Tuwakumbushe wanaoenda kugombea uongozi serikali za mitaa

Tuwakumbushe wanaoenda kugombea uongozi serikali za mitaa

sili SG

Member
Joined
Oct 12, 2018
Posts
22
Reaction score
26
Kwanza nawapongeza wote waliojitathimini na kuona wanaweza kutuwakilisha wengine vilevile wanakubalika katika maeneo yao katika hizi ngazi za chini.

Ila huyu kiongozi atambue na akumbuke kwamba:
  • Hii kazi ni ya wito na ya kujitolea kwa asilimia kubwa unawawakilsha wananchi na kuwatetea wenyonge wenye haki vilevile kutatua matatizo madogo madogo yaliyo katika ngazi husika.
  • Huu uongozi, uwakilishi, kazi haina mshahara zaidi ya posho ndogo ndogo ambayo hawawezi kuishi kwa kutegemea hiyo. Kwahiyo kiongozi anayekwenda kugombea awe na shughuli/kazi/ biashara halali inayomuingizia kipato.
  • Huyu kiongozi atambue akipita kutoa huduma zinazomuhusu ni wajibu wake na bure bila malipo (muhuri haulipiwi).
  • Uongozi huu sio daraja la kuwa dalali wa viwanja, mashamba, machimbo na maeneo ya wazi.
  • Uongozi huu ni wa kujituma kusaidia watu wa eneo la mitaa, vijiji, vitongoji katika mashala mbalimbali katika ngazi hizo.
Ikumbukwe huu ni uongozi wa ngazi ya chini katika mnyororo wa utawala kwa hiyo wajibu wake mkuu ni kuwakilisha wananchi katika ngazi hizo.

Wao wasiwe chanzo cha migogoro, uvunjifu wa amani na kero katika mitaa. Kwa kulazimisha kulipwa ili watimize majukumu waliyoyaomba wenyewe wakiwa wanajua terms and conditions za nafasi hizi.
 
Back
Top Bottom