Serikali lazima ifikie maamuzi magumu kufuta kabisa waganga wa kienyeji nchini bila hivyo mauaji haya yataendelea. Mzizi mkavu utakubaliana na mimi kuwa ninyi waganga wa kienyeji rasilimali mnazotumia kutengeneza dawa zenu ni kutokana na binadamu na mimea kama ilivyo kwa madaktari rasmi , hauwezi kutengeneza tiba ya binadamu bila kutumia mwili wa binadamu.
Upande wa tiba rasmi wanasheria na taratibu zinazowalinda kutumia mwili wa binadamu aliyekufa ( CADAVAR ) katika kufanya tafiti, kutengeneza dawa , na kujifunzia namna ya kumtibu binadamu .
Hata upande wenu waganga wa kienyeji , huwezi kunishawishi kuwa mnatunia tuu mimea kutegeneza dawa za kumtibu binadamu bila kutumia baadi ya rasilimali kutoka kwenye mwili wa binadamu ili kutengeneza dawa za kumtibu binadamu. Swali linakuja rasili mali hizo mmnazipata wapi na mnaongozwa na sheria ipi? wenzenu wa tiba rasmi wanasheria zinazowalinda ijapokuwa hiyo wanaosema cadavar act haijatungwa.
Matokeo ya kuishi kinafiki na kutokuliweka sawa hili jambo limekuwa likisababisha kufukuliwa kwa makaburi ya wapendwa wetu na kuibiwa viungo vyao, kuuwawa kwa watu na kuchukuliwa viungo vyao hali hii imekuwa ni hatari sasa na serikali inabidi iliweke wazi suala hili sasa lipime umuhimu wa kuendelea kuwa na hizi tiba za gizani za kutafuta rasilimali kwa kujificha jificha na kwa njia haramu au kuzifuta kabisa na kutegemea tiba rasmi tuu.
Hii habari ya baadhi ya waganga wa kienyeji kuja mjini na suti na tai wakiwakandya wenzao kwamba ,eti wao wamesajiliwa , kwamba wanatambulika na fufunga dawa zao kwenye chupa rasmi , ni waongo wakubwa. Wanaweza wakawa either ni matapeli wakubwa hawajui lolote kuhusu tiba hizo , ni mazingaumbwe tuu , wanachanganya na usanii na wanachokifanya ni kuchukua majuice na kuyapeleka TFDA kwenda kudhibitisha kuwa sio sumu na hakuna mamlaka yoyote inayothibitisha kuwa zinatibu au la. Au mchana wanajifanya wapo kwenye suti na kwenye vyama vya waganga wa jadi, usiku wapo bise wanafukua makaburi kutafuta viungo vya binadamu. Serikali sasa, ichachamae na kufuta waganga hawa kwani hata magonjwa wanaodai kuwa wanayatibu wizara ya afya , na mashirika ya afya duniani kote yamethibitisha kuwa hakuna dawa wala chanjo ya magonjwa hayo ,iweje watu wajinadi kuwa wanayatibu na srikali inyamaze tuu????