Tuunganishe dots utekwaji wa Mo Dewji

Hii serikali ina mikono ya MUDA!!!!
 

Kwenye hii info ya Ngurumo huyo senior minister atakuwa January Makamba maana toka MO atekwe na hadi kupatikana ndio alikuwa mtoa taarifa ya kinachojiri
 
Linapokuja interest ya nchi lolote lazima lifanyike au kama hujui subiri tu rip Jamal Khashogi.

Jamal Kashoggi haikuwa kwa maslahi ya nchi bali tamaa ya mmoja princes kujihakikishia kwamba yeye ndio mrithi pekee, ndio maana aliwaweka ndani hadi kaka zake na ndugu wengine ili kuwadhibiti. Kashoggi alianza kuwa critic wa ufalme wa Saudia pindi prince mohammed bin Salman alipokuwa crowned.
 
Hoja ya hovyo tu, magunia kwani shs ngapi?
Mkuu hivyo vitu tunavyovidharau ndivyo vinawafanya watu kama MO waendelee kuwa matajiri huku wengi wetu tusijue kama ni fursa. Kuwa na taarifa na maarifa sahihi ni muhimu.
MO alishawahi kukili(in honest way) kuwa kupitia kwenye mkonge anachapa hela kopi,faida yake ni kufuru.
 

Mkuu FisadiKuu,

Kuna mambo mengi katika hayo naona unayapindisha labda kwa makusudi au labda una malengo yako.

1. MO ni kweli anamiliki mashamba ya mkonge ya kiasi ulichotaja lakini si kweli kwamba anamiliki kihalali.

Mengi ya mashamba hayo ameyapata kwa njia zisizo rasmi na kisha kuyachukulia mikopo kwenye benki za nje kama dhamana

Nafikiri unafahamu kwamba kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na ndo maana akaambiwa arudishe sehemu ya mashamba hayo kwa wananchi ambao wengi hawana ardhi ya kulimia au kufanya shughuli zao.

Namba 2 - 4 nazo ni nadharia tu na sidhani kama walokwambia hayo wamefanya hivyo kwa malengo gani.

Tukija kwenye magunia na suala zima la importation naona bado unaonyesha tu kwamba kuna chuki za makusudi dhidi ya MO kutoka kwa serikali.

Mimi kwa uelewa wangu na kwa kufahamu uwezo wa MO naona suala liko hivi, na hili ni kutokana na alichokionyesha January Makamba kwenye masaa 48 yalopita:

1. Kuna mafuta mengi sana yaliingizwa nchini kati ya mwishoni mwa 2016 na mwanzoni mwa 2018 na kusemwa kuwa ni mafuta ghafi na yanakwenda kiwandani.

Badala yake mafuta hayo ambayo yalikuw ana utata na ubora wake yakaishia kwenye soko la rejareja na yakawa yanauzwa.

Mtindo huu upo siku zote na ulishamiri kwa miongo miwili na zaidi. rejea mada ya mada humu JF inayozungumzia sera za serikali ya awamu ya 3.

2. Pia kuna sukari nyingi sana ambayo iliingizwa nchini kati ya 2015-2017 ambayo ilisemwa kwamba ni sukari ghafi na ilikuwa kwa ajili ya kutengeneza vinywaji viwandani.

Lakini ukweli sukari hiyo ilikuwa ni sukari ya kawaida lakini ilikuwa imeisha muda wake kwa ajili ya soko la ndani la rejareja. Hali hiyo ilipekeka sukari za Mtibwa Sugar na Kagera Sugar kuozea kweye mabohari yao.

3. MO ni mfanyabiashara mkubwa sana na mwenye fedha lukuki kasi cha kuweza kuwa na akaunti nje ya nchi na kwingine.

Mimi kama nikiwa ni rafiki yake lakini nafanya kazi serikalini sitapenda nijulikane wapi naweka fedha zangu za kifisadi.

Hivyo kuna uwezekano mkubwa kabisa MO akawa alikuwa anatumiwa na baadhi ya wakubwa serikalini kuficha fedha zao ama nje ya nchi au ndani ya nchi.

Hivi sasa wakubwa hawa ambao ndo walikuwa wakimtumia MO kuna uwezekano mkubwa kwamba wanahaha usiku na mchana kutafuta nini kinafuatia.

Mwisho, MO inasemekana alitupwa na watekaji wake kwenye viwanja vya Gymkhana na akapewa simu na wasamaria wema ambapo aliwasiliana na familia yake.

Kitendo cha polisi kumhoji January Makamba ni katika kutaka kufahamu ni kitu gani waliongea kati yake na MO kabla ya polisi hapo ndipo penye tatizo.

Wewe jiulize iweje awe January Makamba pekee ambae ana uwezo wa kutambua kwamba MO yupo nyumbani amepatikana?

Wataka kuniambia kwamba familia ya MO ilimjulisha MO kwanza badala ya kuwapigia simu polisi na kuwajulisha juu ya utokeaji wa MO.

Mimi hapo naamini kwamba huenda MO alitekwa na kisha akaachiwa ajitokeze.

January Makamba akiwa "clear" na hilo (jambo ambalo nalitilia shaka) basi atakuwa yuko sawa.

Familia yake hiyo ndo walokuwa wa kwanza kumwona MO na kumchukua kisha kumpeleka nyumbani na kisha January Makamba akawa wa kwanza kumwona na kumjulia hali.

Kisha January Makamba akaja kwenye social media na kusema aloyasema kwamba amezungumza na MO kwa dakika 20 na yupo mzima wa afya.
 
Wakishakaa kwenye vitu vya kuzunguka wanajiona washayamaliza maisha..

Wanashindwa kujua hivi vitu vidogo vidogo ndio matajiri hupiga pesa huko..
 
Mkuu Richard;

Familia ya Mo na Makamba ni marafiki wa kipindi kirefu. January kupata taarifa mapema ni kutokana na ukaribu wa familia zao.

Suala la sukari, mafuta ya kula kama ni kweli ni dhahiri Mo alifanya makosa, alivunja sheria hivyo kusingekuwa na nguvu ya kumteka bali wangeenda front..

Suala la ardhi either amelipata kwa kuiba/ubabe/ufisadi ni matokeo ya makosa ya serikali ya CCM huko nyuma hivyo kusingehitaji ubabe aliofanyiwa ili tu arudishe ardhi hiyo.

Suala la magunia ni la kweli kabisa, ingawa pia nakubaliana na mengine uliyoyasema inawezekana pia hayo yametumiwa pia ili kunegotiate the deal..
 

Uko sawa kabisa mkuu.

Ni vizuri tukaweka rekodi sawa maana hata zile radio/video cassette zikiingia mushkeli basi unakaa kitako na unakuwa wazinyoosha kwa uzuuri hata kwa pasi ili tu upate mkanda kamili usio na kasoro.

Amani ikuangaze daima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…