Tutaungana na CHADEMA kuikataa Katiba mpya - Lipumba

Tutaungana na CHADEMA kuikataa Katiba mpya - Lipumba

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Mwenyekiti wa CUF Ibrahim Lipumba amesema chama chake hakiridhishwi kamwe na jinsi mchakato wa Katiba mpya unavyoendeshwa kwani inaonekana wazi uko kwa maslahi ya wachache.

Professor Lipumba amesema CUF wanachosubiri ni kuiona Rasimu ya Katiba na endapo kama itatengengenezwa kwa maslahi ya CCM wataungana na CHADEMA,wanaharakati na wote wanaoipinga Katiba mpya kuomba watanzania kuikataa.

Professor Lipumba amesema msimamo wa CUF ni thabiti kuhusu Katiba mpya na kamwe hawatababaishwa.

Source:Nipashe.


IJUMAA, MEI 17, 2013 04:58 NA BENJAMIN MASESE, DAR ES SALAAM

*Yaunga mkono CHADEMA, JUKATA

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimeanika uamuzi wake wa baraza kuu la uongozi huku kikiionya Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuhuwu mchakato wa Katiba mpya na uchaguzi mdogo wa jimbo la Chambani. CUF kimetangaza kusudio la kujitoa katika mchakato wa katiba na kuuungana na taasisi, vyama na baadhi ya Watanzania ambao wamekwisha kuonyesha shaka juu ya mchakato huo.

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba alikuwa akizungumzia maazimio matano ya kikoa cha baraza kuu la uongozi wa chama hicho kilichokaa kwa siku mbili na kumalizika juzi usiku.

Profesa Lipumba alidai Dar es Salaam jana kuwa chama hicho hakijaona nia njema na utayari wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya kuleta katiba iliyozingatia maoni ya wananchi bali ni maagizo ya CCM kwa manufaa ya wachache.

"Tunasubiri rasimu itolewe na kuisoma lakini tayari tunajua yaliyomo ni maagizo ya CCM na CUF tunaishangaa tume ya Jaji mstaafu, Joseph Warioba kushindwa kujijengea historia ya maisha yao katika siasa na kuendelea kukumbukwa kwa wema kupitia katiba hii.

"CUF hakitakuwa tayari kuiunga mkono katiba ambayo haitakuwa na misingi imara ya demokrasia na isiyotokana na maoni ya Watanzania… tutakuwa tayari kuwahamasisha wananchi nchi nzima kuikataa katiba ya maagizo ya CCM.

"Hatupo tayari kuona matumizi makubwa ya gharama za kuukamilisha mchakato ambao kimsingi ni kiini macho. Tunataka rasimu itolewa na kuwekwa hadharani ili wananchi watoe maoni yao kabla haijapelekwa bungeni kupoigiwa kura.

"CUF tuna ushahidi juu ya watu walioingizwa katika mabaraza ya katiba ngazi ya kata na ndiyo maana yamekuwapo malalamiko mengi, tutaungana na wale waliotangulia kuonyesha shaka wakiwamo Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA) na Chadema wanaosubiria hiyo rasimu,"alisema.

Profesa Lipumba alisema katiba mpya inayotokana na wananchi wenyewe itasaidia kujenga dira mpya ya mabadiliko ya uchumi, siasa, muundo wa uendeshaji wa nchi na kuongeza uwajibikaji kwa viongozi.

Alisema ikiwa tume italeta katiba ya kikundi cha watu wachache na wenye dhamana na kuilazimisha kuwa katiba mpya itasababisha taifa kukosa utulivu.

Uchaguzi Chambani

Profesa Lipumba alisema pia kuwa CUF kimemteua Yusuph Salum Hussein kuwa mgombea ubunge jimbo la Chambani-Pemba katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Juni 16, mwaka huu.

Profesa Lipumba alisema Hussein ni miongoni mwa wanachama 12 waliochukua fomu kuwania nafasi hiyo iliyoachwa wazi kutokana na kifo cha Salim Hemed aliyefariki dunia ghafla akiwa katika shughuli za bunge.

Alisema baraza kuu la CUF limeiagiza kamati ya utendaji na maandalizi ya uchaguzi wa ndani ya chama kuhakikisha uchaguzi huo unaratibiwa vizuri viongozi makini waweze kupatikana kwa ngazi zote ambao wataweka mikakati ya ushindi 2015.

Maagizo serikalini

Profesa Lipumba alisema CUF kimegundua nchi ipo katika matatizo makubwa ya mfumo katika kuasisi asasi zitakazojenga demokrasia na kuendeleza uchumi wa kisasa.

"Kutokana na hali hiyo, tunaiomba Serikali kutekeleza miradi ya maendeleo, kuonyesha nidhamu ya matumizi ya fedha za umma, iache utaratibu wa kukopa bila kuwa na mkakati wa matumizi mazuri.

"Serikali iache utaratibu wa malipo kwa mfumo wa stakabadhi ghalani, iache vitendo vya unyanyasaji, dhuluma, ifanye uchunguzi wa matukio ya mashambulio ya viongozi wa dini na madhehebu.

"Itumie busara kutatua mpasuko wa dini unaonekana kuendelea kukua kwa kasi na kuleta chuki na uhasama, kutafuta suluhisho la nani anastahili kuchinja na Serikali ya CCM iwe na utaratibu wa kutoa taarifa sahihi na wakati,"alisema.

Alisema Serikali inapaswa kuhakikisha inaboresha daftari la kudumu la wapiga kura katika kuelekea uchaguzi mkuu 2015.

Kuhusu matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka 2012, alisema ni vema Baraza la Mtihani Tanzania (NECTA) likafumuliwa na kusukwa upya kwa kuwa viongozi waliopewa dhamana ya kuliongoza na kamati zake wamedhihirisha wapo kwa maslahi ya posho tu.

Profesa Lipumba aliitaka Serikali ya CCM kuondokana na ubabaishaji wa kushughulikia sekta ya elimu nchini kwa vile ni hatari kwa kizazi kijacho na uhai wa taifa.


 
Kama anachozungumza ndicho anachomaanisha, basi ninamuunga mkono. Lakini kumbukeni CCM wana hela ya kuweza kurubuni!!
 
huyu CUF si mke wa CCM na akipewa talaka itakuweje?japo wana hoja
 
Safi sana Lipumba, ukiwa na msimamo huo "thabiti" nahisi hiyo "Ndoa" itakwisha, pia next time ukagombe ubunge hapo Tabora, CUF muwe kama CDM mwaka 2000.
 
Vipi kuhusu ndo a yake? mbona kule bungeni hawaungani na wansema chadema hawana nidhamu sasa huo muungano utakuwaje?
 
Lipumba keshaisha anatumika tu sasa na makampuni ya mafuta.
 
Sasa jamani hawa viongozi walioko serikalin wanaohujumu hili swala la katiba ili hali wamewekeza mabilion ya hela!! Kisha wanahujumu mchakato hawaoni huo ni urasimu wa hela za alipa kodi! Kila siku wapo ziarani kutembeza bakili ila matumizi yanakuwa ya ovyo sana hata kwa jambo la msingi kama hili wenyewe wanachukulia easy!!
 
Prof. Baregu wa Chadema ni hizo pesa wanazopata ndio zinamsababisha aendelee kubaki kwenye KATIBA ni malipo Mazuri sana ya UZEENI
 
Kama anachozungumza ndicho anachomaanisha, basi ninamuunga mkono. Lakini kumbukeni CCM wana hela ya kuweza kurubuni!!

Sidhani kama anachoongea ndio msimamo wa chama chake. Ilibidi kwanza ajiridhishe na hili kabla wabunge wake hawajamuumbua tena!
 
Kwa hili namuunga mkono prof. Hakuna katiba mpya chini ya utawala wa ccm! Jaji warioba na timu yake, wanafumbia udhaifu huo ili kuwapa nafasi maccm ili yaweke mambo wanayoyataka wenyewe kwenye katiba yao! Ccm ni janga kwa taifa letu!
 
Prof. Lipumba amesema vizuri isipokuwa hapo kwenye NECTA. NECTA siyo inayo tayarisha mitaala, NECTA haifundishi wanafunzi, NECTA haiandai sera ya ELIMU, NECTA hailipi walimu. Kazi ya NECTA ni kutunga, kusimamia na kusahihisha MTIHANI full stop. Sasa matokeo mabaya ya kidato cha IV NECTA inahusika vipi? Au kusema UKWELI kwamba wanafunzi wame fail ndiyo kosa la NECTA.

Badala ya kuwaambia Kawambwa na Mulugo wajiuzuru yeye anamurukia Dr. Joyce Ndalichako wa NECTA. Nafikiri ile mihadhala ya wanazuoni wa kiislamu kutokana na chuki walionayo dhidi ya Ndalichako imemuathiri.

Kuhusu kupata katiba mpya, chini ya CCM watanzania tusahau kabisa. Hiyo Rasimu itakayokuja itakuwa ya ki-CCM CCM na tutaipigia kura ya HAPANA. Hapa pesa zetu zinatekettea bure, mark my words.

Judge Joseph Sinde Warioba amepoteza hii GOLDEN OPPORTUNITY ya kujijengea historia katika Taifa letu, pale sasa anapoonekana dhahiri kufuata matakwa ya CCM. Pamoja na Watanzania 20% TU kutaka mfumo wa vyama vingi lakini Judge Nyalali alikuwa na GUTS za kupendekeza mfumo wa vyama vingi Tanzania na mpaka leo anakumbukwa kwa UJASIRI wake huo.

Lakini huyu Judge wa Tume ya mabadiliko ya Katiba, Watanzania tumeuziwa mbuzi kwenye gunia!
 
Tabu ya prof ni kigeugeu,wakimuweka kati CCM anabadili mawazo.
 
Ingekuwa aibu kukutana cc ya CUF bila kutup mrejesho! Sijaona jipya ila walichofanya ni kucheza na alama za nyakati kwa kuongelea vitu "HOT" ambavyo ni chuki za kidini, matokeo ya form foo na katiba ambavy vimeshaongelewa na wengine! Kwa mwend huo ccm wanastahili hati miliki!
 
well said prof ila kwa necta siyo kweli dr ndalichako unamwonea tu hana kosa tatizo lipo wizarani.
 
Hongera mh lipumba kwa msimamo huo,maana watanzania wanateitegemea elimu yako kuwatetea,kuwashauri,na kuwaongoza kama wafanyavyo wasomi wenzio wakin dr slaa, tundu lissu ,dr mwakyembe ,zitto kabwe, pr safari na wengineo. Lakini sio kama wafanyavyo akina chenge,werema na anna makinda pamoja na ndungai.
 
Nikisikia vyama vya upinzani kuwa na msimamo mmoja kama hivi nakuwa nafaraja sana na sasa nangojea na vingine kuwaunga mkono
 
Back
Top Bottom