Tuwakatae Maaskofu wa aina ya Gwajima

Tuwakatae Maaskofu wa aina ya Gwajima

Namkubali Gwajima ni mtumishi wa Mungu na anachukia unafiki
 
Hatuna shida ya viongozi wa dini, shida yetu ni viongozi watakaotupeleka mbinguni kwa haki. Tunataka viongozi wasioleta uchochezi wa kidini, wanaweza kuleta mpasuko mkubwa sana
 
Jamani nawaomba sana tusichanganye mambo! Ya Mungu tumuachie Mungu na ya Kaisari tumuachie Kaisari. Siasa na Dini haviingiliani, na ndiyo maana hakuna usajili wa dini Serikalini. Kama wewe ni kiongozi wa dini endelea na dini usiingie kwenye siasa, mnatuchanganya jamani!!!! Na kama unashughulika na siasa basi baki na siasa, usichanganye na dini!!!! Mbona hamueleweki!!!!!

Gwajima kasema siyo kiongozi wa Dini Bali ni kiongozi wa kiroho! Mwanadamu ana roho, nafsi na mwili. Huwezi ukavitenganisha na mtu akabaki kuwa hai!
Hali kadhalika mtu anahitaji HUDUMA ya kiroho katika mambo yote anayofanya ikiwa ni pamoja na siasa.
 
Yaani Gwajima namkubali mpaka basi tena sijuhi nisemeje yaani mpenda ile mbaya yupo ndani ya moyo wangu masaa yote
 
Sikubaliani na baadhi maaskofu wa aina ya Gwajima kwa kuwa baadhi yao wameshiriki kuvunja ndoa nyingi na kuzifilisi baadhi ya familia huku wao wakijitajirisha kwa kutumia migongo ya ujinga wa baadhi ya waumini wao.

Sikubaliani nao kwa kiasi kikubwa watu waliojipachika uaskofu na unabii wakati nafsi zao zimejaa mambo machafu.

Pia nawachukuia watu waojipachika majina ya uaskofu kwa lengo la kuwaghilibu Watanzania wenzao, ambao wamekumbwa na misongo ya maisha, shida za kila aina ambao hujikuta wakiangukia mikononi mwa hawa matapeli wanaojifanya wana uwezo wa kuwaondolea shida zao.

Wanajiita Maaskofu, manabii, mitume, mitume wa fedha, n.k. ni kejeli na fedheha kwa Mungu! Wanajifanya watumishi wa Mungu lakini kumbe wamejaa roho ya kutumikiwa. Wanasema wao ndio wafuasi wa Kristo lakini hawafuati mafundisho na maisha ya Kristo.

Wanasema wanachunga kondoo wa Bwana wakati wao ndio mbwa mwitu wakali wanaotafuna kondoo za Bwana na kuwalazimisha watu kutoa kila kitu walichonacho hadi wanafilisika lakini kumbe wao wanaishi kwa ufahari mkubwa! Wanalaumu serikali kwa ufisadi kumbe wao ndio mafisadi wa mali za kanisa na waumini wao. Hawana huruma hata kidogo, nia yao ni kula na kushibisha matumbo yao kwa vijisenti vya maskini!

Umewahi kuwasikia hata siku moja wakiweka mikakati makanisani mwao ya jinsi ya kuwasaidia maelfu ya maskini na yatima tuliono? Kati ya vitu wasivyopenda kusikia watu hawa ni huduma kwa watoto yatima, wajane na walemavu.

Kwa tabia hiyo ya maaskofu hao hujipatia fedha nyingi kwa njia ya sadaka, mavumo makubwa kutoka waumini wao ambayo huwapa kiburi na kujiona miungu watu na kutoona haya kuwasema maaskofu wa ukweli, walioupata uaskofu wao darasani na kwa uwezo wa Mungu muumba mbingu na ardhi.

Sikubaliani na maakofu hawa matapeli kwa sababu baadhi yao tunafahamu vizuri historia zao na maisha yao kwa ujumla, historia ya maisha machafu na tabia za kishetani ndio maana wanakimbilia katika ulokole ili kusafisha historia zao ndani ya jamii, huku baadhi yao wakifanikiwa kuanzisha hata makanisa lakini ukiangali kwa ukweli hayana hata hadhi ya kuitwa makanisa.

Naamini makanisa kama haya ya kina Gwajima na maaskofu wengine kama kina Gwajima ndio yale ya manabii wa uongo walioelezwa na Yesu Kristo, mbele ya wanafunzi wake kwamba watatokea mwisho wa dunia na wengi watajifanya wana uwezo wa kuponya.

Makanisa haya yanayoibuka kama uyoga hayana tofauti na yale yaliyotokea Uganda ambako Kibwetere aliwafungia ndani waumini wake na kuwateketeza kwa moto.

Rai yangu kwa Serikali: Upo umuhimu mkubwa sasa, pamoja na uhuru wa kuabudu kwa mujibu wa katiba yetu lakini mamlaka ya usajili wa makanisa na misikiti iwe makini kwa watu wanaojianzishia madhebu kila kukicha kwani mengine yamekuwa yakiwatia umasikini Watanzania na kuleta uchochezi hapa nchini.

Kwa sasa CCM wameamua kujidanganya wenyewe pasipo kujua hathari yake itakayowapata tarehe 25/10)15.

Wameamua kutembea na wasanii wote wa Bongo Flava,Movie, Dance na The comedy ambao wamewanunua kwa kipindi hiki cha kampeni na baada ya uchaguzi hawatakuwa na habari nao.

Ivyo unakuta watoto wengi na wanafunzi kujaa uwanjani ili kuweza kuwaona wasanii, kwasababu hakuna kipindi ambacho wataweza kuwaona bure. Unakuta hata baadhi ya wananchi wa vyama vingine wapenda burudani wanaenda kwa ajili ya kuwaona wasanii. Lakini wanajua siku ya tarehe 25/10/15 kura wapige wapi.

CCM itapatwa na mshangao mkubwa matokeo yatakapotoka. Hawataamini kwani kura zao Zitakuwa chache. Matokeo yake hawatakubaliana na matokeo. Na watasababisha vurugu ya kuomba kura zirudiwe wakisema wameibiwa kura. Watasema mbona mikutano yetu watu walikuwa wanajaa sana. Hawatakumbuka kuwa wananchi wengi na hasa watoto walikuwa wanafuata The comedy, bongo flava,Movie na taarabu

Fuatilia mikutano ya Chadema/ukawa hakuna wasanii. Wananchi wengi wanajitokeza wenyewe bila vivutio vya wasanii. Yani wanaenda wenyewe kwa mapenzi yao, na kusikiliza sera. Maneno machache lakini yenye maana kubwa katika maisha yao. Hakuna matusi wala mipasho, wanaelezwa ukweli.

Mungu Ibariki Chadema/Ukawa
Mungu Ibariki Tanzania
 
Mbona alipoongea Dr slaa hawakusema aache siasa? Maana Dr slaa aliacha chama lakini alisema ataendelea kuuelewesha umma, je huko ni kuacha siasa au kuacha uanachama, mbona Dr slaa alimsema gwajima ni mshenga amekula rushwa bila ushahidi, sasa kwa nini gwajima asitoe ukweli wakati ukweli wao ni kwa ajili ya manufaa ya umma? si kwa ajili yao.
Watu wanaposema viongozi wa dini wasijihusishe na siasa,kwani viongozi si wapiga kura,he si wananchi, je hawana ndugu, jamaa na marafiki ? Kwa hiyo gwajima kusema ukweli wa slaa ni muhimu kwa umma wa wapenzi wa chadema, ili wajue kwa nini kiongozi wao abadilishe usemi namna hiyo. ukweli wa kutupiwa vitu nje na kulala kwenye gari unaonyesha wazi kibano kilichompata slaa, na kwa hakika kwa background yake ya upadre, sidhani kama alishawahi kukutana na wanawake ngangari namna hiyo, kabari ngumu sana
 
Sikubaliani na baadhi maaskofu wa aina ya Gwajima kwa kuwa baadhi yao wameshiriki kuvunja ndoa nyingi na kuzifilisi baadhi ya familia huku wao wakijitajirisha kwa kutumia migongo ya ujinga wa baadhi ya waumini wao.

Sikubaliani nao kwa kiasi kikubwa watu waliojipachika uaskofu na unabii wakati nafsi zao zimejaa mambo machafu.

Pia nawachukuia watu waojipachika majina ya uaskofu kwa lengo la kuwaghilibu Watanzania wenzao, ambao wamekumbwa na misongo ya maisha, shida za kila aina ambao hujikuta wakiangukia mikononi mwa hawa matapeli wanaojifanya wana uwezo wa kuwaondolea shida zao.

Wanajiita Maaskofu, manabii, mitume, mitume wa fedha, n.k. ni kejeli na fedheha kwa Mungu! Wanajifanya watumishi wa Mungu lakini kumbe wamejaa roho ya kutumikiwa. Wanasema wao ndio wafuasi wa Kristo lakini hawafuati mafundisho na maisha ya Kristo.

Wanasema wanachunga kondoo wa Bwana wakati wao ndio mbwa mwitu wakali wanaotafuna kondoo za Bwana na kuwalazimisha watu kutoa kila kitu walichonacho hadi wanafilisika lakini kumbe wao wanaishi kwa ufahari mkubwa! Wanalaumu serikali kwa ufisadi kumbe wao ndio mafisadi wa mali za kanisa na waumini wao. Hawana huruma hata kidogo, nia yao ni kula na kushibisha matumbo yao kwa vijisenti vya maskini!

Umewahi kuwasikia hata siku moja wakiweka mikakati makanisani mwao ya jinsi ya kuwasaidia maelfu ya maskini na yatima tuliono? Kati ya vitu wasivyopenda kusikia watu hawa ni huduma kwa watoto yatima, wajane na walemavu.

Kwa tabia hiyo ya maaskofu hao hujipatia fedha nyingi kwa njia ya sadaka, mavumo makubwa kutoka waumini wao ambayo huwapa kiburi na kujiona miungu watu na kutoona haya kuwasema maaskofu wa ukweli, walioupata uaskofu wao darasani na kwa uwezo wa Mungu muumba mbingu na ardhi.

Sikubaliani na maakofu hawa matapeli kwa sababu baadhi yao tunafahamu vizuri historia zao na maisha yao kwa ujumla, historia ya maisha machafu na tabia za kishetani ndio maana wanakimbilia katika ulokole ili kusafisha historia zao ndani ya jamii, huku baadhi yao wakifanikiwa kuanzisha hata makanisa lakini ukiangali kwa ukweli hayana hata hadhi ya kuitwa makanisa.

Naamini makanisa kama haya ya kina Gwajima na maaskofu wengine kama kina Gwajima ndio yale ya manabii wa uongo walioelezwa na Yesu Kristo, mbele ya wanafunzi wake kwamba watatokea mwisho wa dunia na wengi watajifanya wana uwezo wa kuponya.

Makanisa haya yanayoibuka kama uyoga hayana tofauti na yale yaliyotokea Uganda ambako Kibwetere aliwafungia ndani waumini wake na kuwateketeza kwa moto.

Rai yangu kwa Serikali: Upo umuhimu mkubwa sasa, pamoja na uhuru wa kuabudu kwa mujibu wa katiba yetu lakini mamlaka ya usajili wa makanisa na misikiti iwe makini kwa watu wanaojianzishia madhebu kila kukicha kwani mengine yamekuwa yakiwatia umasikini Watanzania na kuleta uchochezi hapa nchini.

Kwa wewe ambaye hujawahi kusikia mapepo yakiongea ndio huwa yanaongea hivyo sasa ni kazi ila lazima kusudi litimie.
 
Back
Top Bottom