Tuutathimini uhusiano wetu na Israel

Tuutathimini uhusiano wetu na Israel

Joined
Oct 5, 2015
Posts
90
Reaction score
483
TUUTATHIMINI USHIRIKIANO WETU NA ISRAEL.

Kuna haja ya kutathmini uhusiano wetu na Israel. Na ikiwa tunataka mashirikiano na Taifa hilo lisilo na mipaka rasmi ya kijiografia, ni vema tukawa na ajenda rasmi inayotulazimu kuwa na uhusiano nayo lakini ajenda hiyo isituzuie kukemea ukatili wa Israel dhidi ya binadamu.

Israel imekuwa ikilaumiwa na mataifa mengi duniani kwa vitendo vyake dhidi ya Palestina. Mwaka 1967, baada ya vita ya siku sita (six days war) dhidi ya mataifa ya kiarabu, israel baada ya ya kushinda vita ile iljimilikisha ardhi isiyo yake. Ardhi ya peninsula ya sinai ya Misri, ardhi ya miinuko ya Golan ya Syria, ukanda wa Gaza wa palestina na uzio wa magharibi.
Baadae mwaka 1973 Misri iliivamia Israel na kufanya vita iliyoitwa Yom Kippur ambayo ilipelekea mkataba wa amani uliorudisha ardhi ya Sinai mikononi mwa Misri, huku milima ya Golan ikirudi chini ya Syria. Lakini vita ya mwaka 1980-81, ilipelekea sehemu ya milima ya Golan kuwa chini ya miliki ya Israel, pamoja na kuichukua sehemu ya Mashariki ya mji wa Yerusalemu.
Kumeendelea kuwa na vita ndogondogo (skirmishes) na vurugu za kugombea ardhi kwa miaka nenda rudi. Watu wengi wameuawa, wengi zaidi ni wapalestina wasio na nguvu.

Ni mwaka 1967, baada ya "Six day war" Mwalimu Nyerere alitangaza sera ya nje, iliyopinga uonevu na uvamizi wa ardhi ya nchi ingine. Mwalimu alisema, pamoja na mambo mengine, kwamba; uonevu ni uonevu bila kujali nani anafanya au nani anafanyiwa. Na kwamba Israel inapaswa kuheshimu binadamu wengine.

Mwalimu aliongeza kwamba, Palestina ni nchi yenye watu tofauti, wenye itikadi tofauti, imani tofauti na historia tofauti kama ilivyo Israel, na kwamba suala la kukemea Ukatili wa Israel dhidi ya Palestina sio suala la kiimani, wala kiitikadi, wala kihistoria, bali ni suala la ubinadamu.

Wakati huo Mwalimu akitoa msimamo huo, Tanzania na Israel walikuwa na mahusiano ya kidiplomasia. Ubalozi wa Israel ukiwa umefunguliwa mwaka 1963. Lakini mwaka 1973, Israel ilifunga ubalozi wake baada ya uhusiano kudhoofika zaidi. Nchi nyingi za Afrika zilifuta uhusiano wa kidiplomasia na Israel. Zipo pia nchi nyingi za Afrika ambazo hazikuwahi kuwa na uhusiano wa kibalozi na Israel, zikiwemo nchi zote za kiarabu, kasoro Misri.
Baada ya Mwalimu Nyerere kutangaza kutambua uhalali wa mamlaka ya ukombozi wa Palestina (PLO) mwaka 1973, ndipo ubalozi wa Israel ukafungwa rasmi. Mwaka 1980, Marekani ilifungua ubalozi wake katika jengo hilo lilokuwa la ubalozi wa Israel, ambalo mwaka 1998 lilikumbwa na shambulio la ugaidi kwa kulipuliwa sambamba na ubalozi wa Marekani mjini Nairobi.

Wakati tukiwa na mahusiano ya kibalozi na Israel, Tanzania ilinufaika. Barabara nyingi za jiji la Dar es salaam zilijengwa na Israel ikiwemo barabara ya Mandela ya wakati huo. Tanzania ilinufaika pia kwenye teknolojia ya viwanda na kilimo. Inasemekana mfumo wa vijiji vya ujamaa ulioanzishwa na Mwalimu Nyerere ulikuwa ni mfano wa mfumo ulioitwa Kibbutz wa Israel, huku mfumo wa kilimo ukiwa ni mfano wa mfumo wa Israel ulioitwa Moshav.

Lakini pamoja na mahusiano hayo, Mwalimu hakusita kusema ukweli na kusimamia alichokiamini. Mwalimu hakuwa mtu wa kushangilia ukatili wa Israel, iwe kwa sababu za kiitikadi, kiimani, au kihistoria. Na vivo hivyo, hakuunga mkono kila kitu walichodai wapalestina, au washirika wao, kwa mfano, mwalimu hakuunga mkono wazo la kuifuta Israel kwenye ramani wa dunia. Na hakuamini katika nia yoyote ovu dhidi ya Israel. Alionesha imani yake hiyo kwa vitendo.
Labda kwa sababu Mwalimu Nyerere alikuwa mtu anayetambua na kujitambua pia, badala ya kuishi kwa kufuata mkumbo au ushawishi wa mtu mwenye nguvu.
Na sera hiyo ya Mwalimu ndiyo iliyotambulisha Tanzania katika ulingo wa kimataifa. Hata pale uhusiano wa kidiplomasia uliporudi, kulikuwa na sababu za msingi ambazo ni pamoja na mkataba wa amani wa Oslo wa mwaka 1993. Ndipo mwaka 1995, uhusiano ulianza upya na balozi wa Tanzania wa Misri akaongezewa jukumu la kuhudumu Israel na Balozi wa Israel wa Kenya akaongezewa jukumu la kuhudumu pia Tanzania.

Sasa tumeshuhudia ufunguzi rasmi wa balozi ndani ya mipaka yetu, na Sisi (Tanzania) tukifungua rasmi ubalozi wa Tanzania mjini Tel Aviv, Israel. Lakini tukio lilofuata siku chache baadae, la mauaji ya wapalestina zaidi ya 60 sasa, ni jaribio kubwa la kidiplomasia. Jambo lenye ukakasi hapa ni kitendo cha Tanzania kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa ubalozi wa Marekani mjini Yerusalemu, huku, maili chache kutoka eneo la sherehe hizo, ardhi ilipata kunywa damu za wapalestina waliokuwa wakipinga kitendo hiko cha Marekani kufungua ubalozi mjini Yerusalemu. Maelfu ya wapalestina wamejeruhiwa.

Mataifa yaliyohudhuria sherehe hizo ni Mataifa 32 kati ya 86 yalioalikwa. Ni baadhi ya mataifa masikini ya Afrika, kusini mwa jangwa la Sahara. (Tanzania, Kenya, Rwanda, Zambia, Ivory Coast, Cameroon, jamuhuri ya Congo (Congo Brazzaville) DRC (Congo Kinshasa), Ethiopia, Sudan kusini na Angola. Mengine ni Mataifa madogo ya ulaya mashariki na baadhi kutoka Asia.
Kutoka Amerika ya kusini ni Peru na Paraguay pekee.
Katika mataifa 20 yenye uchumi mkubwa duniani, hakuna moja lilohudhuria, ukiacha US wenye ubalozi wao.

Kususa kwa Mataifa mengi, hasa yanayojimudu kiuchumi ni ishara ya kutokubaliana na Kitendo cha US kuhamishia ubalozi wake mjini Tel Aviv, lakini pia mauaji ya wapalestina yalioambatana na sherehe hizo ni kielelezo kwamba, mgogoro wa eneo hilo bado ni mkubwa, na haifai kuunga mkono vitendo vinavyolenga kuchochea mgogoro huo.
Kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa ubalozi wa US mjini Yerusalemu ni matokeo ya kuburuzwa na mawazo ya wenye nguvu, na kukubaliana na mambo yasiofaa kwa sababu tu yanafanywa na mtu mwenye uwezo, kinyume na misimamo ya baba wa Taifa. Lakini pia ni kujifedhehesha mbele ya washirika wetu wengine hasa wale waliopinga suala hilo kwa kutohudhuria.

Kwa muktadha huo kuna haja ya kutathmini upya, mahusiano yetu na Israel. Tanzania ni nchi huru inayopaswa kujisimamia. Ni vema Tanzania ikaamua kuwa na msimamo wake. Mawili yanawezekana; la kwanza ni kurudi kwenye misingi iliyowekwa na Mwalimu Nyerere. Misingi iliyotambulisha Tanzania kama nchi iliyo mstari wa mbele katika kutetea haki za binadamu na ubinadamu. Na kwa hivyo, tukemee vitendo vyote vilivyo kinyume na msimamo huo. Tukifanya hivyo, dunia itatuelewa.
Au, tukitaka kuachana na misingi hiyo basi tuchague upande mmoja. Hatutaeleweka kama tukiunga mkono Waisrael katika vitengo vinavyokiuka haki za binadamu wa Palestina, na kuchochea migogoro, wakati huo huo tuna ubalozi wa Palestina na tunashirikiana nawo. Haieleweki kushirikiana na maadui wawili katika vitendo vinavyokoleza uadui wao. Kama tunashirikiana na wote basi ni vema tukachagua maeneo yasiohusiana na uadui wao. Hata Israel wenyewe wameamua kuwa na ushirikiano na sisi wakijuwa sisi tuna mashirikiano ya kibalozi na Palestina.
Urusi ni mfano mzuri, wanashirikiana na Israel na Iran ambazo ni maadui wakubwa. Israel na Iran wanapogombana, kazi ya Urusi ni kusuluhisha au kukaa kimya, lakini sio kuchagua upande. Februari mwaka huu wa 2018, Israel na Iran walirushiana makombora kwenye maeneo ya Alepo huko Syria. Alichofanya Rais Putin ni kumpigia simu Benyamin Netanyahu wa Israel na kumshauri waache utoto. Lakini April mwaka huu, baada ya kuanza tena majibizano ya maroketi na maguruneti, Putin amekaa kimya. Urusi vilevile haikuudhuria sherehe za ufunguzi wa ubalozi wa US mjini Yerusalemu, pamoja na ziara aliyofanya waziri mkuu wa Israel, Benyamin Netanyahu mapema mwezi mei. Pamoja na kualikwa lakini haikuhuduria.

Kitu gani kilichofanya Tanzania ihudhurie sherehe hizo, huku historia ikitoa ishara ya wazi ya kutokea kwa mauaji yaliyotokea siku hiyo?

Tanzania haikupiga kura kwenye baraza la usalama la umoja wa Mataifa kuunga mkono kuhamishwa kwa ubalozi wa US kutoka Tel Aviv kwenda Yerusalemu, vilevile ubalozi mpya wa Tanzania umejengwa mjini Tel Aviv. Sasa ni nini kilichofanya tukale ubwabwa kwenye sherehe hiyo ya Yerusalemu?

Sasa tuna deni na Palestina. Tuna uhusiano wa kibalozi na Palestina, ambao raia wake wameuawa wakipinga uvamizi wa Israel na ufunguzi wa Ubalozi wa US mjini Yerusalemu huku maofisa wa Tanzania wakila ubwabwa. Angalau kwa kila kijiko cha ubwabwa walichokula maofisa wa Tanzania, roho mbili za wapalestina ziliaga dunia. Tunawaambia nini wapalestina walioamini tunashirikiana nawo?

Mbaya zaidi, hatusikii tamko la serikali kupinga mauaji yale, au hata kutuma salamu za pole kwa wapalestina! Hiki ni kielelezo cha aibu kwenye uwanda wa diplomasia.
Serikali itoe ufafanuzi haraka, tunawahitaji waisrael kwa mashirikiano, lakini hatuwezi kuwaunga mkono katika ukatili wao.

Israel na Palestina wote ni wanadamu na wote wanastahili kuwa na ardhi ya kuishi. Wote wana haki sawa na wote wapewe ushirikiano mahali wanapohitaji, na wote wapingwe wanapokosea.
Tanzania iwe na msimamo huo.
Mungu ibariki Tanzania.
 
Izrael walishafanya watu wajinga, waliwatengenezea Mungu, wakawatengenezea maandiko jinsi ya kumuabudu huyo Mungu na pia wakawatengenezea dini ya kumuabudu Mungu.

Zaidi wakawaambia usipowaombea huyo Mungu waliemtengeneza hatakubariki.

Kwa namna yoyote waamini wa dini za kiyahudu hawawezi kukuelewa.

Izrael inaua wapalestina huku watu wanaiombea, kila ikiua watu wanaiombea iendelee kuua.
 
Natumai bado kama taifa siasa yetu kimataifa ni kutofungamana na upande wowote.Tuangalie masilahi ya taifa letu kwanza.Israeli kama taifa litakuwepo tuwaunge ama tuwatenge.Tuangalie uhodari(strength) wao kwa maslahi ya taifa letu maisha yasonge mbele.
 
Mtoa mada bahati nzuri unajua vema sababu za kuimarika kwa ushirikiano wa pande hizo mbili katika kipindi hiki. In short kuna watu wanaamini kupinga uovu wa waisrail ni kuitafuta laana na kuwakubalua kwa kila kitu ni kujiongezea baraka katika nchi. Safari bado ni ndefu sana wajamen, katika kuendea maendeleo.
 
Tulipokuwa na mahusiano ya kidiplomasia na Palestine,Israel walifunga balozi yao hivyo hivyo kwa muktadha huu Palestine wanaweza kufunga wa kwao pia.
 
Sijaelewa kwa nini tuliwakumbatia Wapelestina kama hatufungamani na upande wowote? Sasa kwa nini tuna laumu kurejeshwa kwa balozi na kuhudhuriwa kwa sherehe za kufunguliwa ubalozi wa US kama hatufungamani upande wowote?
Na mwisho kwa nini kufungamana na Wapalestina sio kufungamana na upande wowote?
 
Izrael walishafanya watu wajinga, waliwatengenezea Mungu, wakawatengenezea maandiko jinsi ya kumuabudu huyo Mungu na pia wakawatengenezea dini ya kumuabudu Mungu.

Zaidi wakawaambia usipowaombea huyo Mungu waliemtengeneza hatakubariki.

Kwa namna yoyote waamini wa dini za kiyahudu hawawezi kukuelewa.

Izrael inaua wapalestina huku watu wanaiombea, kila ikiua watu wanaiombea iendelee kuua.
Huu ujinga umeenea duniani kote kwa hili mwl namkubali sana.
 
Mkuu Christopher nakulubali sana kwa maandiko yako, keep it up. Huu ni uandishi wa mtu aliyeenda shule.
 
Kwa mujibu wa taarifa, zaidi ya robo 3 ya waliouawa walikuwa Wanamgambo wa HAMAS waliojivika kama raia. Hii mbinu wanaitumia sana, kwa kujichanganya mashuleni, mahospitalini, sokoni nk,

IDF sio vichaa wa kushambulia raia wasio na hatia. Ni jeshi IMARA na intelijensia yao iliugundua huu mtego kitambo tu.

Siungi mkono raia kuuawa, lakini katika kuzitekeleza "RULES OF ENGAGEMENT" kunaweza kuwa na casualties chache za wasiohusika lakini targets zikafikiwa kwa wingi.

Mkuu, wewe ni DAKTARI, unajua vyema kuwa dawa zote za binadamu haziko exclusively SPECIFIC & SELECTIVE; Yaani mbali na kumlenga KIMELEA aliyeingia mwilini lakini pia zitadhuru baadhi ya normal cells za binadamu. Ndicho kilichotokea..!
Watu wafukunyuku, ushajua kama huyu jamaa ni daktari wakati hajajitambulslisha kwenye bandiko lake?
 
kuna sehemu mleta Mada kasema Barabara ya Mandela ilijengwa na Israel (wakati huo tukiwa na uhusiano na Israel)
Hapana Port access imejengwa 1980-1982 tena Kambarage alikuwepo, jambo hilo lisingewezekana
Wakati tukiwa na mahusiano ya kibalozi na Israel, Tanzania ilinufaika. Barabara nyingi za jiji la Dar es salaam zilijengwa na Israel ikiwemo barabara ya Mandela ya wakati huo. Tanzania ilinufaika pia kwenye teknolojia ya viwanda na kilimo. Inasemekana mfumo wa vijiji vya ujamaa ulioanzishwa na Mwalimu Nyerere ulikuwa ni mfano wa mfumo ulioitwa Kibbutz wa Israel, huku mfumo wa kilimo ukiwa ni mfano wa mfumo wa Israel ulioitwa Moshav.
 
Izrael walishafanya watu wajinga, waliwatengenezea Mungu, wakawatengenezea maandiko jinsi ya kumuabudu huyo Mungu na pia wakawatengenezea dini ya kumuabudu Mungu.

Zaidi wakawaambia usipowaombea huyo Mungu waliemtengeneza hatakubariki.

Kwa namna yoyote waamini wa dini za kiyahudu hawawezi kukuelewa.

Izrael inaua wapalestina huku watu wanaiombea, kila ikiua watu wanaiombea iendelee kuua.
mungu wao walomtengeneza ni la ajabu Sana lenyewe kazi yake kuwatuma watoto maovu tu,,,kuua kugeuzana na kupora ardhi za wengine, halafu ukikemea Hilo like mungu lao waloliunda ninakulaani
 
Natumai bado kama taifa siasa yetu kimataifa ni kutofungamana na upande wowote.Tuangalie masilahi ya taifa letu kwanza.Israeli kama taifa litakuwepo tuwaunge ama tuwatenge.Tuangalie uhodari(strength) wao kwa maslahi ya taifa letu maisha yasonge mbele.
Sio Sera ya Taifa letu kufumbia maovu dhidi ya binadamu wengine....
 
Mtoa mada bahati nzuri unajua vema sababu za kuimarika kwa ushirikiano wa pande hizo mbili katika kipindi hiki. In short kuna watu wanaamini kupinga uovu wa waisrail ni kuitafuta laana na kuwakubalua kwa kila kitu ni kujiongezea baraka katika nchi. Safari bado ni ndefu sana wajamen, katika kuendea maendeleo.
Jiwe anaogopa limungu lao litamlaani allkiwakemea kuuwa wapalestina Kama kuku....
 
Sera bado ni NAM na sasa tunatekeleza Economic diplomacy , hivyo nashangaa watu wanaingiza mambo ya imani ,

Kama ni kuuwawa ,watu wanakufa kila mahali mgogoro una miaka 70 ,kwanini hamas waendelee kuwatumia watu wasio na hatia kupigana vita

Tunahitaji teknolojia n.k kutoka Israel ,sisi tutabaki na maazimio ya UN na sio US lakini , pia lazima tuangalie maslahi ya Tanzania
 
Back
Top Bottom