Labrujita
JF-Expert Member
- Jun 12, 2015
- 399
- 126
Ndugu wana Jukwaa,
Ni takribani miaka kadhaa imepita Mustafa Sabodo alijitokeza na kujipambanua kama mwanamageuzi mwenye nia ya dhati kuona Tanzania ikisonga mbele huku akiwa kinara wa kuunga mkono harakati hizo kwa kufadhili vyama vya upinzani na hata baadhi ya mikutano ya vyama vya upinzani mfano mzuri ikiwa ni mkutano mkuu wa NCCR 2014.
Leo ametoka kivingine kwa kutangaza kuwekeza shilingi zaidi ya tilioni kumi katika makao makuu ya nchi mkoani Dodoma kwangu mimi hili sio NONGWA kwani nia ni kuendeleza ujenzi na ustawi wa maendeleo ya taifa letu japo ameniacha na maswali kadhaaa;

- Mr Sabodo amekuwa mfanyabiashara kwa muda mrefu na amejijenga vyema katika biashara zake katika mikoa mbalimbali ya nchi hususani Lindi na Daresalaam; kama Dodoma pekee atawekeza tilioni kumi huku kwingine anaweza akawa amewekeza sh ngapi?
- Kiasi cha tilioni kumi pekee kilichotajwa na huyu mtanzania mwenzetu ambacho kimsingi kinazidi budget ya serikali ya Tanzania kwa miaka minne iliyopita na kinazidi budget ya mwisho ya serikali ya Tanzania chini ya rais Mkapa karibu mara tatu kinaleta picha gani?
- Hivi kama budget ya nchi yetu kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ikiwa ni pamoja na kukopa imefika tilioni 29 inashindikanaje watu aina ya Sabodo kuizidi serikali pesa? hapa tuassume Dar es salaam na sehemu nyingine kwa ujumla amewekeza tilioni kumi na ushee.......