Tuthamini amani tuliyo nayo

Tuthamini amani tuliyo nayo

Abuu Dharr

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2017
Posts
2,910
Reaction score
3,024
Assalaam Alaykum,

Nataraji ndugu zangu, mpo salama na wenye furaha pamoja na familia zenu

Naomba niseme nililolikusudia
Yamebaki masiku machache,masiku ambauo,huenda yakatupa dira ya miaka 5 mbele. Dira hiyo huenda ikawa ni njema na yenye furaha au kinyume chake Muhimu kwasasa ni kila mtu kulingania amani ya Nche yetu. Amani inathamani katika jamii kuliko haki ya mtu mmoja mmoja.

Labda huenda ukastaajabu Kwann amani katika jamii ni bora zaidi kuliko haki ya mtu mmoja mmoja?

Jawabu fupi

Kuna wakati ni lazima mtu ajitoe mhanga kwa kupata maumivu makali,kwasababu ya Watu waliomzunguuka

Amani na Haki
Sehemu kubwa vinakaa pamoja,lkn kuna wakati huenda vikaachana kwasababu....

Tulinde amani zaidi,kwasababu ni sehemu ya kujipanga tena vzr katika kutetea haki yako

Tujifunze kuitafuta haki ndani ya amani
Na wala tusijifunze amani ndani ya haki

Vizazi vyetu
Vinahitaji amani,katika kuyaendea mambo mbalimbali

Basi,tusiwe wa mwanzo kuivunja amani kwa makelele ya Wachache na maslahi yao

Amani ni muhimu katika ustawi wa Jamii
Nawatakia siku njema
 
Mkiona watu wameanza kujitambua basi kisingizio kinakuja tutunze amani yetu

Mngekuwa mnaongea hivi hata wakati wa watu wasiojulikana wakiwa wanafanya jambo lao
 
Back
Top Bottom