Tuwaache mafisadi waendelee kupeta!?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuwaache mafisadi waendelee kupeta!??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jan 5, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,921
  Likes Received: 83,430
  Trophy Points: 280
  Mbatia ataka mafisadi waachwe

  2009-01-05 14:24:34
  Na Muhibu Said​
  Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, amewataka Watanzania kuachana na mtindo wa sasa wa kundi moja kulinyooshea kidole lingine kuhusu kashfa za ufisadi na kutumia madaraka vibaya akisema kwamba kitendo hicho kinaigawa nchi.

  Sanjari na kuigawa nchi, Mbatia, ambaye muda wa uongozi wake katika chama hicho ulifikia tamati jana, aliuambia Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa chama hicho kuwa kitendo hicho pia kinakwamisha uzalishaji kwa vile hakuna aliyemsafi katika kashfa hiyo tangu enzi za utawala wa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere.

  Badala yake, amewataka Watanzania wakae chini na kujadiliana kuhusiana na suala la ubinafsishaji, ambalo alisema ndio chanzo kikubwa cha kuibuka kwa kashfa hiyo.

  Mbatia alisema hayo alipokuwa akitoa nasaha katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa chama hicho, uliofanyika katika ukumbi wa kituo cha Msimbazi, jijini Dar es Salaam.

  Alisema suala la kutumia madaraka vibaya, ni la muda mrefu kwa Watanzania nchini na kwamba hakuna asiyeguswa kwa namna yo yote na kashfa hiyo.

  ``Kwa mfano, jana (juzi) alikuja mtu ofisini kwangu kutoka Mtwara, akaniambia kuwa usikanyage Mtwara na hoja yako ya kutaka Mkapa aondolewe kinga ili ashtakiwe, akaniambia kama unataka Mkapa aondolewe kinga, basi aondolewe na Mzee Mwinyi pia, kwa kubariki ubadhirifu wa IPTL (mradi wa kuzalisha umeme) wakati wa utawala wake.

  Hata leo Nyerere akifufuka ataambiwa alitumia madaraka yake vibaya, hivyo naye ashtakiwe. Kila mtu anamnyooshea mwingine kidole,`` alisema Mbatia.

  Alisema nchi hivi sasa imefikia pabaya, ambapo Watanzania wameanza kuitana mafisadi, baada ya kuacha kuitana ndugu na mheshimiwa, kama walivyokuwa wakifanya hivyo huko nyuma.

  ``Tumetoka kwenye kuitana ndugu, tukaenda kwenye kuitana mheshimiwa sasa tumekwenda kwenye kuitana mafisadi.

  Kama hujatoa kibanzi katika jicho lako, ona boriti la jicho lako,`` alisema Mbatia, ambaye kauli zake zilionekana kupingana na juhudi za makundi mbalimbali ya jamii nchini kupinga vitendo vya ufisadi.

  Alisema amesikitishwa na gazeti moja nchini, ambalo lilimkariri wakati akiwa masomoni nje ya nchi akishauri Rais Mstaafu Benjamin Mkapa aondolewe kinga ili ashtakiwe mahakamani kwa tuhuma za ufisadi zinazomkabili, wakati hakuwahi kusema kitu kama hicho.

  ``Naviomba vyombo vya habari vinitendee haki,`` alisema Mbatia akimaanisha kuwa haungi mkono hoja zinazotolewa na baadhi ya watu kuwa Mkapa anapaswa kushitakiwa kutokana na kutumia vibaya madaraka yake katika mchakato wa ubinafsishaji wa mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, mkoani Mbeya.

  Mkapa na wenzake wanadaiwa kujimilikisha hisa asilimia 80 kupitia Kampuni ya Tan Power Resources Limited kwa Sh. milioni 700 badala ya thamani halisi Sh. bilioni nne. Pia wanadaiwa kulipa Sh. milioni 70 tu.

  Kutokana na hali hiyo, Mbatia, aliyekuwa akigombea uenyekiti wa chama hicho, aliwataka Watanzania kutoa hoja zenye kujenga ustawi kwao badala ya kuendelea na mjadala unaozua mgogoro miongoni mwao, ambao alidai kuwa unaigawa nchi na kukwamisha uzalishaji.
  ``Hakuna uzalishaji, ni mjadala tu wa mgogoro,” alisema Mbatia.

  Naye Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu huo, alivitaka vyama vya siasa kutekeleza yale wanayosema.
  ``Ninavitaka vyama vya siasa, wazingatie wanayosema.

  Wamekuwa wakisema kuwe na mshikamano na tuwe na utaifa. Watekeleze kwa vitendo. Siyo baada ya hapo kila chama kinafuata yake,`` alisema Tendwa.

  Pia, alisisitiza mahitaji ya mabadiliko ya sheria ya ruzuku na kuvitaka vyama vya siasa kuwafikia wananchi na pia serikali ibadilike na kudhibiti rushwa katika vyama vya siasa.

  SOURCE: Nipashe
   
 2. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2009
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  jibu hoja zake siyo kumshangaa tu mheshimiwa bubu, haitusaidii kushangaaa
   
 3. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Masikini Mbatia sijui sikuhizi kawaje? Zamani alikuwa akiongea mambo ya maana lakini siku hizi ni utata mtupu!
   
 4. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #4
  Jan 6, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anakula hela za mafisadi lazima awatete kwa vyovyote vile; Wamemnunulia malori; wamemkirimu kwa kazi iliyofanyika tarime nk; so lazima sasa lengo lake kuungana na CCM si muda mrefu.
   
 5. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #5
  Jan 6, 2009
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Laiti NCCR isingekuwa chama kibaraka basi muda huu kingeshakuwa marehemu.SUrvival strategy ya Mbatia na wenzake ni kuendelea kujikomba kwa nguvu kwa CCM na mafisadi ili chama hicho kiendelee kuwa hai.Safari ya ukombozi halisi wa Mtanzania bado ni ndefu sana.
   
 6. Haki.tupu

  Haki.tupu JF-Expert Member

  #6
  Jan 6, 2009
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hakuna hoja ya Bubu kujibu! Si kila asemacho mtu ni hoja.
   
 7. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #7
  Jan 6, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Mbatia hana mbunge hata mmoja kwahiyo hana ruzuku ya Tendwa!! wafuasi nao njaa tupu kwahiyo lazima ajiuze to the highest bidder na kwasasa bidders wanaolipa ni mafisadi. Siasa za Mbatia sikukuhizi ni kuwatetea hao wezi ili wammegee!! Mbinu anayoitumia ni kwa kuitisha press conference na waandishi wa magazeti basi kwani mikutano ya hadhara hawezi kupata mtu hata mmoja! Ukisikia mamluki wa kisiasa ndio hawa.
   
 8. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #8
  Jan 6, 2009
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  NCCR-MAGEUZI ni chama cha CCM toka mwanzo. Angalia orodha ya viongozi wake waliorudi nyumbani kwao (CCM): Lamwai, Wassira, Nsanzugwanko, Nyakyoma, Bagenda na wengine wengi. Kazi yao ilikuwa kuvuruga upinzani. Hata hawa akina Mbatia ni watoa taarifa (informers) na watu wa kutumiwa kuvuruga harakati na kampeni za mageuzi. Ndiyo maana NCCR kama chama kiko hoi lakini akina Mbatia binafsi wana magari ya kifahari, majumba na siha zinazoashiria kuwa wana wajomba mahali. Sitashanga wajomba hao ndiyo hao hao mafisadi.
   
 9. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #9
  Jan 6, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Kwani alichosema hakina maana kwako? Pengine kina maana elfu mia kwa wananchi wengine wenye nia kama yake. Wala huna haja ya kumwonea huruma! Suala hapo ni kuikubali hoja yake ama kuipinga.
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  Jan 6, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nadhani Mbatia alinukuliwa vibaya na mwandishi wa habari. Kama ni kweli alisema hayo kwa Watanzania basi anatatizo kubwa sana kwenye uchanganuzi wa mambo.
   
 11. mwakatojofu

  mwakatojofu JF-Expert Member

  #11
  Jan 6, 2009
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni kweli wapo wengi wakuwashughulikia. ni wengi zaid ya wanaoshughulikiwa au watakao shughulikiwa.
  katika jamii zetu tuna wahalifu wengi. wez wa kuku, wagomvi, watumiaji madawa ya kulevya na wauzaji wao na nk.
  unafikiri tunawakamata wote? subutu! ni sehemu ndogo tu ndo tunashughulika nayo na sababu ni ugumu wa kuwa kamata wote, nyenzo chache tulizonazo na nk. lakin wanaonusurika wanakaa wakijua kuwa wanawindwa na wakikamatwa a, b, c, mpaka z kitawapata.

  tusichoke kusema hiki na kile si kizuri eti kwasababu watu wengi wanakifanya au walikuwa wanakifanya. walikuwa wanafanya ndo maana leo tunasema tuko nyuma hatupigi hatua mbele kama taifa. je waendelee kuharibu au tujaribu kuwadhibit? tuliwaachia wakatuharibia. tujaribu kuwadhibit huenda ikawa the opposite

  ``Hakuna uzalishaji, ni mjadala tu wa mgogoro," sa kama unazalisha wengine wanakwapua utabakiwa na vingapi? assume unajaza ndoo maji na kwa chini imetoboka. ndoo itajaa saa ngapi?

  cha muhimu ni kuwa asionewe mtu. kuonea nako ni ufisadi
   
 12. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #12
  Jan 6, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mimi namuunga mkono Mbatia, kwa sasa wengi wataona ni mwehu, lakini ndio moyo wa kizalendo!

  Tunapoteza muda tu, kuna mafisadi kama wafanyakazi wa kawaida maofisini wanaojiwekee safari zisizokuwa na tija na posho za ajabu ajabu kila siku....

  Tangu lini mtu anayelipwa 500,000/= awe na nyumba ya millioni 800 tena wakati huo huo anaenda kazini ati kutafuta sh. 500,000/-

  Wizi mtupu kila mahali!
   
 13. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #13
  Jan 6, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  ....kujiunga na chama tawala is of little effort, the opposite is also quite true!!
   
 14. A

  Alpha JF-Expert Member

  #14
  Jan 6, 2009
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 614
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  So we should just allow everybody to steal without any consequences? While we are at it why don't we just get rid of all traffic laws. Everybody breaks them so we are just wasting time trying to enforce them. Actually why not just get rid of all laws, they are a waste of time.

  We must be the smartest people on earth i wonder why every other country has not thought of this. They must all be stupid.

  :rolleyes:
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Jan 6, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,921
  Likes Received: 83,430
  Trophy Points: 280
  Mbatia remarks on corruption provoke storm

  2009-01-06 11:41:30
  By Correspondent Felister Peter  Politicians have challenged a statement given by NCCR-Mageuzi Chairman James Mbatia on people suspected of corruption, with MP Anne Kilango saying Mbatia is now speaking like a priest.

  Mbatia was quoted on Sunday as saying that public leaders who are currently facing charges of abuse of office, tax exemption and occasionally loss to the government should be freed because there is no single honest and clean person in Tanzania.

  The Member of Parliament for Same East Ane-Kilango Malecela told ‘The Guardian’ in a telephone interview yesterday that with all the efforts that President Jakaya Kikwete has made to fight corruption, there was no way someone could emerge and demand that people accused of corruption should be freed.

  She said that Mbatia had to make his statement clear and manifest his stance on whether he supported or fought corruption so that he could be challenged.

  ``I don`t understand what Mbatia is talking about because everyone has his own capacity of thinking and analysing issues.

  I want to exactly know whether he is supporting or fighting corruption``, said Kilango.

  Dr Wilbroad Slaa, Member of Parliament for Karatu, said he has been shocked by Mbatia`s statement and that his argument could not change the attitude of other people.

  He said if Mbatia was coward, then he did not have the confidence to fight corruption. ``He better stays away and leaves other people who are committed to continue with the struggle.``

  Dr Slaa said Mbatia\'s statement would not demoralise them as they would continue fighting for the country`s resources not to be exploited by few people.

  ``If Mbatia is not clean, then it is okay. He should not try to convince other people to believe that all Tanzanians are corrupt,`` he said.

  The Member of Parliament -Bariadi East, John Cheyo said there was no way dishonest people should be left free. Any person who commits an offence must face the law, Cheyo said.

  Mbatia was quoted yesterday saying there is no honest person in this country and so he doesn`t see the reason why few people should be taken to court.

  He said if properly investigated, every one would be found with faults. He said Tanzanians must now think of privatisation which is the main source of all the current problems.

  He went further saying that if it was a matter of taking to court every corrupt person, then former presidents Ali Hassan Mwinyi and Benjamin Mkapa should be charged because there were so many corrupt incidences during their reigns.


  Mbatia was also quoted as saying that if Mwalimu Julius Nyerere was still alive, once investigated, he would also have been found with corruption scandals.

  More than 20 people have also been arraigned in court allegedly for stealing from the Bank of Tanzania`s External Payment Arrears (EPA) account.

  SOURCE: Guardian ​
   
 16. mwakatojofu

  mwakatojofu JF-Expert Member

  #16
  Jan 6, 2009
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tusiwaachie mafisadi. kweli watu wengi ni mafisadi lakini si wote.
  tubuni mbinu na mikakati ya kushughulika na wote wanaoharibu - kama kuelimishana, kuongezana mishahara yetu ikidhi mahitaji. tukiacha hali kama ilivyo hatutokaa tufike popote kama taifa.
  tutakuwa taifa la wezi.
  kila mtu atakuwa anaiba.
  ndo unapotaka tuelekee?
  haiwezekani
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Jan 6, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,921
  Likes Received: 83,430
  Trophy Points: 280
  Tunapoteza muda kupambana na mafisadi!!!!?:confused: :confused: :confused:
  Hii ya leo kali!!!!
   
 18. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #18
  Jan 6, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mbatia anakula halua ya mafisadi na ndio wanaomfadhili,huyu bwana alitumwa kumng'oa Mrema ili NCCR kiwe CCBb,fuatilia matukio ya viongozi wake tangu mwanzo,kuna mamluki wengi waliopandikizwa kama anavyosema Liundi.Sasa mafisadi wanaifanya NCCR kichaka chao kutokana na njaa ya viongozi wake.Hiyo ndiyo TZ na Viongozi vyama vinavyojiita pinzani.
   
 19. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #19
  Jan 7, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kibunango soma post ya Ushirombo chini ya post yako hii
   
 20. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #20
  Jan 7, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tukiwaachia wahalifu wowote (wawe mafisadi au wengineo) ni kosa kubwa. Kufikiria kuachana na mafisadi ni kukosa uzalendo. Inawezekanaje kiongozi wa chama mwenye heshima na nia ya kuona ustawi wa nchi ashauri Mafisadi (wezi wakubwa) waachwe huru? Mimi nashangaa sana kauli za baadhi ya viongozi. Anataka nchi iweje hii? Mbona sijasikia hata mara moja akitaka wezi wadogo wadogo waachiwe huru? Au amelambishwa asali?
   
Loading...