Tutumie rasilimali ya gesi na petroli kuinua kilimo

Lasway.Jr

JF-Expert Member
Jul 25, 2015
230
405
TUTUMIE RASILIMALI YA GESI NA PETROLI KUINUA KILIMO

Kwanza tumshukuru mungu kwa kuwa tumezaliwa katika nchi nzuri ya Tanzania yenye amani na utulivu, nchi ambayo watu wake ni wakarimu, wachapakazi na wazalendo. Nchi yetu ina rasilimali nyingi sana kama madini ya aina mbalimbali katika maeneo kama Mererani, Mwadui, Geita, Chunya n.k, pia tuna mbuga za wanyama kama Serengeti, Manyara, Mikumi, hifadhi ya Ngorongoro n.k pia tuna na mlima mrefu wenye uzuri wa kuvutia watalii ulipo kule nyumbani Kilimanjaro
Kwa ujumla Tanzania ina eneo la hekta milioni 94.5 kati ya hizo hekta milioni 6.15 ni maeneo ya bahari na maziwa, pia hekta milioni 44 ndizo zinazofaa kwa kilimo sawa na asilimia 46.6% ya ardhi yote ya Tanzania ndio rasilimali mama tuliyo nayo sisi watanzania ambapo asilimia 80% ya watu ni wakulima na wanategemea kilimo kama shughuli ya kujipatia kipato na chakula.
Leo nitaeleza kwanini kilimo na ni kwa namna gani sisi watanzania tunatakiwa kufungua macho yetu na kuona uwepo wa gesi asilia kama njia ya kuimarisha kilimo chetu kwani jamii nyingi za kitanzania zinategemea sana kilimo pia hatuwezi kuwa na viwanda venye uzalishaji mzuri kama kilimo kinasuasua kwa kuwa mali ghafi za viwanda vyetu hutegemea sana kilimo kwa asilimia zaidi ya 70%
Kwa kuanza na kilimo chenyewe tukumbuke kuwa miaka ya nyuma nishati ya umeme ambayo tuliyokuwa tunaitumia ilitokana na nguvu ya maji yaani kwa kizungu Hydroelectric Power ambapo mitambo ya kufua umeme katika mabwawa yetu kama Nyumba Mungu, Mtera, Kihansi, Kidatu na kwingineko ilitegemea kwa asilimia 100% uwepo wa maji ya kutosha ndio maana kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi yalisababisha maji kupungua katika mabwawa hayo yaliathiri sana uzalishaji wa nishati hiyo na watanzania tukateseka sana.

Lakini ni bahati iliyoje wakati huu kulingana na maneno ya Waziri wa nishati na madini Mh Prof Sospeter Mhungo alisema kwa sasa karibia zaidi ya nusu ya umeme wa tanzania unatokana na Gesi, na naamini kwa kasi ya maendeleo tuliyo nayo kwa sasa baadaye miaka inayokuja umeme utakuwa unazalishwa kwa gesi na kutosheleza mahitaji ya nchi na tutaacha kutumia umeme unaotokana na nguvu ya maji sasa fursa ninayoiona hapa mpaka kunisukuma kuandika hii makala ni kwamba MAJI YOTE SASA YANARUDI KWENYE KILIMO, Takwimu zinasema kuwa asilimia 24.1% ya ardhi Inayofaa kwa kilimo ndio inayolimwa kwa sasa kwa hiyo bado tunahitaji kuwekeza zaidi kwenye kilimo kwa sababu ardhi nzuri na yenye rutuba bado ipo na pia rasilimali maji bado zipo za kutosha. (Based on data presented on the national government websitehttp://www.tanzania.go.tz/landsf.html.) kwa hiyo nategemea kwa uwepo na maji ya kutosha sasa wizara mbili ambazo zilikuwa zinakinzana kutokana na matumizi ya maji yaani wizara ya nishati na madini na wizara ya maji na umwagiliaji hasa kwenye utoaji wa vibali vya matumizi ya maji yaani Water permit ukinzani huo hautakuwepo tena na watanzania tulione hili na tuanze kuchukua hatua kuwekeza kwenye kilimo tuweze kuongeza hiyo asilimia 24.1% angalau tufikie kulima asilimia 40% ya ardhi yetu na tukifikia hapo ndipo kauli ya kusema kilimo ndio uti wa mgongo ambacho kinachangia 33% ya Gross domestic product(GNP) (2011-2015 kulingana na takwimu za benki ya dunia) wa taifa hili utatimia.
Zipo faida nyingi za kuimarisha kilimo kwanza kabisa upatikanaji wa chakula cha kutosha nchini kwa kuwa tunajua endapo watu watapata chakula cha kutosha na bora basi watakuwa na nguvu ya kufanya shughuli nyingine za kimaendeleo kwa ufanisi mkubwa kinyume na watu wakiwa na njaa itakuwa ngumu sana kwao kufanya shughuli nyingine za uzalishaji mali ili nchi yetu iweze kuendelea
Hapa ningependa kuwaongelea wafanyakazi wa serikali wanaokaa maofisini na wakati wote hulalamika kulipwa mishahara midogo tatizo hili litaisha tuu pale ambapo kilimo kitaimarishwa na upatikanaji wa chakula kuwa mzuri na hata bei ya vyakula hivi itakuwa nafuu kwa hiyo hata mfanyakazi wa hali ya chini ataweza kumudu kujitosheleza kwa chakula na lawana kwa serikali zitapungua
Kama wananchi hasa vijana kama tutaifanyia kazi fursa hii tutaipunguzia serikali mzigo wa kutenga bajeti ya chakula cha msaada kila mwaka kusaidia jamii zetu na hivyo basi pesa hizo zitaenda kufanya shughuli nyingine za kimaendeleo .....youth wake up
Kwa mtazamo chanya wa jicho lenye kuona mbali kwa Tanzania yetu tunaelekea kwenye uwezo wa nchi kuweka mkazo kwenye uzalishaji wa bidhaa za ndani yaani viwanda vya kutengeneza bidhaa mbali mbali lakini tunachotakiwa kuwaza na kufanyia kazi ni kwa namna gani viwanda hivi vitaweza kupata mali ghafi? jibu ni rahisi sana kwani watanzania wengi ni wakulima na wafugaji kwa hiyo mali ghafi za kulisha viwanda hivi itategemea kwa kiasi kikubwa sana kilimo kwa hiyo ni fursa kwa vijana na wawekezaji kujibidiisha na kilimo tena cha kisasa ili viwanda ambavyo tuna ndoto ya kuwa navyo visije vikafa kama ilivyotokea kwa viwanda vya pamba, katani,kahawa,ngozi n.k
Rasilima ya Gesi asilia itavisaidia viwanda vyetu kujiendesha kwani umeme wa uhakika umepatikana.Kwa hiyo uchakataji na usindikaji wa bidhaa za kilimo na nyinginezo utakuwa wa kiwango cha juu na hapo ndipo ninapoiona Tanzania ya ndoto zangu
Katika kilimo pia jambo la kuangalia ni namna ya kuyatumia haya maji tuliyapata baada neema ya gesi asilia katika nchi yetu, tunatakiwa tuwe na njia bora za matumizi ya maji ili yaweze kutosheleza mahitaji yetu ya sasa na ya vizazi vijavyo nasema hivi nikiwa kama mtaalamu wa rasilimali maji na uwagiliaji (irrigation and water resources Engineer(T).) Nawashauri wakulima na wawekezaji wote kutumia wataalamu hasa wazawa katika shughuli za uzalishaji ili kuendena na ukuaji wa teknolojia ya kilimo ambayo inahimiza sana kuhusu namna ya kutumia maji kidogo na kuongeza uzalishaji.
Lasway Octavian J
Bsc Irrigation and Water Resources Engineering
Sokoine University of Agriculture
 
Back
Top Bottom