chadema, mwenyewe aliondoka tena kwa mbwe mbwe nyingi tu! akakimbilia NCCR - Mageuzi, kafika kule akaendeleza mbwe mbwe, akafikia hatua ya kubishana na uongozi alioukuta, akataka ligi akijua watanifanya nini mimi nimekipa chama heshima mimi ni mbunge,

Ni mambo ya kitoto, na yatazidi kumgharimu katika harakati zake za siasa, arudi Chadema ila Chadema wapo smart zaidi ya hao NCCR - Mageuzi, huko wakimsimamisha akashinda ubunge, akileta dharau watamvua uanachama na ubunge ataukosa sasa kama hatafikiria hilo aende TADEA, NRA, UPDP, CHAUSTA nk hivi vyama havina uwakilishi Bungeni kama wanampenda jimboni kwake aende huko akishinda tu! ataheshimiwa sana na viongozi wa vyama hivi hatafukuzwa ila CHADEMA hakumfai.
Suala si Kupoteza Ubunge Je , Tuhuma alizotoa ni kweliau ni uOngo???
 
Nakumbuka baada ya Kafulila kutoka CDM, Mh.Zitto alimpa magari ya kusaidia kampeni zake Kigoma. It seems wana uhusiano wa karibu na Kabwe. I hope even this time atambeba tena.
 
Tusizunguke mbuyu story ambayo wengi hawataki kuisikia ni kwamba Kafulila kaponzwa na Zitto period, na kama dili lingefanikiwa wangefanikiwa wote, anyway leaving the past behind & worrying about the future.

Kafulila hakufukuzwa CDM aliondoka mwenyewe kwa jaziba zake na ndoto zake kwa hiyo yuko huru kabisa kurudi, navyoijua CDM nafikiri hata leo akiamua kurudi atapokelewa tu, yeye asione aibu wamefanya hivyo wengi kina Wassira, Tambwe Hizza tena Tambwe alisema akirudi CCM alale na mama yake sembuse Kafulila. Kafulila ni mpiganaji mzuri anaweza kuwa hazina nzuri ya chama, binafsi ningependa arudi ila ajiulize mara mbilimbili WHY ALWAYS ME. Kwa upande wa CDM wakiamua kumpokea wajue wanawakutanisha tena marafiki wawili ndani ya chama kimoja wawe tayari ku handle the outcomes ni hivyo tu. Otherwise all the best welcome home again our hero 'mission unaccomplished' tujipange upya.
 
Wanajamvi JF
Tumuombee msaha kafulila ili arudi CHADEMA kuendeleza harakati za kuijenga TZ kwa sababu

  • Alikuwa mwanachama wa CDM
  • Aliungana na wabunge wa CDM bungeni kususia hoja ya katiba
  • Anaonyesha kweli yeye ni mpinzani wa CCM si kibaraka
  • CDM ni chama tawala cha upinzani nchini Tz kama CCM wanavyofanya wapokea walio hama na kurejea upya
  • etc
Wajumbe wengine pia wahamie CDM kwani wamekuwa ni wachapa wazuri ndani ya chama chao wakijiunga na CDM wataku mtaji wa faida kubwa

Nawasilisha

Mkuu DC unataka virus ije CDM wakati bado kuna mi virus kama Zitto, Shibuda na Selasini hatujai-frash vizuri ikafa.....o
Ok kama kweli Kafulila ni mpinzani kwanini aliungana na Rashid kubadili kipengele cha kutambua kambi rasmi bungeni? tena yeye ndio alieandika barua na mnafiki mwenzie Rashi hamad... Sorry kamuombee msamaha TLP
 
Yeye mwenywe KAFULILA aje aombe msamaha na siyo sisi tumuombee kwa niaba yake maana baadae anaweza akatugeuka akasema sisi ndio tulimfuata na kumuombea msamaha! unajuaje kuwa aliyeanzisha uzi sio kafulila.
 
waunda chama ch.ao na mwenzie zitto kama walivo kuwa wamepanga
 
tena we ni mwongo ,umetanguliza chuki binafsi,alomwita sisimizi ni Dr Slaa sio MBOWE
 
Ikumbukwe kuwa Kafulila hakufukuzwa cdm ila alijiondoa yeye mwenyewe.. Na kwa tabia zake amevuna alichopanda jamani.
 
kwake sehemu salama ni DP hana tofauti sana na mch. Mtikila.
 
Back
Top Bottom