Tutegemee mengi kutokea kwenye mikutano ya CHADEMA. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tutegemee mengi kutokea kwenye mikutano ya CHADEMA.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mangaline, Jul 15, 2012.

 1. Mangaline

  Mangaline JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 1,052
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kila mabadiliko lazima yawe na gharama zake. Upepo unaonesha wazi chadema inaendelea kukubalika siku hadi siku. wakati huohuo, chama chetu kikiendelea kupoteza mvuto mijini na vijijini, ndani na nje ya nchi.
  Ukweli ni kwamba, hakuna mtawala aliye tayari kugawa nchi kwa njia rahisi ya kuhesabu karatasi, hasa ukichukulia kuwa karatasi zenyewe zimepigwa na wanakijiji wa kutoka ndani kabisa, asiyejua hili wala lile, jema wala baya (samahani kwa wakao kwazwa).
  Pamoja na yote hayo, ipo dhana ya kuwa iwapo chama chenu kikichukua nchi, madhambi mengi yenye mfano wa dr. uli, yataibuliwa na kuna hatari ya kufikishwa the hague.
  Hivyo, ili kuendelea kulinda masilahi, pamoja na kulindana, ni lazima tutegemee fujo, mawe, ngumi, na hata mauaji kutokea katika mikutano ya chadema. na hii ndiyo gharama ya mabadiliko. lazima tukubali kuwa HAKUNA WOKOVU BILA MATESO.

  WAZO LANGU:-
  Tuweke kumbukumbu na orodha ya wote watakao poteza maisha katika kutetea na kupigania ukombozi wa kweli, ili historia iwaenzi kama mashujaa wa mabadiliko, kwa kuwa hayo hayaepukiki.
  Pili, tunawaomba mtuhakikishie kama madhambi tuliyotenda tukiwa madarakani (kwa miaka 50) hayatatupeleka the hague.
  "MUNGU IBARIKI TANGANYIKA, MUNGU IBARIKI ZANZIBARI, RIP TANZANIA"
   
Loading...