Tutete kidogo: Mamlaka ya CAG | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tutete kidogo: Mamlaka ya CAG

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GINHU, May 3, 2012.

 1. G

  GINHU Member

  #1
  May 3, 2012
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu wa JF salamu
  Hoja yangu kwa leo ni kuteta kuhusu mamlaka aliyopewa CAG.

  Akihutubia kilele cha cha maadhimisho ya sikukuu ya Wafanyakazi duniani MEI MOSI, katika uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Raisi Kikwete alielezea kwa kirefu majukumu na mamlaka ya CAG currently Bw. Uttoh (a.k.a OTTU). kwa upande wa Mamlaka, Raisi alisema, ili CAG awe na uhuru kamili, ilitungwa sheria ya kutoingiliwa ktk utendaji wake, si Raisi ama chombo kingine chochote hakiwezi kuingilia mamlaka yake. Raisi akishamteua CAG hana mamlaka ya kumwondoa na km kuna dosari yoyote katika ripoti zake, halimashauri/idara husika wanatakiwa wapeleke malalamiko yao katika mahakama ya Rufaa na si vinginevyo.

  Hoja yangu hapa ndugu wanaJF ni:
  1. kama huyu mteule wa Raisi hawezi kuhojiwa na mamlaka yoyote, sasa anawajibika kwa nani? na ni nani wa kumwajibisha? nauliza hivyo maana isije ikatokea mkubwa huyu akawa na bifu na ofisi fulani akaamua kutoa ripoti mbaya ili amkomoe mbaya wake.
  2. Je ripoti za huyu bw mkubwa zinakaguliwa na nani?

  Ndugu wanaJF naomba kutoa hoja
   
 2. T

  The Infamous JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2012
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  mahakama
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  May 3, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu soma Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 143 na 144.

  Mahakama ina nguvu kikatiba kuchunguza kama CAG anatekeleza madaraka yake kwa mujibu wa katiba (ibara ya 143 (6)).

  Kuhusu kumuondoa kazini pia kuna mchakato wa kikatiba ambapo kama Rais anataka kumfuta kazi itabidi ateue tume ya kumchunguza CAG.
   
 4. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Na katika nchi yetu siyo CAG peke yake bali pia majaji wa mahakama kuu na rufaa na gavana wa benki kuu.

  Hizi ni nafasi nyeti sana ambazo mtu akiwa katika nafasi hizo hatakiwi kuzifanya huku akiwa na wasiwasi wa kuondolewa!
   
 5. G

  GINHU Member

  #5
  May 3, 2012
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu soma Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 143 na 144.

  Mahakama ina nguvu kikatiba kuchunguza kama CAG anatekeleza madaraka yake kwa mujibu wa katiba (ibara ya 143 (6)).

  Kuhusu kumuondoa kazini pia kuna mchakato wa kikatiba ambapo kama Rais anataka kumfuta kazi itabidi ateue tume ya kumchunguza CAG.

  mkuu nashukuru sana for your directives; Nimesoma hizo ibara lakini kuna mapungufu makubwa ya kikatiba kuhusu kinga hizo alizopewa. mf kibara 144 km kuondolewa kwa CAG itabidi raisi aunde tume ya watu wasiopungua 2, ambapo mwenyekiti na nusu ya wajumbe sharti wawe ni majaji tena wa mahakama kuu ama za rufaa ktk nchi za jumuiya ya madola. Hapa ndo penye utata ktk kuwajibishwa kwa bw. mkubwa huyu. pengine kuna haja ya kulijadili upya jambo hili ktk katiba ijayo.


  Naomba tuendelee kuteta ktk hili.

  Asanteni
   
Loading...