Tutumie nafasi na akili zetu kuiondoa ccm madarakani. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tutumie nafasi na akili zetu kuiondoa ccm madarakani.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Concrete, Sep 22, 2012.

 1. C

  Concrete JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Habari za punde kutoka chanzo cha ndani kabisa cha serikali na vikao vya juu vya CCM kinaeleza mipango mikubwa kabambe ya hila za kisiasa kuhakikisha kwa hali na mali CCM inabaki madarakani 2015.

  Mipango hiyo haijali ni gharama kiasi gani watatumia iwe ni pesa au maisha ya watanzania ilimradi tu wabaki madarakani.

  Mikakati hii tayari hatua ya mwanzo ilishaanza kabla ya sasa ila kinachotakiwa kufanywa ni kubadili baadhi ya mbinu na kuongeza nguvu zaidi kwenye eneo la mafanikio.

  Baadhi ya mikakati hiyo ni:

  1/Kuhodhi mihimili yote ya dola(Mahakama, Bunge na Serikali)

  2/Kutumia vyombo vyote vya dola(Polisi,JWTZ, TISS)

  3/Kutumia taasisi zote za umma(Vyombo vyote vya habari vya umma, Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nk.)

  4/Kupandikiza mamluki ndani ya wapinzani wa kweli na taasisi za wanaharakati wa kweli.

  5/Kutumia baadhi ya taasisi na viongozi wa kidini.

  6/Kutumia vitisho dhidi ya mtu binafsi au taasisi zote ambazo zitaamua kusimamia haki (eg.kufilisiwa, kunyang'anywa uraia, kufukuzwa kazi, kushtakiwa, kuzushiwa, kustaafishwa, kufungiwa)

  MY TAKE
  *MTAJI WAO(Pesa, Madaraka, Nguvu)
  *UDHAIFU WAO(Mgawanyiko, Woga, akili ndogo, uchache wao, kukosekana usiri)
  *NGUVU YETU(Wingi wetu, umoja wetu, akili kubwa, Mwenyezi Mungu)

  Ningependa kutoa wito kwa wapenda haki wote wa watanzania ambao tungependa kuona ukombozi wa nchi yetu anawadia tuungane kwa hali na mali kutumia NAFASI zetu na AKILI zetu kupambana na wadhalimu hawa kwa kufanya yafuatayo:
  1/Kumwaga hadharani kila mpango wa siri wanaoupanga(Tuwaumbue kabla hawajatekeleza)

  2/Tupambane nao kwa kila hoja wanayokuja nao hadharani(Tuhoji, Tupinge, Tukosoe)

  3/Tuwaelimishe na kuwahamasisha watanzania wote ambao bado wako usingizini.
   
Loading...