IamMrLiverpool
JF-Expert Member
- Apr 27, 2014
- 4,812
- 7,277
Naomba kujuzwa kuna utofauti kati ya TA (Tutorial Assistant) na lecturer mwenye idea please
naomba kujuzwa kuna utofauti kati ya TA(tutorial assistant) na lecturer mwenye idea please
tutorial assistant ni mkufunzi tu wa ngazi ya chini ambaye kamaliza shahada yake ya kwanza na huwa anafanya tu majukumu ya instructions kwa wanafunzi kwa maelekezo ya mhadhiri wa somo husika. lecturer ni mhadhiri halisi wa somo husika na huyu huwa ana elimu ya shahada ya uzamivu ( phd ) na yeye ndiyo mpango mzima kwa ufundishaji na kwa kukuongezea tu ulisahau pia kuuliza na huyu assistant lecturer kwani ngazi zao huko vyuoni huanzia na tutorial assistant kisha assistant lecturer na lecturer. huyo assistant lecturer huwa anafanya kazi za kufundisha pia na mara nyingi hufundisha wanafunzi wa kuanzia mwaka wa pili na watu humu vyuoni na hawa elimu zao huwa ni shahada ya pili au shahada ya uzamivu. nadhani nitakuwa nimekufumbua japo kidogo na ngoja niwaachie na wengine. nimependa sana spirit yako ya kuwa inquisitive na inaonekana utakuja kuwa academician mzuri sana huko baadae.
Mkuu TA ni ngazi ya kwanza kwenye kuajiriwa kama Mhadhiri. Huyu huwa na Shahada ya kwanza tu ya tasnia yake. Akipandishwa anakuwa Assistant Lecturer akiwa sasa na Shahada ya Uzamili/Umahiri. Akipata Shahada ya Uzamivu anakuwa Lecturer.
Kimsingi,Lecturer ni ngazi ya juu kuliko TA. Na hata elimu zao ni tofauti. Hivyo,mishahara ni tofauti pia.
Lecturer ni Dereva na TA ni Utingo
Unaweza kuwa senior lecturer bila kuwa bila kuwa na PhD, but una masters na mzoefu kazini
haya wasomi
hiyo ilikuwa zamani, sasa hivi kama huna PhD huwezi kuwa lecturer
Mbona ifm vijana wa bachelor wanafundishwa na walimu wenye bachelor na hao walimu wana bachelor wanajiita lecturers. Soma kitabu chao cha mwongozo na uone. Ifm bachelor hufundishwa na bachelor wenzao.
☺☺☺☺☺☺☺☺☺☺☺☺☺☺☺☺☺
Mkuu toka umejiunga hii ndio post yako ya kwanza, unasoma ifm nini?
soma prospectus ya ifm uone alafu uulize mwl wa somo na uangalie kwenye prospectus utaona wenye bachelors ndio waalimu wa wanafunzi wa bachelor wanajiita lecturers.
Ifm ukiwa na masters wewe ni full lecturer. ni aibu na hatari kwa mstakabali wa elimu Tanzania.