Tuwakatae vibaraka wa CCM ndani ya CHADEMA

Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,143
3,196
Kila kunapokucha tunasikia makelele mengi sana kuhusu matumizi ya hela ya CHADEMA na mapungufu mengine mengi ya viongozi wa chama. Tulianza kuyasikia haya tangu wakati wa akina Mtela, na sasa akina Mwigamba. Lakini hatujawahi kusikia hata mtu mmoja anahoji matumizi ya hela na mapungufu ya kiuongozi yaliyopo kwenye vyama vingine. Wakati huo huo watanzania wote ni mashahidi kwamba ni CHADEMA pekee hapa nchini ndiyo inayofanya vema katika shughuli za kisiasa na kuwapa wakati mgumu sana CCM. Wote tunajua kwamba ni CHADEMA inayojishughulisha na harakati/program mbalimbali zinazogharimu mamilioni ya fedha katika harakati za kujijenga.

Ni kwanini hivi vyama vingine haviulizwi kama vinapeleka wapi ruzuku ilihali hatuoni harakati zozote za kujenga chama kama zinazofanywa na CHADEMA? Ni kwanini viongozi wa vyama vingine hawaulizwi hata pale vyama vyao vinapopoteza umaarufu na kuteketea. Hivi ni nani aliyewahi kuhoji uhalali wa Mtikila, Mrema au Cheyo kuendelea kuwa viongozi wa vyama vyao, pamoja na vyama vyao kuteketea kabisa kisiasa? Ni nani aliyehoji uhalali wa Lipumba na Seif kuendelea kuwa viongozi wa CUF huku wote tukishuhudia CUF inavyopoteza umaarufu na kupotea kwenye ramani ya siasa nchini? Ni kwanini kila kuchapo ni wafuasi wa CHADEMA tu wanaibuka na kujifanya wasamalia wema wenye nia ya kukiokoa chama kwa kueleza mapungufu lukuki ya uongozi wa CHADEMA, huku wote tukishuhudia kazi nzuri inayofanywa na CHADEMA Katika siasa za Tanzania?

Kwahakika mimi kama mwanaCHADEMA mwenye akili timamu, na ninayefikiri kwa kina, siwezi kutilia shaka matumizi yoyote ya fedha ndani ya chama hiki kwa kuwa outputs za kazi ya hiyo fedha zinaonekana. Hata kama kuna makombo ambayo yanaokotwa na kuliwa si kitu, kwa kuwa naamini kiasi kikubwa kinatumiwa kwa kazi za siasa. Hata mimi ningepewa nafasi kama za viongozi wa CHADEMA hivi sasa, naamini kuna mahali ningejipendelea. Mimi ni binadamu lazima ningefanya hivyo, kwanini wakifanya wengine liwe ni jambo kuubwa la kupita kupiga kelele mitaani ilihali hata mimi katika mapungufu yangu naweza kufanya hayohayo?

Hebu tufikirie hili: CCM wanapokea ruzuku kubwa zaidi kushinda ya CHADEMA kwa karibu mara tatu kama si nne, lakini hatuoni chochote wanachokifanya? Je kuna yeyote amewahi kujifanya ni mwanaCCM mkereketwa wa kutetea matumizi ya fedha ndani ya CCM na kuhoji mahali zinakopelekwa fedha zote za ruzuku na za misaada kutoka vyama rafiki wa CCM? CUF kikiwa kama chama kikuu cha upinzani Zanzibar, na chama chenye wabunge wengi next to CHADEMA, kinapokea kiasi kikubwa cha ruzuku, lakini hakijishughulishi na harakati za kukijenga chama kama ambavyo CHADEMA inafanya kwa ruzuku zake kidogo, mbona huko hatuoni yeyote anajitokeza na kujifanya msamalia mwema mwenye nia ya kukiokoa CUF na matumizi mabaya ya fedha?

Nitamshangaa sana mwanaCHADEMA yeyote atakayeinuka na kusema eti ameshawishika vya kutosha na propaganda za akina Mwigamba na vibaraka wengine wa CCM na kuanza kukichukia au kuwachukia viongozi wakuu wa chama. Kwa akili ya kawaida kabisa, unaweza kutambua kuwa hapa pana kitu kinaendelea; kuna watu ndani ya CHADEMA wananunuliwa na CCM na kukubali kutumika katika harakati za kukichafua na kukivuruga chama ili kipoteze uwezo wa kutoa ushindani wa kutosha kwa CCM. Ni dhahiri kwamba vita yetu inazidi kuwa pana na ngumu. Ni wakati wa kila mwanachadema sasa kusimama na kuwapinga hawa vibaraka wa CCM waliopo ndani ya CHADEMA.
 
Mkuu umeongea vema sana, na itoshe kusema wahujumu chama wote tutawadhibiti bila kujali nafasi zao katika chama ama sura zao,

Kila mwanachadema awe mlinzi wa chama kuanzia sasa popote alipo
 
kudadadeki, antivirus inayotumiwana CHADEMA naikubali sana, ina scan virusi nouma, hadi sasa 20% scanning........ virusi kibao vimeshakamatwa, kufikia 2015 vitakamatwa vingi. kirusi cha uchaguzi wa ndani ya chadema tayari deleted, hahahahaha, CC MANI Elli mwitamaranya
 
Last edited by a moderator:
Umeongea point ila hapo ulipotoa argument kuwa kwa sababu vyama vingine hawahoji matumizi ya ruzuku basi nasisi tusihoji ndo umeharibu maana nzima ya point yako
 
Kusema kweli mpaka sasa hakuna hata MwanaCHADEMA mmoja aliyejibu hizi tuhuma,Nasema tena hakuna aliyejibu zaidi ya blah blah tu!CHADEMA tumezoea kuwashambulia CCM haya sasa yametuka hatujui tufanye nini.
 
Nina imani kubwa kwamba kama wanachadema tutakataa kununuliwa, basi hata kama zitakuja propaganda za namna gani hazitatufanya tuyumbe na kurudi nyuma katika harakati zetu za kumkomboa mtanzania kutoka katika mikono ya nyang'anyi CCM.
 
CDM tusikubali kushindwa kusonga mbele.ng'ombe tumekwisha mchinja sasa tushindwe kumalizia kuchna mkia?wasaliti wote ndani ya CDM na Wapigwe tu!
 
Kusema kweli mpaka sasa hakuna hata MwanaCHADEMA mmoja aliyejibu hizi tuhuma,Nasema tena hakuna aliyejibu zaidi ya blah blah tu!CHADEMA tumezoea kuwashambulia CCM haya sasa yametuka hatujui tufanye nini.
Hatuoni hoja ya kujibu. Zila hoja za akina Mwampamba wakati ule zilionekana za maana sana na zenye mshiko mkubwa kwa walio wengi, lakini hadi leo wameshindwa kuwasilisha ushahidi wowote wa wazi kama walivyoahidi, na mwisho wa siku wameishia kupiga kelele zisizo na msingi. Ndiyo maana tunaamini kwamba shutuma zilizo nyingi ni za kupika. Kama ni hoja ya katiba kwa mfano, Mnyika keshaitolea ufafanuzi. Kwahiyo sioni hoja nyingine inayohitaji majibu.
 
Mchawi wa chadema ni viongozi wa chadema hasa mbowe na slaa waliochakachua katiba halafu wanakimbilia kumpiga mwigamba.
 
Umeongea point ila hapo ulipotoa argument kuwa kwa sababu vyama vingine hawahoji matumizi ya ruzuku basi nasisi tusihoji ndo umeharibu maana nzima ya point yako
Ni kweli Deo, lakini nia yangu haikuwa kulinganisha transparency ya vyama vingine na kuilinganisha na ya kwetu. Nia yangu ni kutaka kuonyesha kwamba kuna hujuma. Wale wanaoibuka kwetu na kujifanya wapiganaji ni dhahiri kwamba wanatumwa.
 
Hatuoni hoja ya kujibu. Zila hoja za akina Mwampamba wakati ule zilionekana za maana sana na zenye mshiko mkubwa kwa walio wengi, lakini hadi leo wameshindwa kuwasilisha ushahidi wowote wa wazi kama walivyoahidi, na mwisho wa siku wameishia kupiga kelele zisizo na msingi. Ndiyo maana tunaamini kwamba shutuma zilizo nyingi ni za kupika. Kama ni hoja ya katiba kwa mfano, Mnyika keshaitolea ufafanuzi. Kwahiyo sioni hoja nyingine inayohitaji majibu.
Jibu hoja hizi,
kwa nini viongozi wenu walichakachua katiba?

kwa nini mnyika na slaa walitudanganya kuhusu katiba ya 2004 na 2006?

kwa nini mwigamba alipigwa na viongonzi wa chadema wakati kasema kweli?
 
Mkuu umeongea vema sana, na itoshe kusema wahujumu chama wote tutawadhibiti bila kujali nafasi zao katika chama ama sura zao,

Kila mwanachadema awe mlinzi wa chama kuanzia sasa popote alipo

Mahali Chadema mnapochemka ni.hapa. Mnadhani kila anayewakosoa ana nia mbaya. Wengi wanawakosoa kwa nia nzuri, wanataka mjirekebishe ili muwe mbadala wa vyama vyao sasa au hapo mbeleni. Hata nawajua wanachama wa ccm Wengi tu ambao kwa namna moja au nyingine wanawatazama kama chama mbadala ya Ccm. Lakini kwenu imekuwa tofauti, mnatazama wale walio wenu tu.hamtazami Watanzania kwa ujumla wao. Kwahiyo hao mnaosema wasiwaingilie mambo yenu kwa sababu ni wanaccm ndio wapiga kura wenu. Kwani mkipigiwa kura na wanachadema tu mtashinda uchaguzi? Jengeni Chadema ya Watanzania sio Chadema ya watu flani flani.
 
Mkuu Lukolo kwa kuwa hawa vibaraka hasa wale walio katika uongozi au ubunge wanajulikana basi anzeni kabisa kuwatenga hadi waone kuwa CDM si sehemu yao, ila pia ili mambo yawe safi, mambo yote ni 2015 tu. Watasambaratika kama maghorofa yanayodondoka DSM kwa udhaifu wa uongozi thabiti. Kazi ni kutumia nguvu kubwa kuandama CDM tu.
 
Nina imani kubwa kwamba kama wanachadema tutakataa kununuliwa, basi hata kama zitakuja propaganda za namna gani hazitatufanya tuyumbe na kurudi nyuma katika harakati zetu za kumkomboa mtanzania kutoka katika mikono ya nyang'anyi CCM.
mkuu acha wanaoweza kununuliwa sasa wanunuliwe ili tuwajue na tuwaondoe tuendelee kupanga safu nyingine na nyingine hadi mwisho wa siku tuwe na timu bora itakayoweza ku'sign mikataba ya nchi kwa manufaa ya watanzania wote pasipokununuliwa na wachina na wazungu,
 
hatuwezi kuingia uchaguzi mkuu 2015 na watu wenye tamaa na sanduku za hela kwa vile tu hawakuonyeshwa hizo hela mapema, ngoja kila mmoja aonyeshwe masanduku ya hela sasa na apime mwenyewe nafasi aliyonayo achague moja, kutumikia wananchi au kutumika na mabwana zake kwa vipande vya shekel.
 
Ni kweli Deo, lakini nia yangu haikuwa kulinganisha transparency ya vyama vingine na kuilinganisha na ya kwetu. Nia yangu ni kutaka kuonyesha kwamba kuna hujuma. Wale wanaoibuka kwetu na kujifanya wapiganaji ni dhahiri kwamba wanatumwa.
Mkuu mimi sioni kama kweli hawa watu wanatumwa ila kinachoonekana wanachadema wengi wanalazimishwa kutenda dhambi ndani ya chadema kwa kunyimwa uhuru wa kuhoji yanayotokea ndani ya chadema ndiyo maana haya yanatokea.
 
CHADEMA ukitaka wakupige waambie wakaguliwe mahesabu au uwaambie Wafanye uchaguzi wa viongozi wao, lazima watakupiga tu maana hawana namna nyingine!
 
Hatuoni hoja ya kujibu. Zila hoja za akina Mwampamba wakati ule zilionekana za maana sana na zenye mshiko mkubwa kwa walio wengi, lakini hadi leo wameshindwa kuwasilisha ushahidi wowote wa wazi kama walivyoahidi, na mwisho wa siku wameishia kupiga kelele zisizo na msingi. Ndiyo maana tunaamini kwamba shutuma zilizo nyingi ni za kupika. Kama ni hoja ya katiba kwa mfano, Mnyika keshaitolea ufafanuzi. Kwahiyo sioni hoja nyingine inayohitaji majibu.

Suala la Katiba ya 2004 na ile ya 2006 ni suala la kupuuza?CHADEMA itaanza kuangamia kama hatutakuwa tumejipanga kujibu hizi tuhuma na hakuna njia nyingine ya kuwanyima CCM fursa ya kuishambulia CHADEMA zaidi ya kuondokana na uongozi ulioko madarakani,That's the only way!!!
 
Back
Top Bottom