Tuunganishe dots utekwaji wa Mo Dewji

Tuunganishe dots utekwaji wa Mo Dewji

FisadiKuu

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2015
Posts
8,337
Reaction score
13,656
Wasalaam wanabodi.. Hivi ni nyepesi nyepesi tu nizijuazo. Twende tusafiri pamoja..

1. Mo ana miliki hekari zaidi ya 90,000 za mkonge ambazo pia anatumia mkonge kutengeneza magunia.

2. Mo mwaka jana amekopesha serikali/vyama vya msingi magunia yenye thamani zaidi ya billion 10.. Mpaka anatekwa alikuwa hajalipwa na alisumbuana sana na serikali..

Screenshot_2018-10-21-19-23-10-1.png

3. Mo mwaka huu aligoma kukopesha serikali magunia yake, serikali ikategemea magunia kutoka India. Wakala aliyeleta magunia kutoka India trip 1 tu akachemsha kodi za bandari, trip ya 2 mzigo ukamshinda ukabaki bandarini, Mo akaenda kuununua wote akaenda kuuweka store.

4. Serikali ikakosa magunia, hasahasa kwenye msimu huu muhimu wa korosho ambao mwaka jana kwa kodi moja tu ya (export levy) serikali ilidhurumu/iliwarusha wakulima zaidi ya Billion 200.

Sasa tuje kwenye nadharia:

5. Serikali baada ya kukosa magunia, ikabidi ianze kurumbana na Mo awapatie magunia. Mo labda aligoma akishinikiza alipwe pesa zake.. Serikali nayo ikatunisha misuli..
Screenshot_2018-10-21-19-22-40-1.png

6. Baada ya kutokukubaliana, Mo akatekwa, ukizingatia msimu wa korosho tayari na magunia ya kutosha hawana. Mind you; Korosho kwa sasa ndio inaingiza pesa nyingi za kigeni kama sio nyuma ya utalii basi ni zaidi ya utalii.. kukosekana kwa magunia kutaadhiri ununuzi na usafirishaji wa korosho zilizununuliwa.

7. Naibu waziri wa ardhi akaenda Korogwe kwenye mashamba ya mkonge ya Mo akitishia kuyagawa kwa wananchi. *mind you, mashamba hayo ndio huzalisha hayo magunia*

8. From my source, juzi maghala yaliyoifadhi magunia yalifunguliwa na magunia yakapakiwa. Mmoja wa dereva aliyepakia magunia kuyapeleka Masasi ni rafiki yangu..

9. Deal done; Mo akakubali kushindwa hivyo akaachiwa aende zake.

Karibuni tujadili..

Cc: Pascal Mayalla Salary Slip @brittanica
 
Attachments

  • Screenshot_2018-10-21-19-23-10-1.png
    Screenshot_2018-10-21-19-23-10-1.png
    16.9 KB · Views: 129
Nasikia kumbe kuna hela baadhi ya wafanya biashara wakubwa waliombwa kila mmoja kutoa wenzake wakatoa yeye nasikia alisema hawezi kutoa hiyo hela maana analipa kodi nyimgi na kubwa hivyo akafanyiwa umafia huo.hii nimeipata sehem nyeti kwa mtu ambae kwa kweli alivyokuwa anaongea huenda kama kuna kaukweli maana hapo alipo ni sehem nyeti
 
Kuendesha nch sio mchezo,ikulu hakukimbiliwi,kwenye hotuba best ya nyerer ile ya 1995 pale Kilimanjaro hoteli mwalimu alisema wakati anapita barabarani wakati yeye rais akiona ombaomba anaona ule ni mzigo wake,sasa NGOSHA ZE DON kavamamia ikulu pupa pupa akajua kina jahcarhire walikuwa wanafaidi,kuingia hola hakuna pesa,hela ya mshahara hana,akaanza kupunguza wafanyakazi nako hola,fukuza wateule wa kikwete labda aliona wana connection za wizi nako hola hela hana,punguza semina warsha safari makongamano sherehe za kitaifa labda hela itaonekana nako hola,akaona ngoja azuie mafao ya kujitoa nako hola,sasa ameanza kuvamia wafanyabiashara huku ndio atadondokea PUA kabisa maana ukicheza na mfanyabishara hakawii ku_shift the CAPITAL tu.
 
Naamini atalipwa pesa yake.

Ni kosa kubwa sana kuua mtaji wa mtu. Awamu hii serikali imeua mitaji ya wengi. Swali la msingi ni mtakusanya wapi kodi?

Hata kama mtu ni mdaiwa sugu wekeni mazingira ya kukusanya na kurejesha deni lote pasipokuua biashara ya mtu ili kulinda kodi, kipato cha wananchi na ajira kwa watanzania. Tusiangalie leo tu, tuangalie kesho....kumbukeni sisi ni ulimwengu wa tatu sio Marekani hapa.

Ni mbaya zaidi kunyang'anya kwa wasiokuwa na hatia...,maana hamtoishia hapo mtamaliza wote then mtageukana nyie kwa nyie
 
Kuendesha nch sio mchezo,ikulu hakukimbiliwi,kwenye hotuba best ya nyerer ile ya 1995 pale Kilimanjaro hoteli mwalimu alisema wakati anapita barabarani wakati yeye rais akiona ombaomba anaona ule ni mzigo wake,sasa NGOSHA ZE DON kavamamia ikulu pupa pupa akajua kina jahcarhire walikuwa wanafaidi,kuingia hola hakuna pesa,hela ya mshahara hana,akaanza kupunguza wafanyakazi nako hola,fukuza wateule wa kikwete labda aliona wana connection za wizi nako hola hela hana,punguza semina warsha safari makongamano sherehe za kitaifa labda hela itaonekana nako hola,akaona ngoja azuie mafao ya kujitoa nako hola,sasa ameanza kuvamia wafanyabiashara huku ndio atadondokea PUA kabisa maana ukicheza na mfanyabishara hakawii ku_shift the CAPITAL tu.
Kaleta taharuki kwa wazalishaji mali
Anajiua bila kujua
Alidhani viwanda ni maneno, serikali yake itakufa kibudu
 
Back
Top Bottom