Tutegemee mambo mazuri zaidi kutoka kwa Mwigulu Nchemba

mbeyaman

Member
Sep 28, 2013
97
0
Hii kasi ya utendaji wa Naibu Waziri wa Fedha ni faraja kubwa kwa Watanzania ambao tumekuwa tukikamuliwa kodi lakini pesa zinapotea kimiujiza baada ya wajanja wachache kuzila.

Kwa kuona hayo Naibu waziri wa Fedha,ndugu Mwigulu Nchemba ameamua kupambana kuzuia pesa za walipa kodi zisipotee na kuishia kwenye matumbo ya wajanja wasiotakia mema Taifa letu.Hivi majuzi tu kupitia utendaji wa Naibu waziri wa Fedha pesa nyingi takribani bilioni 40 zimeokolewa zikisubiri kulipa mishahara hewa serikalini kwa mwezi huu wa nane.

Hakika Mwigulu Nchemba ameonesha utendaji na uzalendo wa nchi yake kwa hali ya juu.Watendaji wote wa serikali wazidi kumpa ushirikiano Mwigulu ili apambane na ufisadi katika nchi yetu.

Nampongeza mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano,ndugu Jakaya Kikwete kwa upeo wake wa hali ya juu kumteua Mwigulu Nchemba kuwa Naibu waziri wa Fedha.
 

mbeyaman

Member
Sep 28, 2013
97
0
Kwa nini asiwe na ubavu ? Jamaa ana ujasiri wa hali ya juu.Kitu ninachompendea ni mkweli na muwazi linapokuja swala la maslahi ya taifa.
 

samaki2011

JF-Expert Member
Dec 17, 2013
1,775
0
hizo ni kauli za watu waliochukuliwa msukule, mtu akiwa ni msukule huwa hajitambui kwani roho yake, nafsi yake na mwili wake na akili zake ziko under control ya mtu mwingine. Siku tutakapokuwa tumeiondoa ccm ndo utajitambua
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom