Namsikitikia kafulila, amepoteza ubunge mapema mno na yote ni sababu ya kukosa hekima, swala la kupewa msamaha na Chadema, kafulila hakufukuzwa Chadema, mwenyewe aliondoka tena kwa mbwe mbwe nyingi tu! akakimbilia NCCR - Mageuzi, kafika kule akaendeleza mbwe mbwe, akafikia hatua ya kubishana na uongozi alioukuta, akataka ligi akijua watanifanya nini mimi nimekipa chama heshima mimi ni mbunge,
Ni mambo ya kitoto, na yatazidi kumgharimu katika harakati zake za siasa, arudi Chadema ila Chadema wapo smart zaidi ya hao NCCR - Mageuzi, huko wakimsimamisha akashinda ubunge, akileta dharau watamvua uanachama na ubunge ataukosa sasa kama hatafikiria hilo aende TADEA, NRA, UPDP, CHAUSTA nk hivi vyama havina uwakilishi Bungeni kama wanampenda jimboni kwake aende huko akishinda tu! ataheshimiwa sana na viongozi wa vyama hivi hatafukuzwa ila CHADEMA hakumfai.