Tutampata wapi Mwalimu Nyerere mwingine wa kuikemea Serikali?

Major

JF-Expert Member
Dec 20, 2007
1,865
2,453
Nakumbuka wakati wa uongozi wa Wa Mzee wetu Ali Hasan Mwinyi. Kuna mahali alifika akatoka kabisa nje ya mstari wa Uongozi, Watanzania wengi walinung'unika sana Mitaani lakini hakuna hata mmoja aliyejaribu kujitokeza hadharani na kuikemea, sisi wana CCM wote tuliufyata,

Ndipo akaibuka Simba mmoja toka nyikani Tena Mwana CCM tena Mwanzilishi wa Harakati za kumng'oa Mzungu Mkoloni na Dikteta, Akasema no! wewe ni Rais wangu nakuheshimu lakini nikiwa Kama baba wa Taifa hili nasema no Imetosha. Akaitisha mkutano na waandishi wa habari pale Kilimanjaro Hotel, kilichonishangaza ni wingi wa waandishi wa habari wa ndani na wa nje waliohudhuria na tena wengi wao wakionyesha kabisa shauku ya kutaka kujua Huyu SIMBA asiyeogopa chochote anataka kuwaambia nini watu wake

Namshukuru Mungu maneno ya Hekima toka kwa Yule SIMBA yalipenya katika Miyoyo ya wale waandishi na Ktk Miyoyo ya Watanzania na Nina Imani yalipenya pia ktk moyo wa Mzee Mwinyi, na kwa kuwa Yule mzee hakuwa na kiburi wala majivuno alijirekebisha kwa kiwango cha Kuridhisha.

Sasa kwa hivi sasa Watanzania tunajiuliza tutampata wapi Rais mstaafu asiyeogopa ili amwambie huyo aliyepo kwamba huko anakoelekea siko, Kama alivyotoka Hadharani Mwalimu Julius Kambarage na Kumwambia Wazi wazi mzee Mwinyi kwamba amepotea njia na Arudi ktk mstari na Mwinyi bila hiyana akarudi ktk Mstari.

Kwa sasa hivi na hali iliyopo ktk vijiwe vyote vya mjini kila mmoja anazungumzia jinsi hali ya Nchi Ilivyo mbaya, kwa sasa kuliko wakati mwingine wowote tangu Tupate Uhuru, Marais wetu wastaafu, please Okoeni hili Jahari, vinginevyo mkichelewa Wote tutazama.
 
Simba gani huyo yeye mwnyewe kwenye utawala wake alikuwa na mapungufu zaidi yawaliokuja baada yake
 
mapungufu alikuwa nayo na hata yeye mwenyewe alikiri, lakini alisema, inafaa tuchukuwe yale mazuri tuyaendeleze na yale mabaya tuachane nayo
 
Tumeshampata mkuu,
Hashimu Rungwe..usiwe na wasi wasi anaendelea kumkemea ila dereva pombe imemnoga haelewi hasikii.
 
Mkuu unakumbuka wakati ule Lyatonga akiwa na wafuasi wengi na baada ya mikutano ya siasa watu walikuwa wakisukuma gari lake, CCM tuliogopa na Tukaamuru polisi waanze kumtwanga na mabom ili kumpunguzia kasi, lakini Mwalimu Nyerere akajitokeza hadharani na akatufundisha kwamba kumzuia ni kumjengea umaarufu. Mwacheni tu watu wambebe. Na kweli Akaachwa na wala hakuleta madhara yoyote
 
Watu huwa wanmponda nyerere..na bahati mbaya sijapata bahati ya kushuhudia utawala wake nikiwa na akili timamu..
Ila kwa mujibu wa historia nadiriki sema hakuna kama yeye..hebu jaribuni kuwaza je hawa ndio wangekuwa awamu yake ingekuwaje..yule mzee alikuwa na mapenzi ya wazi kwa watanzania..alitupenda tokea moyoni hakuwahi kutuibia hata punje..
Nirudi kwenye mada..baba wa taifa alikuwa na ujasiri wa kukemea maovu kwa sababu moja kuu..hakuwa na doa ya ufisadi kwenye utawala wake..hakuwa na mawaa yoyote pindi cha utawala wake ..yalikuwepo makosa madogo ya kisera na aliwahi kuyakiri..
Sasa waliomfwatia waligubikwa na rushwa na madudu chungu mzima kwa hiyo wakitoka madarakani hawana ujasiri wa kuzungumza maana wakithubutu wanaweza mkasirisha aliyeko madarakani akawachoma..
Mfano ni kama wewe baba wa familia ukaopoa mchepuko na kwenda nao gesti..ukiwa gesti ghafla ukahongana na mwanao wa kike.hakika utakosa ujasiri wa kumuuliza unafanya nn.nawe utakiwa mtetezi wake mkuu kwenye maovu yake..hata siku akipata mimba waweza mpatia hela ya kuitoa ili mama asifahamu siri yenu
 
nakupa 5 mkuu,nakumbuka alimwambia Mzee Mwinyi kwamba watu unaowaongoza wanataka kujua wakiamka kesho wafanye nini, na kuwa Nchi lazima iongozwe kwa Mujibu wa katiba uliyoapa kuilinda
 
Kwa tanzania hii hakuna kama nyerere..bado sana.
Hata huyu wanayemfananisha naye hawamtendei haki mwalimu aisee..
Kipindi cha uongozi wa mwalimu hakuelekeza miradi mikubwa ya serikali butiama..
 
Mkuu nakumbuka moja ya hotuba zake wakati wa mkutano mkuu wa ccm wa Kumtafuta mgombea Uraisi awamu ya Mzee Mkapa, Alisema "Nchi inaongozwa na Kiongozi na Huyo kiongozi anaongozwa na Katiba Huwezi kuongoza watu kwa matakwa yako wakati tumekuchagua na tukakuapisha na ukaapa kuilinda na kuitetea katiba, Leo katiba hiyo hiyo uliyoapa kuitetea unaionea aibu, basi Raisi huyo hatufai
 
Madhara ya kuendesha Nchi bila kufata katiba ni Makubwa kuliko viongozi wanavyofikiri, na ndiyo maana sasa hivi kuna matamko kutoka kwa kila mtu, huyu anasema wanyang'anye mihuri huyu anasema wapewe, huyu anasema machinga waondoke huyu anasema wasiondoke, yaani ni sarakasi tupu.
 
Mmh Natoka mafichoni ili niwapashe. Huyu Nyerere munaemsifia ndie alieiuwa miji ya Tanga, Lindi, Mtwara, na Kigoma kwa makusudi na kuibomoa kabisa reli ya kusini. Nchi ilimshinda kabisa yeye uongozi wake ulikuwa kutoa khadithi za kulaani ubepari na kupalilia umasikini Tanzania. Haki ya Mungu watanzania walivaa vipolo na magunia huko vijijini,na dawa ya msuwaki nobe nayo ilikuwa dili kinoma. Sabuni za kukogea zikitoka Zanzibar kuja bongo kimagendo. TV ilikuwa ajabu anayo yeye tu. Huyu akimpiga vita mzee wa ruhsa kwa ruhsa zake. Tumepitwa na Kenya kwa noma zake
 
Bro kumbuka wakati huo uchumi wa nchi nyingi ulikuwa mchanga sana, lakini nijuavyo Mimi, Yule alikuwa ni mpenda haki popote, na alimwogopa mungu, na ndiyo maana hata huko kwa Museveni wanataka afanywe na kanisa kuwa Nyerere Mwenye Heri
 
Watu huwa wanmponda nyerere..na bahati mbaya sijapata bahati ya kushuhudia utawala wake nikiwa na akili timamu..
Ila kwa mujibu wa historia nadiriki sema hakuna kama yeye..hebu jaribuni kuwaza je hawa ndio wangekuwa awamu yake ingekuwaje..yule mzee alikuwa na mapenzi ya wazi kwa watanzania..alitupenda tokea moyoni hakuwahi kutuibia hata punje..
Nirudi kwenye mada..baba wa taifa alikuwa na ujasiri wa kukemea maovu kwa sababu moja kuu..hakuwa na doa ya ufisadi kwenye utawala wake..hakuwa na mawaa yoyote pindi cha utawala wake ..yalikuwepo makosa madogo ya kisera na aliwahi kuyakiri..
Sasa waliomfwatia waligubikwa na rushwa na madudu chungu mzima kwa hiyo wakitoka madarakani hawana ujasiri wa kuzungumza maana wakithubutu wanaweza mkasirisha aliyeko madarakani akawachoma..
Mfano ni kama wewe baba wa familia ukaopoa mchepuko na kwenda nao gesti..ukiwa gesti ghafla ukahongana na mwanao wa kike.hakika utakosa ujasiri wa kumuuliza unafanya nn.nawe utakiwa mtetezi wake mkuu kwenye maovu yake..hata siku akipata mimba waweza mpatia hela ya kuitoa ili mama asifahamu siri yenu
Wengi wanaomponda Nyerere ni wafuasi wa dini fulani wanaodai kuwa eti aliwagandamiza kwa kutetea mfumo Kristo katika utawala wake japo wenyewe hao hao pia wanakiri kuwa hawakuwa na elimu inayotakiwa ili kuweza kupewa nyadhifa kubwa kubwa serikalini. Hotuba yake ndefu na yenye mambo ya msingi sana na inayotakiwa kusikilizwa na kila Mtanzania hasa kwa wakati huu hii hapa. Unaweza kuanzia dakika 8:30
 
Hayati Mwalimu Nyerere namkubali kwa uzalendo aliokuwa nao kwa nchi yake. Ila Mwalimu kama binadamu wengine alikuwa na mapungufu yake. Moja ya tatizo kubwa la Mwalimu ni "Kutambua tatizo na kutolitatua"

Mwalimu alijua wazi kuwa katiba yetu inamapungufu na hilo alilikiri wazi "Kama ikitokea kiongozi anayeamini ndani ya udikteta na akaamua kuitumia katiba kutimiza udikteta wake, basi anaweza" (nukuu isiyo rasmi)

Kwa kuwa Mwalimu aliliona hilo na alikuwa na uwezo wa kulitatua na yeye hakutatu basi tukubali kuwa haya ya sasa ni matunda ya Mwalimu.

Kikubwa ninachoweza kumsifu Mwalimu ni Hekima na Busara zake ambazo zilitosha kuiongoza Taifa ata kama tusingekuwa na katiba na wananchi wangefurahi
 
Nilikua nikisoma kitabu kimoja kinachotoa taswira ya nchi miaka ya 1961-1967 yaani baada ya Uhuru na kabla ya Azimio la Arusha.

Kimeandika mengi ila kwa ufupi Mwalimu na sera yake ya Ujamaa ilipunguza kwa kiasi kikubwa sana unyonyaji wa kikoloni ulikua umeacha makucha baada ya Uhuru. Viwanda, Mashamba, Hospitali na Shule nyingi zilimilikiwa na wakoloni. Maduka makubwa na makampuni yalikua ya wageni. Tusidanganyike maendeleo sio GDP pekee, mwalimu aliwekeza katika rasilimali watu. Wazee wa leo watajisifia walikua na maadili,utu na nidhamu haya ni matunda ya sera za Mwalimu.

Baada ya Mwalimu sera zimejikita katika "vitu" zaidi kama ujenzi wa barabara, shule na maabara zimesahau watu wanaotumia hivyo vitu. Madhala yake ni kupungua kwa ubora wa elimu, maadili, utu na heshima kwasababu jamii nzima inaangalia una nini, unaingiza sh ngap n.k
 
Kuna watu wanashindwa kutofautisha wakati wa Mwalimu na wakati uliopo sasa. Ila kuwakumbusha tu ni kwamba wakati huo nchi nyingi zilikuwa ni changa sana, na hata population ya watu ilikuwa ni kidogo sana. Nchi ilikuwa ni masikini kabisa, yaani Mwalimu alianzia Ground zero.
 
Bro kumbuka wakati huo uchumi wa nchi nyingi ulikuwa mchanga sana, lakini nijuavyo Mimi, Yule alikuwa ni mpenda haki popote, na alimwogopa mungu, na ndiyo maana hata huko kwa Museveni wanataka afanywe na kanisa kuwa Nyerere Mwenye Heri
Na uchimi ulidorora haswa baada ya vita vya nduli..mzee alikuwa na dira ya kuiendeleza hii nchi..sema bahati mbaya vijana wake walikuwa wanfki na wasiomwelewa hata kidogo..
Alitumia fedha kidogo aliyonayo kuwapatia elimu bora tena bure ili waje wasaidia watanzania baadae..ila ndio yanekuwa majizi na kuona wengine malofa..
Mwacheni mwalimu aitwe mwalimu hakuna mfanowe kwenye hili bara..we jiulize kati ya mwalimu na mandela ni nani kalipigania hili bara? Jibu ni nyerere.lakini jiulize ni kwa nini heshima kubwa anapatiwa mandela..jibu ni kwamba mwalimu aliwatumulia mbali na biashara zao akazitaifisha ilihali mandela alipatiwa uhuru wa kuongoza serikali ila nahisi waliingia makubaliano ya siri kuwalinda na kulinda maslahi ya weupe..na ndio maana wanimba sana sifa zake kuliko za mwalimu wetu mpendwa..
 
Kama Kristo alivyosema amri kuu ni Upendo..nami pia naamani sifa kuu ya kiongozi ni uzalendo...
Rais pekee aliyekuwa mzalenda tanzania ni nyerere...hebu litazame azimio la arusha kwa undani ndio utatambua kipimo cha uzalendo wa mwalimu..na kama sio vita ya idd amin na kuanguka kwa ussr hii nchi ingekuwa mbali sana..
Maana mwalimu aliifanya tanzania ya viwanda kwa vitendo si kwa maneno
 
Back
Top Bottom