JamiiForums
JF Official Account
- Nov 9, 2006
- 6,202
- 5,012
TUHUMA ZA RUSHWA YA NGONO: TAARIFA ZAIDI ZINAHITAJIKA
Habari,
Kumekuwa na tuhuma kadhaa ambazo zimekuwa zikisambaa kwenye Mtandao wa JamiiForums zikielekezwa kwa madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya
Wengi wa walioleta tuhuma hizo hawakuleta taarifa za kina ili kusaidia kuwatia hatiani wanaotuhumiwa
Kupitia Miscellaneous Amendment Act namba 3 ya mwaka 2016, Sheria ya Uhujumu Uchumi ilifanyiwa mabadiliko na kutambua makosa yote yaliyopo ndani ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (isipokuwa kosa chini ya Kifungu cha 15) ni makosa ya Uhujumu Uchumi
Hivyo, Rushwa ya Ngono kwa sasa ni Kosa la Uhujumu Uchumi na adhabu yake sio faini tena ila ni kifungo cha mpaka miaka 20 jela
Vyombo vya Dola vimeziona tuhuma hizo (katika JF) na Mamlaka zinahitaji wenye taarifa za kina zinazoweza kuwasaidia wachunguzi wazilete taarifa hizo zikiwa detailed (hata kama kuna viambatanisho zaidi) ili wahusika/watuhumiwa wachukuliwe hatua stahiki
Unaweza kuweka bayana kwenye mjadala huu au kwa kututumia PM/DM au barua pepe sensitive@jamiiforums.com au uwasiliane na Waziri wa Afya (Waziri Ummy Mwalimu) kwa kumtumia DM kupitia mitandao ya Twitter au Instagram.
Ummy Mwalimu, MP (@umwalimu) | Twitter
Hata walio nje ya Mkoa wa Mbeya, tunapokea taarifa zao pia za Unyanyasaji na Rushwa ya Ngono katika Sekta ya Afya.
Asanteni sana
======
UPDATES
=======
JamiiForums imeyawasilisha kwa Mamlaka husika Malalamiko yaliyotolewa na Mdau wa JamiiForums kupitia hii thread hapa chini, Na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) wameshaanza kuyafanyia kazi.
Soma hapa: Tuhuma za rushwa ya ngono kwa madaktari bingwa Hospital ya Rufaa ya kanda Mbeya
Hatua zimeanza kuchukuliwa

Ummy Mwalimu (@ummymwalimu) • Instagram photos and videos
753K Followers, 367 Following, 1,845 Posts - See Instagram photos and videos from Ummy Mwalimu (@ummymwalimu)
instagram.com