Tutende wema, ipo siku ule wema utakulipa

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
37,104
Reaction score
55,514
Kuna rafiki yangu mmoja tulikutana naye shuleni (sekondari) miaka 35 iliyopita; Kiuchumi, wao walikuwa wako vizuri kiasi kwa kipindi kile.

Katika shule tuliosoma, shule yetu ilikuwa na changamoto ya madawati; wapo waliokuwa wakikalia matofari kutokana na upungufu wa madawati na wachache wakikalia madawati waliotengenezewa na familia zao.

Huyu rafiki yangu, aliniruhusu kukalia dawati lake kwa kuninusuru mimi kukalia matofari mpaka nahitimu shule (o-level))

Baada ya pale tulifaulu, na kila mmoja akapangiwa shule tofauti za ufundi kwa ‘A-level’; baada ya kupangiwa shule tofauti, tukawa tumepotezana na hakukuwa na mawasiliano tena.

Tumekuja kuwasiliana kipindi hiki (wiki 2 zilizopita) baada ya kunitafuta hapa na pale.

Siku hiyo nilipokea ujumbe kwenye akaunti yangu moja ya mtandao wa kijamii kutoka kwa huyo rafiki yangu, akijitambulisha na kutaka kujua kama mimi ndiye eqn x; nami nikamjibu hujakosea akaunti bali ndio mimi, wote tukafurahi sana kwa sababu tulipotezana miaka mingi na tukabadilishana namba.

Mnavyojua tena, maisha upanda na pia ushuka; alinijulisha wazee wake walishatangulia mbele za haki, nyumba yao iliungua na moto, biashara za mzee zikafa, nayeye pia alikutana na mitihani ya kidunia iliyompelekea kupoteza kazi na kukimbiwa na mkewe pamoja na watoto; na kwa sasa maisha yake ata kula yake ni changamoto.

Ilinifanya nitafakari kidogo kwa kurudi nyuma miaka 35 iliyopita, nikajikuta sina la kuongea; nilichofanya ni kumuambia, ondoka kwenye huo mkoa A uliopo na nenda mkoa Z ukasimamie ‘banda langu la chipsi’ huku tukiangalie mengine; utakula bure, utalala bure, na utavaa bure; alishukuru sana.

Ndipo nilipojifunza, wema siku zote unalipa.

Tuwatendee wenzetu wema hatujui ya kesho; leo unaweza kuwa na nafasi kubwa nzuri, kesho ukawa ni omba omba, maisha yanabadilika.

dpo.jpg
 
Shida Kuna wakina punda huwa wanalipa mateke ndiyo maana watu wanasita kumpa mtu msaada
Ni kweli, wapo wanaolipa mateke ila kuna muda wakijitafakari wanajiona wamefanya makosa.
 
miaka 35 iliopita... Aya ngoja tuweke na sukari japo adhima yako ya kuelimisha ulimwengu imetimia
 
Kuna rafiki yangu mmoja tulikutana naye shuleni (sekondari) miaka 35 iliyopita; Kiuchumi, wao walikuwa wako vizuri kiasi kwa kipindi kile.

Katika shule tuliosoma, shule yetu ilikuwa na changamoto ya madawati; wapo waliokuwa wakikalia matofari kutokana na upungufu wa madawati na wachache wakikalia madawati waliotengenezewa na familia zao.

Huyu rafiki yangu, aliniruhusu kukalia dawati lake kwa kuninusuru mimi kukalia matofari mpaka nahitimu shule (o-level))

Baada ya pale tulifaulu, na kila mmoja akapangiwa shule tofauti za ufundi kwa ‘A-level’; baada ya kupangiwa shule tofauti, tukawa tumepotezana na hakukuwa na mawasiliano tena.

Tumekuja kuwasiliana kipindi hiki (wiki 2 zilizopita) baada ya kunitafuta hapa na pale.

Siku hiyo nilipokea ujumbe kwenye akaunti yangu moja ya mtandao wa kijamii kutoka kwa huyo rafiki yangu, akijitambulisha na kutaka kujua kama mimi ndiye eqn x; nami nikamjibu hujakosea akaunti bali ndio mimi, wote tukafurahi sana kwa sababu tulipotezana miaka mingi na tukabadilishana namba.

Mnavyojua tena, maisha upanda na pia ushuka; alinijulisha wazee wake walishatangulia mbele za haki, nyumba yao iliungua na moto, biashara za mzee zikafa, nayeye pia alikutana na mitihani ya kidunia iliyompelekea kupoteza kazi na kukimbiwa na mkewe pamoja na watoto; na kwa sasa maisha yake ata kula yake ni changamoto.

Ilinifanya nitafakari kidogo kwa kurudi nyuma miaka 35 iliyopita, nikajikuta sina la kuongea; nilichofanya ni kumuambia, ondoka kwenye huo mkoa A uliopo na nenda mkoa Z ukasimamie ‘banda langu la chipsi’ huku tukiangalie mengine; utakula bure, utalala bure, na utavaa bure; alishukuru sana.

Ndipo nilipojifunza, wema siku zote unalipa.

Tuwatendee wenzetu wema hatujui ya kesho; leo unaweza kuwa na nafasi kubwa nzuri, kesho ukawa ni omba omba, maisha yanabadilika.

View attachment 3432622
Wema wenye upendo kwa wengiine ni asset isioonekana na maisha yako yatakuwa tofauti na wengine
 
Naam ni kweli wema unalipa sana
 
Back
Top Bottom