TUWACHORe

TUWACHORe

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,114
Reaction score
34,957
1540557_711412665544106_601141664_o.jpg


Mdada akila majani ambayo huduma hiyo wanasema ni chakula kutoka mbinguni mwe!
 

Mdada akila majani ambayo huduma hiyo wanasema ni chakula kutoka mbinguni mwe!

Kuna mengi ambayo yamekuwa yakizungumzwa kuhusu huduma za watumishi mbalimbali, moja wapo ni hii huduma iitwayo Rabboni Centre ministries iliyopo Pretoria nchini Afrika ya kusini, huduma hii iliyochini ya mwanzilishi wake mwalimu ,mchungaji na nabii Daniel Lesego ilianza mwaka 2002. Ni huduma ambayo kwa watu wasioabudu hapo huitilia mashaka kutokana na mwenendo wake.

Kwasasa wapo kwenye mfungo ambao watu hufika kanisani na hatimaye wanaishia kula majani yaliyopo nje ya kanisa hilo akisema kwamba Roho Mtakatifu huongoza mtu kula chochote huku ikidaiwa kuwa manyasi hayo ni chakula kutoka mbinguni.

Inaelezwa kwamba mara baada ya maombi waumini wengi huanza kutapika jambo ambalo kanisani hapo huashiria kwamba mtu amejazwa Roho Mtakatifu.

Lakini kama haitoshi nabii Lesego hufanya maombi huku amewakanyaga watu. Huduma hii imekuwa gumzo nchini humo na nchi jirani kwa jinsi mambo yao yanavyokwenda.

Mnasemaje watumishi kuhusu jambo hili? mwe kula manyasi kweli? mma!


Hapa nabii huyo akikanyaga watu kama njia ya mafundisho yake.

Haa!! angalia jamani, sasa ng'ombe watakula nini jamani???

Mungu tufunulie macho ya rohoni kuyajua mambo haya kama ni wewe au sisi kha!

Hajamaliza bado.

Baada ya manyasi ni mwendo wa kutapika sasa









Picha ya juu na hii huyu ndio nabii Lesego Daniel mwenye maono na huduma hii.

Watu wanajaa kwenye huduma.

Mwe! kama uti wa mgongo shida hii dawa

Maombi yanaendelea.

Waumini wakikaribisha mwaka mpya.

Nabii anafundisha huku skuna yake imekanyaga mtu, sijui



Tembelea TOVUTI YAO Picha zote kwa hisani ya ukurasa wao wa Facebook.
 
Duniani kunamambo na mambo yenyewe ndo kama haya sasa alafu hapo kuna watu unakuta wanaelimu zao tena nzuri tu wanafanyishwa mambo kama haya kazi kwelikweli.
 
dah!! ngoja niwaache wenye iman zao labda kuna watakacho jifunza juu ya issue hii.
 
Duniani kunamambo na mambo yenyewe ndo kama haya sasa alafu hapo kuna watu unakuta wanaelimu zao tena nzuri tu wanafanyishwa mambo kama haya kazi kwelikweli.

KANISA HILO LIPO NIGERIA SIO HAPO NYUMBANI.





 
Last edited by a moderator:
Kuna mambo ya kijinga sana yanaendelea humu duniani
Kila kitu imani kama kweli imani hii kaja nayo na kutufundisha Bwana Yesu Kristo mimi sitoweza kuifuata kabisa kwanini nile majani? Ng'ombe na mbuzi watakula nini?
 
Kila kitu imani kama kweli imani hii kaja nayo na kutufundisha Bwana Yesu Kristo mimi sitoweza kuifuata kabisa kwanini nile majani? Ng'ombe na mbuzi watakula nini?

No, watu wanaangamia kwa kukosa maarifa, hapo hajuna cha nabii wala mtume. Mtume au Nabii lazima adhibitishwe kwa mujibu wa Biblia, siyo watu kama hawa wanaojipachika huduma kwa mgongo wa Ukristo kumbe ni wahuni tu. Watu wanadanganywa kwa sababu hawataki kujifunza na kujua bible inasemaje wanakimbilia kuombewa wapate miujiza.
 
Ukiisha mtu nafasi kubwa sana ya kumiliki uwezo wako wa kufikiri,ni angalabu kutotumika kwa namna ambayo ambao hawatumiki hawatasita kukuona mwehu...
 
Ni ngumu sana kumuelewa na kuelewa maarifa ya huyu tumuitaye Mungu...
 
nayeye anaonesha mfano wa kula hizo nyasi au ni kwa wafuasi wake tu,kweli dunia ina mengi
 
Back
Top Bottom