Tuunge mkono uwekezaji wa Sabodo Dodoma lakini tusiache kujifunza

Labrujita

JF-Expert Member
Jun 12, 2015
399
126
Ndugu wana Jukwaa,

Ni takribani miaka kadhaa imepita Mustafa Sabodo alijitokeza na kujipambanua kama mwanamageuzi mwenye nia ya dhati kuona Tanzania ikisonga mbele huku akiwa kinara wa kuunga mkono harakati hizo kwa kufadhili vyama vya upinzani na hata baadhi ya mikutano ya vyama vya upinzani mfano mzuri ikiwa ni mkutano mkuu wa NCCR 2014.

Leo ametoka kivingine kwa kutangaza kuwekeza shilingi zaidi ya tilioni kumi katika makao makuu ya nchi mkoani Dodoma kwangu mimi hili sio NONGWA kwani nia ni kuendeleza ujenzi na ustawi wa maendeleo ya taifa letu japo ameniacha na maswali kadhaaa;

  • Mr Sabodo amekuwa mfanyabiashara kwa muda mrefu na amejijenga vyema katika biashara zake katika mikoa mbalimbali ya nchi hususani Lindi na Daresalaam; kama Dodoma pekee atawekeza tilioni kumi huku kwingine anaweza akawa amewekeza sh ngapi?
  • Kiasi cha tilioni kumi pekee kilichotajwa na huyu mtanzania mwenzetu ambacho kimsingi kinazidi budget ya serikali ya Tanzania kwa miaka minne iliyopita na kinazidi budget ya mwisho ya serikali ya Tanzania chini ya rais Mkapa karibu mara tatu kinaleta picha gani?
  • Hivi kama budget ya nchi yetu kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ikiwa ni pamoja na kukopa imefika tilioni 29 inashindikanaje watu aina ya Sabodo kuizidi serikali pesa? hapa tuassume Dar es salaam na sehemu nyingine kwa ujumla amewekeza tilioni kumi na ushee.......
Binafsi namtakia utekelezaji mwema wa ahadi yake katika kuisaidia serikali kufikisha huduma kwa wananchi wa Dodoma na Tanzania kwa ujumla japo naamini umetuachia funzo sisi watanzania wenzako.
 
Sarcasm!
 
Mmnaompinga sabodo, mmgekuwa mmesoma alichokisema labda mmeelewa...,...hakusema hela anayo, alichokisema atatumianlines zake credit kupata hiyo hela
 
Hatupingi Mkuu.ili upate mkopo lazima uwe na collateral security.pesa hiyo ni ndefu Sana'a.bank gani itampa mkopo bila security.mtanzania aliyekopa pesa ndefu ni mo katika bank za south Africa.
 
Mimi bado nipo nashangaaa. Na nikilitegemea Leo ningesikia kwenye TV zetu za bongo hii taatifa lakini sijaona.. This is a lot of money aiseee!!!!
 
Yeye azilete tu hatutamuuliza kazipata wapi, tunachotaka ni kuwa amewekeza nyumban tanzania na tena makao makuu ya nchi ambayo serikal inahamiapo
 
Trion 10 siyo nyingi.
Tatizo lenu mnafikiri kila biashara lazima utoe hela yako mfukoni.
Hua waanaandika proposal na buzinez plan unaenda kukopa.
Ukitegemea kuanzisha biashara kwa pesa zako mfukoni utasota sana.
 
Hatupingi Mkuu.ili upate mkopo lazima uwe na collateral security.pesa hiyo ni ndefu Sana'a.bank gani itampa mkopo bila security.mtanzania aliyekopa pesa ndefu ni mo katika bank za south Africa.
bado unamawazo ya collateral tu, jaribu kuficha mawazo ya kimasikini, estate developers hawakopi finca au pride.
 
Kumbe ni tajiri mpaka anasahau vihela vidogo anavyopaswa kuilipa halmashauri,nadhani uzee unamjia vibaya hako ka ponjolo.
 
Back
Top Bottom